Binafsi mtu anayenipa kadi ya mchango wa sherehe namwona kichwani hamnazo

Binafsi mtu anayenipa kadi ya mchango wa sherehe namwona kichwani hamnazo

Pamoja sana

Binafsi nilikataa kuchangiwa sendoff niliwashinda wapinzani wa katazo langu ambao ni ndugu na jamaa waliokua wanang'ang'ania ati nichangiwe sababu wao wamechangia

Unataka kuoa au kuolewa weka mipango yako sawa kadri ya uwezo wako sio kadri ya mifuko ya wengine
Kweli kabisa
 
Ukiwa huna pesa kila mchango utaona ni mzigo, sasa rafiki yangu anaoa nisiende harusini kumpongeza? Niende kula harusini bure? Urafiki ni kukutana bar na kununuliana bia?

Huwezi ukawa mvivu wa kusoma magazeti eti ukapenda kusoma vitabu, kama huwez kuchangia sherehe hata hyo misiba au elimu hutoweza. Na mkono usiotoa kitu ni ngumu kupata kitu.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Angalia hata kwenye jamii nenda kwenye misiba, harusi, kusaidia watu angalia wachangajia ni wale wale kutoa ni moyo kama huna utakua ni mtu wa sababu nyingi
 
Angalia hata kwenye jamii nenda kwenye misiba, harusi, kusaidia watu angalia wachangajia ni wale wale kutoa ni moyo kama huna utakua ni mtu wa sababu nyingi
Misiba sawa.Harusi mjipange kabla ya kuwaza kula ubwabwa.
 
Hapa nina kadi zaidi ya 14 ambazo zinatakiwa kuchangiwa. Na mbaya zaidi ni kwamba hizi kadi majority zina limit ya minimum contribution ya 70K.

Nikisema nilipie zote kwa kiwango cha 70,000 ina maana mara 14 hapo unaweza pata kiasi natakiwa kutoa.

Hii michango inatufarakanisha sana na watu wetu wa karibu kiasi kwamba hata heshima anayokupa inategemea na kiasi utachomchangia.
 
Labda waweke kiambatanisho mfano, 5000 mwaliko tuu, 10000 unapata na soda2, 20000 soda na ubwabwa maharage tuu, 30000 ubwabwa nyama, 100000 vyakula na soda/ bia.
Kwahiyo mchangiaji unachagua menu yako kabla ya kuchanga.
Hiyo imekaa kisomi
 
Mimi nafikiri kama kipato chako hakiruhusu na tena umemwambia mapema mwenye sherehe kwamba hautaweza kuchangia hautaona tena simu wala meseji zake za kukuomba michango

Sidhani kama kuna mtu atakulazimisha uumchangie.
 
Sherehe na misiba ni mambo yanahusu watu yaani ndugu, jamaa na marafiki kwa kifupi ni mambo ya kijamii. Kwa hiyo kuchangia ni jambo la kawaida.

Kusomesha, matibabu, mtaji hilo ni jukumu lako binafsi hayo ni mambo ya kifamilia

Unataka nani alipe ada ya mwanao na wewe ndiye uliyemwaga uno kumleta duniani
 
Back
Top Bottom