Binti mdogo anayemfungia ndani Mama yake mgonjwa aliyepooza kutwa nzima na kwenda kutafuta pesa za kumuhudumia inaumiza wengi mtaani

Akipata kitu Cha kumtoa nje, nani atamwangalia wakati wa mchana mjukuu na Binti wanapokya hawapo nyumbani?
jirani anaweza fanya hiyo kazi nafikiri maana ni kitendo cha dakika kadhaa kumtoa nje endapo atapata kiti cha kusukuma
 
Duuh asee kuna siku jamaa alisema kwa uchungu siku akimwona mungu atamuuliza kwann wengine wanaishi maisha ya mateso kwann unampa ulemavu maskini asiye jiweza kwann Mungu ...hata mimi bado najiuliza sana uwepo rehema za mungu na bado maisha duni. mungu anafurahia nini kutizama mtu anateseka kiasi hicho???
 
serikali yetu inahangaika kuhudumia watu wenye uwezo kama wasanii ili mradi kupata attention ya watu.
 
Weka namba za simu either ya kwako au huyo dada ili watu waweze kumsaidia,weka picha ambayo haitadhalilisha bali itaonyesha uhalisia ili watu waweze kuguswa na kusaidia.Namba yako pia ni muhimu ili uweze kutoa msaada utakaohitajika kwani kuna watu huo uwezo wanao,hata kama hawana basi wale wenye kidogo wataweza kusaidia kwa chochote...
 
Habari hii ni muhimu sana.
 
Video please
 

Watu wengine hupitishwa ktk magumu ili wewe upate kumshukuru na kumuabudu Mungu
 
Watu wengine hupitishwa ktk magumu ili wewe upate kumshukuru na kumuabudu Mungu
Asee kweli atese mtu mwingine ili yeye aabudiwe kweliii hii ni sawaa ...kwann asitumie mbinu nyingine kujipatia hizo ibada kuliko kitesa wengine asee...
 
Cha kufanya :

  • weka location wanapokaa.
  • weka namba ya mhusika.
  • watu wana utayari wa kusaidia..
  • uswahili umekuwa mwingi
 
Imeniuma sana, maisha tunayo ishi watanzania niya uchungu Sana. Kuna watu wanaisha kwa tabu sana na huzuni nyingi.
 
alafu kuna jamaa leo hii ameishaingiza mil 50 na ushee na analalamika maana alitegemea mil 100 nakuendelea, wewe massawe kuja usome hii ujifunze kitu, usijione mungu mtu.
 
Halafu utakuta fisadi limekaa baa viti virefu anapiga bia ya bei mbaya!! Ombi langu, nawaomba watu wa namna hiyo wajaribu kutoa mchango kwa mateso kama haya..
 
Km inawezekana tupate mawasiliano ya binti tumsaidie chochote.

Cha kufanya :

  • weka location wanapokaa.
  • weka namba ya mhusika.
  • watu wana utayari wa kusaidia..
  • uswahili umekuwa mwingi
Nilikuwa nasubir niombe ridhaa yake kama atakubali kuweka namba yake mtandaoni. Amekubali na ntafanya hivyo pale juu kwenye uzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…