Binti (miaka 19) amepotea, naomba msaada kwa atakayemuona

mkuu hizi case za teenagers kupotea asilimia kubwa huwa wanarudi wenyewe ndani ya huo muda,na mara nyingi huwa ni mapenzi.
 
Binti yangu wa kazi aliondoka kama hivi na baada ya siku nne akarudi akasema nilikuwa kwa nabii x (hili kanisa lipo dsm) akadai kuanzia sasa atahudumu kanisani.

Akabeba vilivyo vyake akaondoka ila tukamwambia hakufanya sawa na nikamwambia baada ya siku tatu afuate hela yake.

Baada ya siku tatu alikuja akiongozana na vijana wawili ambao alisema anasali nao.

Nimefupisha sana ila tumekaa nae miaka miwili.
 
Hajatoroshwa na mwanaume, huyo ni mtu mzima kwaiyo ni katoroka na mwanaume. Hapo ni kuomba msaada kwenye kampuni za simu ili kujua watu aliokua anawasiliana nao mara kwa mara.
 
Amesema simu haipatikani, utatrakije simu ambayo haipo hewani?
Lengo la kutrack Huwa sio kujua tu kujua simu Iko eneo gan, simu ikiwa on kinachoongezekaga ni live location tu ila ikiwa imezimwa unaweza kujua alikuwa anazungunza na Nan? Mara ya mwsho kabla ya simu kuzimwa pamoja na kuona jumbe fupi za maneno aliyo tuma na kupokea
 
Mungu ajalie hitaji la moyo wako umpate akiwa yu mzima wa afya njema
 
Hawa watoto wetu watauwa wazazi kwa presha na sukari wakati mwenyewe kijibinua kwenye tendegu la kitanda. Mtu ametupa hela angalau awe na kaujuzi kwa kumfaa maishani yeye anakimbilia mtalimbo
 
mkuu ulikuwa unaishi nae vizuri kwaupendo kama mwanao wa kumzaa?? yani nikimuangalia huyoo binti namuona kama alikuwa anamanyanyaso anapata.

la msingi ni kuomba Mungu apatikane akiwa buheri wa afya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…