Binti amkataa Baba mlezi siku ya Harusi, ampa heshima zaidi Baba mzazi.

Binti amkataa Baba mlezi siku ya Harusi, ampa heshima zaidi Baba mzazi.

ukiwa na huruma kwenye hii dunia ujue kuna siku moyo wako utaumia sana... hv unapata wapi ujasiri wa kulea mtoto wa mwanamme mwenzio... maisha mafupi sana tafuta pesa zikusaidie uzeeni unalea litoto la watu the end of day halikukumbuki..
Kwa upande mwingine kuna wanaolea na kuja kuona matokeo chanya. Ni kwa sababu tu ubaya huvuma kuliko uzuri ndiyo maana husikii. Kwa mfano kwenye hili tukio, kama huyo baba mlezi asingeachwa basi kuna possibility kubwa hii thread isingefunguliwa.
 
Lazima liwakute.
Ukimuumiza mtu asiye na hatia malipo yake utayapata hapa hapa duniani kabla hujaondoka.
Limkute kwani amefanya kosa gani? Mtu kumtambulisha baba mzazi ndiyo iwe sababu ya kupata laana,? Hivi nyie watu mkoje! Ulitaka adanganye kuhusu babake mzazi?
 
Baba mzazi alikuwepo na alikuwa akihudumia vizuri Tu , ambane huyo single Maza amueeleze vizuri ,

Mwisho wa siku atajikuta hata watoto anaofikir ni wake basi na hao yeye NI mlezi Tu.
 
Hii habar Yako inatia mashaka hiyo ya kusema baba mzazi kaibuka tu siku ya harusi na kupewa kipaumbele ni ngumu kuamini, pia ni ngumu kama mtoto umemlea vizur Toka akiwa mdogo alafu aje akukatae ukubwani binafsi naona Kuna vitu umeviruka kwenye hii habar Yako.
 
Unaweza kuta huyo baba mlezi aliwahi kumuomba mechi huyo binti na kujiharibia heshima. Mwanamke kuolewa na wanaume wengine wakiwa na watoto hasa wa kike, wanapobalehe huwa wanapitia mambo mazito. Ninazo shuhuda nyingi za wababa wa kambo kuwabaka watoto wao wa kambo hadi wengine kuzalishwa kabisa.
 
Kwema Wakuu!

Hii inavunja moyo kwa wanaume walioamua kuoa single Mothersl.
Haiwezekani binti umelelewa tangu ukiwa mtoto, ukasomeshwa na Baba mlezi(wakambo) ukamaliza mpaka chuo cha usimamizi wa fedha.

Miaka yote huyo Babaako mzazi hakuwepo. Hakujua unakula nini wala unavaa níni. Wala hakuonyesha kujali,

Umefikisha miaka 25 ndio anajitokeza.
Siku ya harusi unampa heshima kipaombele huku ukimpuuza baba wa kambo aliyekulea.

Nimeumia sana. Hii sherehe imefanyika jana jioni.
Mzee wa Watu katia huruma kweli. Mama mtu naye ni kama hakuonyesha kujali zaidi ya kufurahia sherehe ya binti yake huku aliyemlea sura yake ikiwa haina furaha.

Hata kutambulishwa tuu.

Aiseeh!

Hata kula sikula nilirudi kula makande yangu.

Hekima ni kitu muhimu sana.

Jioni njema
Huyo mtoto hajitambui! Alitelekezwa halafu analeta nyodo?
Pole kwa bwana harusi, maana kaoa mwanamke anayepokea ushauri mwingi KUTOKA kwa mama takezazi zaidi. Ndo maana unajuta Baba mlezi hakifurahia Hilo tukio
 
Back
Top Bottom