Binafsi siwezi kuajiri dada wa kazi nyumbani kwangu

Binafsi siwezi kuajiri dada wa kazi nyumbani kwangu

Kwa utafiti wangu mdogo nimegundua watu wengi hasa wanawake huleta dada wa kazi ndani ili kujionesha ati wana pesa Kwa kuwa wana wasaidizi hawa.

Hivi hawa wadada wa kazi wanafanyaga jambo Gani la maana au gumu ambalo mwanamke asilifanyaje.
Yaani kulea, kulisha na kufulia mtoto hadi uajiri mdada wa kazi.

Wanawake kiasili ni wazazi na walezi
Kama hawezi kulea basi hafai kuwa mke wa mtu.

Kwangu sitaki dada wa kazi hata iweje, mwanamke aache kila kitu alee mtoto.

Hawa dada wa kazi ni makatili sana, wanalisha watoto vinyesi, hawawapi chakula n.k

Wanawake utawakuta hata hawako busy , wapo tu wanaajiri hawa mabinti kama fashion
Mkuu ukiwa na uchumi mzuri hilo linawezekana lakini kama na wewe ni wale wa tusaidiane majukumu basi mdada wa kazi kwenu itawalazimu tu
 
Chukua mdada then fanya kumlea kama ndugu yako sio unamtesa kama mbwa . Mchukue kama msaidizi wa nyumbani tena unamchukulia kama mwanao au ndugu yako ,ikiwezekana hata kumsomesha fresh .
Hapo ndo utakosea kabisa mkuu, hawa wadada wa kazi kinachowatesa ni kama vile wana roho inayo waongoza kufanya ujinga.

Ukimjali sana = makosa.

Ukimtesa sana = makosa.

Kuwa natural. Usimtese wala usimjali sana. Kaa kati kwa kati
 
Bila msaidizi dah, muhimu aishi bila kunyanyasika, apewe stahiki zake na ikiwezekana akitoka kwako awe na cha kujivunia! Mke alienda shule tena vuzuri kabisa, hawezi kutumia elimu yake kunipikia..after all I can cook!
 
Tuna share mkuu mwasibu
Usiwe serious sana, mtani wangu
Sharing yako ingeeleweka kama ungewasemea wanaokuwa na beki3 bila sababu ya msingi na uhitaji kuliko kuongea generally. Kwa familia ya kisasa ni nadra sana kutohitaji beki 3. Hata kama mkeo ni mtu wa nyumbani,kuweka nyumba katika hali ya kuvutia beki 3 anahitajika, ndio maana wakaitwa wasaidizi. Sasa mkeo atafanya kila tone la kazi, si atakuwa hoi sana hata kukupa mzigo usiku itakuwaje
 
Hapo ndo utakosea kabisa mkuu, hawa wadada wa kazi kinacho watesa ni kama vile wana roho inayo waongoza kufanya ujinga.


Ukimjali sana = makosa.

Ukimtesa sana = makosa.


Kuwa natural. Usimtese wala usimjali sana. Kaa kati kwa kati
Tumeishi na mdada wa kazi mpaka kaolewa ila tuna undugu nae kwa mbali maana katoka sehemu moja na baba yetu, alisomeshwa computer ngazi ya cheti, alikuja kuolewa baadae kidogo muda huo baba alikuwa kashapata wajukuu.
 
Back
Top Bottom