Binti Ana Ujauzito wa Miezi 3, Sasa Wazazi Wake Wanataka Nikae Naye—Lakini Bado Sijajipanga

Binti Ana Ujauzito wa Miezi 3, Sasa Wazazi Wake Wanataka Nikae Naye—Lakini Bado Sijajipanga

Habari za muda huu wakuu mimi ni kijana wa kiume
Miez minne iliyopita nilianza uhusiano na binti mmoja jirani na ofisini kwangu. Ni binti mdogo miaka 22 na bado anaishi na wazazi wake.
Ishu ikatokea binti nimempa ujauzito na sasa una miezi mitatu juzi nimeitwa kwao mama yake anataka kunikabdhi binti nikakae nae kwangu hapa anasubiliwa baba yake ambae yupo safarini kikazi arudi mchakato uanze.

Sasa ndugu zangu mimi bado sijajipanga kuowa mshahara wangu ni laki 6 tu na sina kitega uchumi kingine naishi kwenye chumba kimoja tena kisela sina kijiko wala kikombe. Ntawezaje kujivika majukumu ya kuishi na mtu nawaza malengo yangu yatatimia kweli je siku nikikosa kazi na tayari nina familia inanitegemea. Ushauri wenu ndugu zagu hapa nimeshaambiwa na mama mkwe inabidi tuanze kliniki nachoka ndugu zangu. Naombeni ushauri ni kipi nifanye hapa au wenzangu mliopitia hali kama hii mliwezaje kusarvive.
Kwanini ulipiga kavukavu? Kwa maelezo yako hata hio kazi ya laki 6 huna ni msela wa mtaa tu 😂 saiv wewe ni baba mtarajiwa amsha akili
Ila genye 😂 😂
 
Kwanini ulipiga kavukavu? Kwa maelezo yako hata hio kazi ya laki 6 huna ni msela wa mtaa tu 😂 saiv wewe ni baba mtarajiwa amsha akili
Ila genye 😂 😂
Nimecheka sana aseeh
 
Umeongea ujinga. Kila mtu atalipwa kwa anachokifanya. Yeye analilia juu ya k ya huyo binti anamgeuza anavyotaka alitegemea yatatokea mahindi?.

Pili huyo binti amchukue aishi nae tu. Kwa familia zetu nyingi kuoa hakuna kujipanga. Utajipanga ukiwa ndani na mkeo.

NA ANA BAHATI TAYARI ANA KAZI YA KUINGIZA LAKI 6 KWA MWEZI. SISI WENZIE TULIANZIA BILA BILA JOBLESS. TATIZO VIJANA WA SIKU HIZI NI WAOGA HALAFU WANAPENDA TAMU ASAHAU HATA KINACHOFUATA

AKILI YA KUIPANGILIA HIYO LAKI 6 ATAIPATA YEYE MWENYEWE AKIANZA MAISHA NA MKEWE. NA ATAIPANGILIA VIZURI.
TATIZO WAKIMUACHIA TU AJIPANGE KAMA ANAVYOSEMA UJUE YULE BINTI IMEKULA KWAKE,HATAMUOA KAMWE.
Nisamehe kwa huu ujinga nilioubwabwaja mkuu 🙏
 
Unachokikwepa sasa kipo pale pale mkuu kubali kubeba majukumu kama mwanaume kubali uhalisia na toa hayo mawazo ya kutoa hiyo mimba. Kwa sasa punguza matumizi yasiyo ya lazima na ujitahidi kuweka akiba zaidi.
 
Unachokikwepa sasa kipo pale pale mkuu kubali kubeba majukumu kama mwanaume kubali uhalisia na toa hayo mawazo ya kutoa hiyo mimba. Kwa sasa punguza matumizi yasiyo ya lazima na ujitahidi kuweka akiba zaidi.
Shukran sana mkuu nimekuelewa vzr
 
Kwahiyo kakabidhiwa majukumu bila kupenda😁

Wazazi walitazame hili la kumkabidhi ma bint zao Kwa kigezo Cha mimba.

1 September: "binti ananipenda kweli na ananiona mimi ndio kama mzazi wake"

Leo hii: "binti hanipendi na hajawahi kuonesha upendo kwangu. Anampenda bwana mwislamu"

Iko shida sehemu 😀
 
Laki tatu za mahitaji ya nyumbani watu wawili inatosha kabisa

Na unasevu vzr tu

Kama ungejua hujajipanga ungepigia mfuko lkn kama ulikubali ulie peku


Mpokee uishi naye
 
wakati unamkaza akili zako zilikuwa wapi?,,,,, 4 months na mimba juu...... washirikishe jamaa wa karibu unaowaamini, omba umtunze akiwa kwao, simamia hilo....... je mimba ni yako kweli dogo?.........kubambikiwa ndio style ya wasichana kwa sasa......kuwa makini......wote wawili ujana bado HAMJAUFAIDI......
 
Back
Top Bottom