Binti (miaka 19) amepotea, naomba msaada kwa atakayemuona

Binti (miaka 19) amepotea, naomba msaada kwa atakayemuona

Nenda cybercrime waende kuangalia mawasiliano yake ya mwisho kwenye kampuni ya simu yamkin utapata kitu, andaa hela walau kilo 3
 

Attachments

  • 1693076679565.jpg
    1693076679565.jpg
    98.7 KB · Views: 5
MTU mzima hivyo anapoteaje?,mie nilipoamaliza form 4 nikiwa na 18 yrs nikiondoka home pasipo MTU yoyote kujua baada ya wiki ndio nikamjulisha mama.
 
Mbona kama anaonekana alikuwa anashida kichwani huyu alafu kapo wayuwayu😁😁
Habari ndugu zangu.

Ninaomba msaada, binti huyu ninaambatanisha picha zake amepotea tangu tarehe 27/08/2023.

Binti huyu anaitwa Antia Focas, nyumbani walizoea kumuita Nyakato. Ana umri wa miaka 19. Mkazi wa Mkundi Morogoro, japo ana miezi mitatu tu tangu ahamie mkundi, mwanzoni tulikuwa tukiishi Kihonda-Maghorofani. Mimi ni baba yake mdogo, nimekuwa nikiishi naye kwa muda wa miaka mitatu sasa tangu nimtoe kwa wazazi wake.

Niligundua kuwa amepotea tarehe 27/08/2023 muda wa saa 7:30 (saba na nusu) mchana, hii ni kwa sababu alikuwa akimpeleka mtoto shule alafu anapitia kujifunza cherehani, ikifika saa sita na nusu anakwenda shule kumfata mtoto, wanarudi nyumba muda wa saa 7:30. Siku hiyo ilifika muda huo hajarudi, ilipofika saa nane na nusu tukapiga simu shuleni na kugundua kuwa hata mtoto alikuwa hajachukuliwa pale shuleni, shule inaitwa WESLEY.

Tulipopiga simu kwa mtu aliyekuwa akimfundisha cherehani, alisema kuwa alifika tu asubuhi, akaaga kuwa anakwenda saloon, kuosha nywele na kusuka. Tulipofatilia saloon, tukaambiwa kuwa hakufika. Tulitoa taarifa katika kitua cha polisi cha Kihonda, tukaambiwa turudi baada ya masaa 48 kama hajapatikana, tuliporudi tukapewa RB namba na kuambiwa tuendelee kumtafuta.

Bahati mbaya hadi leo hatujampta, alikuwa na simu lakini tangu apotee haipatikani. Pengine ni rahisi kufikiri kuwa labda katoroshwa na mwanaume, lakini mazingira aliyoondoka yatia shaka, kwani hakubeba kitu chochote. Hakubeba hata nguo moja wala mkoba. Naomba msaada wenu kwa atakayemuona.

Simu 0766729127/0688746145.

Asanteni.

View attachment 2735961View attachment 2735963View attachment 2735964View attachment 2735973
 
Raia kama askari , askari kama raia ... Yaani wewe mtoto wako wa kike aliyevunja ungo akipotea na ukaenda kutoa taarifa polisi, kisha ukapewa jibu kuwa mwanao yupo kwa mwanaume utajisikia vipi?
Mtoto wa kike mwisho wake ni kupata mume unataka nisemeje hapo!?
 
Kwa muonekano wa Binti, ukitazama macho yake mkao katika picha, Jambo la kwanza naloona ni kuwa yupo, yupo kwa mwanaume ama kama si kwa mwanaume bas kaenda fanya kazi mahala pengine... YUPO, picha inajieleza, huenda hakuwa na amani sana kuish kwako Mkuu...
 
Back
Top Bottom