Binafsi mtu anayenipa kadi ya mchango wa sherehe namwona kichwani hamnazo

Binafsi mtu anayenipa kadi ya mchango wa sherehe namwona kichwani hamnazo

Tatizo kuna maeneo kama kanda ya kaskazini ukiandaa sherehe ukaalika watu bila wao kuwa wamechanga hawaji, wanaona umewaona ni masikini hivyo umewaita ili uwalishe bure ( dharau) ndio maana hata matajiri huchangisha
Dunia duara!!!!!
 
Acheni uchawi sherehe ni watu,sasa mnataka mje kula bila kuchangia,au uchange usije ili shughuli idode,huo ji utamaduni wetu sioni tatizo hapo
 
Ila kweli tunatakiwa kubadilika ukitaka kuoa jipange usisumbue watu kuchangia sherehe yako, alika watu wa muhimu tu wakihudhuria watu 20 tu ambao hujawaomba mchango wakala vzuri wakasherehekea vzuri bila fujo kistaarabu imeisha hiyo acha kusumbua watu unachangisha watu 300 alaf mnaachana ndan ya miez 6 we kiazi nini?
 
hapa kwenye hili suala imekua tatizo kidogo kwakua maisha magumu na watu wanataka kufanya vitu vikubwa zaidi ya uwezo wao.
Mimi nilishakataa habari za michango ya sherehe kwakua pia siendi sana kwenye hizo mambo na hata nikiwa na jambo langu naalika ndugu kadhaa marafiki kadhaa imeisha hiyo na hakuna atakaepewa kadi ya kuchangia utaalikwa hutaki basi hamna ulazima.
Unakuta familia inataka kufanya sherehe ya 30-40m ila Wao hawana hata 5m sasa unajiuliza hela zote hizo zipatikane kwenye kamati na michango hivi kweli si bora uangalie mfuko unasemaje alafu ufsnye sherehe ndogo nzuri . Na kuna katabia eti usipo changia na kushiriki sherehe za watu na wao hawata kuja zako [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mm nachojua nashiriki misiba kwakua ni jambo linalotia faraja kwa muhusika ila sherehe hata nisipoenda nafsi hainisuti wala sijiskii vibaya.
Wapo watu naweza wachangia ila sio kile kiwango wanachotaka yaani kwenye sherehe nimechanga hela kubwa ni 30k basi mbali na hapo sin msaada mwingine na nachangia ila kufika kwenye sherehe ni nadra
 
Mi nachangia ndugu mwanandugu tu kwa upande wa sherehe. Ila kwa masuala ya shida au matatizo nachangia wote ndugu na wasio ndugu.
 
Kama mtu unaweza kunywa bia za elfu 10, au 20, au hata 50 kwa mwezi kwanin nisichangie harusi

Kama unaweza mhonga mchepuko au mwanamke kwanin nisichangie life is too short ukipata nafasi na uwezo enjoy

Kwa sis Wanaume unaweza ukawa unalipia kingamuz lakin hata usipate mda hata wa kuangalia sababu unaondoka asubuhi unarudi usiku Sasa kwanin usichangie harusi
Weye changia.Ila mimi mnialike nitaleta zawadi.Halafu,ni hiyari yenu kunialika kama ilivyo hiyari yangu kuhudhuria.
 
Sema huna hela tu kijana nasio kutoa visingizio.

Mtu mwenyewe unakaa chanika,kutwa kudandia madaladala hyo hela ya kuchangia unaitoa wapi ikiwa kula yako yenyewe tu ya tabu
Heshimu chanika mkuu.
Unaijua chanika?
 
Sherehe hujachangia nani aje raha ya sherehe uchangie,

mim mwenyewe sipendi kwenda kwenye sherehe ambazo sijachangia

Sherehe ni pongezi
Kama unatamani kuchangia utachangia bila kuombwa tena Mimi naweza kusema nilichangiwa sana na kwa upendo mkubwa na waliohudhuria kwenye sherehe yangu japo sikuomba michango
 
Sherehe ni pongezi
Kama unatamani kuchangia utachangia bila kuombwa tena Mimi naweza kusema nilichangiwa sana na kwa upendo mkubwa na waliohudhuria kwenye sherehe yangu japo sikuomba michango
Kuombwa Tena naumesema hauhitaji michango kadanganye watoto wadogo
 
Back
Top Bottom