Binafsi mtu anayenipa kadi ya mchango wa sherehe namwona kichwani hamnazo

Uko sahihi 100%.
 
Sherehe hujachangia nani aje raha ya sherehe uchangie,

Mimi mwenyewe sipendi kwenda kwenye sherehe ambazo sijachangia
 
Tafuta pesa ili ufanye sherehe kubwa unayoitaka,na sio kusubiri hela za wanaume ili ukaolee.
Kuna matajiri Wana hela na still wanachangisha kwanin ili watu wawe comfortable

hivi mwanaume unavaa unapendeza unaenda kwenye sherehe unakula na kunywa huku hujachangia hata mia unajisikiaje

Mimi siwez nenda kwenye sherehe ambayo sijachangia ni bora nisiende sitakua huru
 
Sisi watanzania tumezoea kusaidiana kwenye shida na raha km huna unasema tu sasa makasiriko na kuona watu hawana akili inatoka wapi ....au ww mkimbizi nn umetoka kwenye jamii ya watu poli huko wana rohoo mbaya km shetani.
 
Kwahiyo kuomba mchango wa harusi ndo kukosa akili.

Wewe na akili zako mpaka saivi umeisaidia nini jamii inayokuzunguka tu

Si kila jambo duniani hapa lazima ukubariane nalo wewe na likiwa tofauti ulione la kijinga..!
 
Mimi nadhani "kuchangisha watu" ni umasikini mkubwa zaidi ya "kukataa kuchanga".

Tutafute hela ili tusichangishe watu kwenye mambo madogo madogo kama harusi.
Watu wajifunze kujitegemea/kusimamia mambo yao.Nitawachangia wasiojiweza na wenye nia thabiti ya ndoa.Ujanjaujuanja haufai.Kitonga kipigwe marufuku.
 
Watu wajifunze kujitegemea/kusimamia mambo yao.Nitawachangia wasiojiweza na wenye nia thabiti ya ndoa.Ujanjaujuanja haufai.Kitonga kipigwe marufuku.
Kama mtu unaweza kunywa bia za elfu 10, au 20, au hata 50 kwa mwezi kwanin nisichangie harusi

Kama unaweza mhonga mchepuko au mwanamke kwanin nisichangie life is too short ukipata nafasi na uwezo enjoy

Kwa sis Wanaume unaweza ukawa unalipia kingamuz lakin hata usipate mda hata wa kuangalia sababu unaondoka asubuhi unarudi usiku Sasa kwanin usichangie harusi
 
Hatamimi ndio falsafa yangu.
 
Bora hata hiyo kidoogo! inayonishangaza zaidi na sitakaa nichange ni ile mtu anafikisha kwa mfano miaka 5, 10 15... ya ndoa halafu anachangisha watu afanye sherehe! ujinga kabisa, wewe ndiye unayesherehekea, gharamia kila kitu ili uite watu uje ufurahi nao kwa kutimiza hiyo the so called yako! sio watu wakuchangie, alaaa! halafu unaletewa na zawadi wakati mwingine unakasirika kwa nini flani hajakuletea zawadi huo ni ung'ong'olo in "masikiopopotz voice"
 
Hapo sawa, hata Mimi nashauri watu wafanye sherehe kulingana na uwezo walio nao.
 
Tatizo kuna maeneo kama kanda ya kaskazini ukiandaa sherehe ukaalika watu bila wao kuwa wamechanga hawaji, wanaona umewaona ni masikini hivyo umewaita ili uwalishe bure ( dharau) ndio maana hata matajiri huchangisha
 
Africa ni wachawi sana!! Hatusaidiani kwenye mambo ya msingi bali tunabebana kwenye masuala ya kipumbavu! Ndio maana wazungu wanatubagua sometimes kwa sababu mambo mengi tunayoyafanya ni ya kipumbavu na si kimaendeleo,
 
"Usiache ambachao kwa msala upitao" binafsi natoa sana sema siwez kuhudhuria wala Mimi binafsi kuchangisha mtu....ukiniletea kadi means umeniheshimu na kuona kwamba ninao uwezo basi sina shaka kuchangia ila sitoweza kuhudhuria binafsi ...nitashiriki jambo lifanikiwe tu maana kila mtu na imani yake nilishawahi kushiriki harusi ya jamaa mpaka hatua ya kupamba ukumbi ila mda wa sherehe nilisepa nikarudia nae asubuhi kutoa mapambo na kuondoa vitu kama viti..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…