Binti mdogo anayemfungia ndani Mama yake mgonjwa aliyepooza kutwa nzima na kwenda kutafuta pesa za kumuhudumia inaumiza wengi mtaani

Binti mdogo anayemfungia ndani Mama yake mgonjwa aliyepooza kutwa nzima na kwenda kutafuta pesa za kumuhudumia inaumiza wengi mtaani

Ni
Peleka hii habari kwenye vyombo husika, wao ndo wataleta taarifa official nje na hapo ni UTAPELI
Nimeshea hapa nilichokutana nacho pamoja na kutoa wito kwa serikali kuangalia namna ya kuwasiaidia wagonjwa wa muda mrefu kama hawa na wala huyo binti hakunituma hapa kuomba chochote. Binti karidhika na maisha anayoishi
 
Serikali za mtaa, kata wapo wapi wao ndo wapo karibu zaidi na jamii na watakuwa wanalijua hili , wanafanyaje kazi zao?
 
alafu kuna jamaa leo hii ameishaingiza mil 50 na ushee na analalamika maana alitegemea mil 100 nakuendelea, wewe massawe kuja usome hii ujifunze kitu, usijione mungu mtu.
Kila mtu anakula kulingana na kipato chake, maisha lazima yaendelee
 
Ni Binti mdogo mwenye umri wa miaka 23,na mwenye mtoto mmoja Familia hii haina Baba kwani baba yao alishafariki Miaka mingi iliyopita na kijana aliyempa mimba binti alimtelekeza tangu mtoto akiwa ana miezi 6.

Mama wa huyu binti ana umri wa miaka 63 alikuwa mzima kabisa tangu kuzaliwa huku akifanya vibarua vya hapa na pale lakini miaka sita iliyopita ghafla alipata tatizo hili la kupooza viungo vya mwili, ulimi kuwa mzito na hivyo kushindwa kuongea vizuri, pamoja na kuzimia mara kadhaa kila wiki tatizo linalooendelea hadi sasa.

Kutokana na uwezo duni wa hii familia walishindwa kumpeleka Hospital kubwa kwa uchunguzi zaidi

Binti huyu amepangisha chumba kimoja kidogo akiwa yeye, mtoto wake wa kiume na mama yake huyo huku pembeni kukiwa na Ndoo yenye mfuniko wake ambae mama huyo hutumia kama choo usiku na mchana.

Alfajiri binti hujihimu kuandaa chai kwa ajili ya mama na mtoto wake ambae nae huenda shule na kumfungia mama yake ndani huku ufunguo akiacha kwa jirani hadi mwanae huyo ambae yuko la kwanza atakaporudi mchana na kumpa bibi yake chakula kilichopikwa usiku wa jana yake kwa ajili ya mlo wa mchana, hapo watajifungia ndani wote hadi binti atakaporudi saa moja usiku toka kibaruani.

Mara kadhaa bibi huyo amekuwa akizimia humo ndani na mjukuu huyo humwacha hivyo hivyo hadi fahamu zitakaporejea. Binti hiyo nilipata nafasi ya kumuuliza anagunduaje kama mama yake alizimia mchana na kunijibu kuwa hugundua hilo kutokana na kinyesi kutapakaa kitandani au chini au majeraha atakayomkuta nayo pindi arudipo jioni..

Kama kuna Umuhimu wa kuweka picha ya huyo Bibi mgonjwa basi ntaweka hapa.

Na hata kama kitapatikana wheelchair ♿ kwa ajili ya kumtoa nje wakati wa kuota jua pia itakuwa msaada mkubwa kwenye familia hii.

Wito wangu kwa Serikali iangalie Namna ya kusaidia aina hii ya wagonjwa kwani wapo wengi wanaopitia tabu na inatesa sana familia kwa kuwaletea umaskini na usongo mkubwa wa Mawazo.

Update :
Wengi naona wametaka namba ya binti na kabla sijafanya hivyo niliomba ridhaa ya binti kwanza na Amekubali.
Namba yake hii pia ipo whatsapp unaweza piga video call au picha kwa ajili ya kumuona mamake na huyo binti. 0685 52 86 30
Hbr za asubuhi. Kwa kuwa nimeona, nachukuwa wajibu wa kuwasiliana na mhusika Ili nijue iwapo kuna hatua za awali zilichukuliwa na kama bado zifanyike ikiwemo za ustawi wa jamii.

Ila baadae nitakuja na kipindi cha elimu kwa jamii kuhusu hatua za kuchukua kimfumo kwa wote wenye changamoto kupitia mamlaka ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa kupitia dhana ya ugatuaji madaraka ambapo, huduma zote zimesogezwa Karibu na wananchi kupitia ofisi za wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri ambalo, kuna wataalamu wa wizara zote za kisekta wakihudumia wananchi.

Ahsante Sana. Ngoja tumtafute kwa msaada wa haraka, mengine yatafuata.

Shukrani.
 
Hbr za asubuhi. Kwa kuwa nimeona, nachukuwa wajibu wa kuwasiliana na mhusika Ili nijue iwapo kuna hatua za awali zilichukuliwa na kama bado zifanyike ikiwemo za ustawi wa jamii.

Ila baadae nitakuja na kipindi cha elimu kwa jamii kuhusu hatua za kuchukua kimfumo kwa wote wenye changamoto kupitia mamlaka ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa kupitia dhana ya ugatuaji madaraka ambapo, huduma zote zimesogezwa Karibu na wananchi kupitia ofisi za wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri ambalo, kuna wataalamu wa wizara zote za kisekta wakihudumia wananchi.

Ahsante Sana. Ngoja tumtafute kwa msaada wa haraka, mengine yatafuata.

Shukrani
Itakuwa vema kama utatupa mrejesho humu jambo liliponzia ili nasi tujue kilichoendelea.

Ahsante.
 
Mama D maisha ni jinsi vile kila mtu anavyoyachukulia. Inaumiza kujua kuwa kuna watu wanaishi maisha ya aina haya na serikali ipo inayopaswa kutoa huduma kwa watu wenye matatizo kama haya. inapaswa kuwekwa mfuko wa kijamii kama ilivyo katika nchi za wenzetu kwaajili ya kushugurikia wazee na wenye matatizo.
Mbona wenzetu wameweza na wananchi wanakatwa kodi?
Umeongea ukweli mtupu ila sio kwa serikali yetu hii ambayo kila mtu anawamba usawa wake hamuwazii mwingine anachowaza ni yeye tu
 
Hii Dunia ukiwa na shida shida nayo ukiwa na raha rahaa nayo.
Hakuna jipya ishi kulingana na wakati.
 
Nilienda kuiona Hiyo familia na matatizo ya huyo Binti yamenifanya niwe nae karibu kiasi fulani. Na ninatoaga kidogo kilichopo ndani ya uwezo wangu hata kama Mboga basi maisha yanaenda.
Ubarikiwe mno kipenzi ...Mungu akuzidishie maradufu ya ulichotoa
 
Umeongea ukweli mtupu ila sio kwa serikali yetu hii ambayo kila mtu anawamba usawa wake hamuwazii mwingine anachowaza ni yeye tu
Wenye shida ni wengi shida ni taarifa wanaojitokeza wengi wamepata msaada kwa serikali na jamii pia.
Wapo waliopata matibabu,mitaji,
Ukificha shida atajua Nani sasa
 
Bila kuweka majina yao, maeneo wanayoishi na namba za simu bado itatafsiriwa kama hadithi kwa baadhi ya wasomaji
 
Ingependeza ukaweka hata namba yako ili michango ipitie kwako maana kuna baadhi ya wachangiaji humu wanaweza kutumia namba kupeleka application kwa huyo binti
 
Sawasawa. Naomba kuuliza hivi TASAF tukiacha na kuimpower poor families economically je inawafikia watu wenye matatizo kama hawa? Au kuna haja ya kutanua majukumu yake na kuanzisha hili la kulea wazee kwakuanzisha facilities maalumu kila mkoa zitakazozokusanya vikongwe watakaothibitika familia zao hazina uwezo?
TASAF mradi wa watu wabongo uwape pesa eti wazifikishe sehemu bila kuzichota thubutuu!!
 
Back
Top Bottom