Kuna mambo kadhaa yanatia shaka kwenye stori hii, kiasi kwamba yanaonekana kuwa ni hypothetical, hayana ukweli
MOJA: Ticket kukosekana Dar es Salaam halafu kupatikana KIA, hii ni paradox
MBILI: Ticket moja tu kupatikana KIA, na si mbili. Another paradox
Binti huyu alikuwa anajua nini alikuwa anafanya, na possibly siku anakamatwa haikuwa mara yake ya kwanza. Ndiyo maana alifungwa
Miaka takriban 7 binti yuko ndani lazima wapelelezi watakuwa walijiridhisha kabisa kuwa alikuwa ameshakuwa mshiriki kwenye biashara hiyo. Hakuna watu waangalifu kama wapelelezi, na hasa wanapokuwa wanafanyia kazi kesi ya mtu ambaye si adui wa mtu binafsi, bali wa JMT. Angalau unapokuwa unashtakiana na mtu mwingine, kwa bahati mbaya wakati mwingine inaweza ikatokea mwenzako akakuzidi hoja za mdomoni mahakamani wakati kumbe uko innocent halafu kuzidiwa kwako huko kukawapelekea wakaamua kulingana na ushahidi ambao mwenzako ameutoa na unaaonekana una-sound zaidi kuliko ule wa kwako, wakati kumbe uko innecent ila ni bahati mbaya umezidiwa hoja tu. Tofauti na unapokuwa wewe umeikosea Jamhuri, huwa wanajiridhisha kabisa kuhakikisha kuwa Jamhuri hawaionei, na wewe pia hawakuonei.
Binti angekuwa hajui kitu kabisa kama ulivyoeleza wewe hapa, na mamlaka za upelelezi zikajiridhisha hivyo kwamba alikuwa hajui chochote kabisa kuhusiana na biashara hiyo, angeishia rumande tu na wala asingefungwa.
Kwa inavyoonekana hapa kwenye stori yako, binti huyu alikuwa anajua kabisa na possibly alikuwa ameshafanya mara moja au mara mbili na kufanikiwa, na hivyo siku hiyo nayo pia alikuwa anajua kuwa atafanikiwa.
Kujua huku ndiko kulikopelekea asiwaage wazazi wake. Haiingii akilini kwamba mtu umepata mchumba wa nje tena wa uhakika, unakwenda kutambulishwa kwao halafu asiwaage wazazi wako, badala yake umuage wifi yako tu. Wifi huyu naye ndiye aliyemponza kwa sababu inaonyesha angalau kulikuwa na cheche zilikuwa zinamfikia pasipo wazazi wa binti kujua