Binti (miaka 19) amepotea, naomba msaada kwa atakayemuona

Poleni,

Ila.sidhan kama kapotea nnachoona hapo 99% kadanganywa na mwanaume, hizi case zipo nyingi sana mtaani ,hawa mabinti ambao hawana shughuli maalumu ya kuwaingiza kipato cha kueleweka ,akili zao zinakua na wenge sana
Mfano mzuri ni ma house girl ,wanatoroshwa sana na kwenda kuishi kinyumba na wahuni

Naomba utatupa mrejesho hapa
 
Picha moja binti akila ice cream,, na pembeni yake kuna kikopo kingine kimoja cha ice cream,,
Lakini hakuna mtu.

Anza na kufatilia aliyekuwa nae kwenye ice cream ni nani?

Utakuja kunishukuru baadae
 
Binti yangu wa kazi aliondoka kama hivi na baada ya siku nne akarudi akasema nilikuwa kwa nabii x (hili kanisa lipo dsm) akadai kuanzia sasa atahudumu kanisani.

Akabeba vilivyo vyake akaondoka ila tukamwambia hakufanya sawa na nikamwambia baada ya siku tatu afuate hela yake.

Baada ya siku tatu alikuja akiongozana na vijana wawili ambao alisema anasali nao.

Nimefupisha sana ila tumekaa nae miaka miwili.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Unajua humu watu hawana experience yoyote kazi ni kuropoka tu kutrack tena unaweza watumia hao hao ukiwa nyumban Wana kutrakia mtu yoyote ambae unashda nae uwe na hela tu.
Una track vp simu ambayo ipo offline,means simu haitumiki na line haitumiki....hyo kitu nachojua hakiwezekan...
 
Habari ndugu zangu.

Ninaomba msaada, binti huyu ninaambatanisha picha zake amepotea tangu tarehe 27/08/2023.

Binti huyu anaitwa Antia Focas, nyumbani walizoea kumuita Nyakato. Ana umri wa miaka 19. Mkazi wa Mkundi Morogoro, japo ana miezi mitatu tu tangu ahamie mkundi, mwanzoni tulikuwa tukiishi Kihonda-Maghorofani. Mimi ni baba yake mdogo, nimekuwa nikiishi naye kwa muda wa miaka mitatu sasa tangu nimtoe kwa wazazi wake.

Niligundua kuwa amepotea tarehe 27/08/2023 muda wa saa 7:30 (saba na nusu) mchana, hii ni kwa sababu alikuwa akimpeleka mtoto shule alafu anapitia kujifunza cherehani, ikifika saa sita na nusu anakwenda shule kumfata mtoto, wanarudi nyumba muda wa saa 7:30. Siku hiyo ilifika muda huo hajarudi, ilipofika saa nane na nusu tukapiga simu shuleni na kugundua kuwa hata mtoto alikuwa hajachukuliwa pale shuleni, shule inaitwa WESLEY.

Tulipopiga simu kwa mtu aliyekuwa akimfundisha cherehani, alisema kuwa alifika tu asubuhi, akaaga kuwa anakwenda saloon, kuosha nywele na kusuka. Tulipofatilia saloon, tukaambiwa kuwa hakufika. Tulitoa taarifa katika kitua cha polisi cha Kihonda, tukaambiwa turudi baada ya masaa 48 kama hajapatikana, tuliporudi tukapewa RB namba na kuambiwa tuendelee kumtafuta.

Bahati mbaya hadi leo hatujampta, alikuwa na simu lakini tangu apotee haipatikani. Pengine ni rahisi kufikiri kuwa labda katoroshwa na mwanaume, lakini mazingira aliyoondoka yatia shaka, kwani hakubeba kitu chochote. Hakubeba hata nguo moja wala mkoba. Naomba msaada wenu kwa atakayemuona.

Simu 0766729127/0688746145.

Asanteni.

View attachment 2735961View attachment 2735963View attachment 2735964View attachment 2735973
Endelea kumtafuta ila usitumie vitisho kwake au kwa mtu alie nae
 
Nimempata. Alitoroshwa na huyu jamaa. Baada ya kumtorosha alimbadilishia namba ya simu, hadi sasa anatumia namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina la huyu jamaa. Kwa mujibu wao wameoana. Asanteni kwa michango yenu, mbinu nilizopata humu ndizo nilizozitumia kumpata. Asanteni sana.
 
Attachments

  • IMG-20230915-WA0068.jpg
    IMG-20230915-WA0068.jpg
    14.6 KB · Views: 3
Nimempata. Alitoroshwa na huyu jamaa. Baada ya kumtorosha alimbadilishia namba ya simu, hadi sasa anatumia namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina la huyu jamaa. Kwa mujibu wao wameoana. Asanteni kwa michango yenu, mbinu nilizopata humu ndizo nilizozitumia kumpata. Asanteni sana.
Sasa mkuu hebu ngoja kwanza...
 
Nimempata. Alitoroshwa na huyu jamaa. Baada ya kumtorosha alimbadilishia namba ya simu, hadi sasa anatumia namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina la huyu jamaa. Kwa mujibu wao wameoana. Asanteni kwa michango yenu, mbinu nilizopata humu ndizo nilizozitumia kumpata. Asanteni sana.
Wameoana[emoji1787][emoji1787]

Uyo jamaa sio dereva wa boda kweli mana ndio michezo yetu sisi..,mabeki tatu,mama ntilie,hao wa kushona yan mademu flan vitonga
 
Hapo mjiandae kupokea mdogo wako akiwa na mimba

Huyo muhuni atamchoka soon
Nimempata. Alitoroshwa na huyu jamaa. Baada ya kumtorosha alimbadilishia namba ya simu, hadi sasa anatumia namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina la huyu jamaa. Kwa mujibu wao wameoana. Asanteni kwa michango yenu, mbinu nilizopata humu ndizo nilizozitumia kumpata. Asanteni sana.
 
Pole sana mkuu, ILA hawa police ni piece of shit, why wasubirie 48hrs?,hii sheria ya wapi?nchi hii kweli ni pithole one,mtu akiwa potea, police wanatakiwa waanze muda huo huo kumtafuta, 48 hrs ameshavuka hizi porous borders zetu ndio maana jeshi la police nitalivunja na all above 40 yrs nitawapa marching order, leta vijana wapya wenye ari mpya
Taarifa ya mtu kupotea kiutaratibu inathibitika baada ya masaa 48, unatoa taarifa za awali kituo cha polisi halafu unaendelea kumtafuta sehemu mbalimbali, huwenda mtu alianguaka njiani kapoteza fahamu akakimbizwa hospitali, inatakaiwa muhusika/mtafutaji kwanza upite sehemu zote hizo, yaani mahospitali na kwengineko, baada kukosa majibu ndio unarudi tena kituo cha police na jalada la kupotea linafunguliwa baada ya masaa hayo 48. Ila kama unazo taarifa kamili za kutoroshwa au kuibiwa na kuna wahusika unawashuku hapo polisi wanafungua jalada muda huohuo.
 
Habari ndugu zangu.

Ninaomba msaada, binti huyu ninaambatanisha picha zake amepotea tangu tarehe 27/08/2023.

Binti huyu anaitwa Antia Focas, nyumbani walizoea kumuita Nyakato. Ana umri wa miaka 19. Mkazi wa Mkundi Morogoro, japo ana miezi mitatu tu tangu ahamie mkundi, mwanzoni tulikuwa tukiishi Kihonda-Maghorofani. Mimi ni baba yake mdogo, nimekuwa nikiishi naye kwa muda wa miaka mitatu sasa tangu nimtoe kwa wazazi wake.

Niligundua kuwa amepotea tarehe 27/08/2023 muda wa saa 7:30 (saba na nusu) mchana, hii ni kwa sababu alikuwa akimpeleka mtoto shule alafu anapitia kujifunza cherehani, ikifika saa sita na nusu anakwenda shule kumfata mtoto, wanarudi nyumba muda wa saa 7:30. Siku hiyo ilifika muda huo hajarudi, ilipofika saa nane na nusu tukapiga simu shuleni na kugundua kuwa hata mtoto alikuwa hajachukuliwa pale shuleni, shule inaitwa WESLEY.

Tulipopiga simu kwa mtu aliyekuwa akimfundisha cherehani, alisema kuwa alifika tu asubuhi, akaaga kuwa anakwenda saloon, kuosha nywele na kusuka. Tulipofatilia saloon, tukaambiwa kuwa hakufika. Tulitoa taarifa katika kitua cha polisi cha Kihonda, tukaambiwa turudi baada ya masaa 48 kama hajapatikana, tuliporudi tukapewa RB namba na kuambiwa tuendelee kumtafuta.

Bahati mbaya hadi leo hatujampta, alikuwa na simu lakini tangu apotee haipatikani. Pengine ni rahisi kufikiri kuwa labda katoroshwa na mwanaume, lakini mazingira aliyoondoka yatia shaka, kwani hakubeba kitu chochote. Hakubeba hata nguo moja wala mkoba. Naomba msaada wenu kwa atakayemuona.

Simu 0766729127/0688746145.

Asanteni.

View attachment 2735961View attachment 2735963View attachment 2735964View attachment 2735973
Wafuatulie mnara wa mwisho ambao simu yake ilikuwa ina ping, pia waonbe Subpoena ili mtandao wa simu watoe taarifa ya meseji na simu zote zilizoingia na kutoka siku za karibu na tukio
 
Nimempata. Alitoroshwa na huyu jamaa. Baada ya kumtorosha alimbadilishia namba ya simu, hadi sasa anatumia namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina la huyu jamaa. Kwa mujibu wao wameoana. Asanteni kwa michango yenu, mbinu nilizopata humu ndizo nilizozitumia kumpata. Asanteni sana.
Daahh mwamba kala chuchu mwezi mzima hatar sana, Hawa mabinti miaka 17-21 ni visanga sana.
 
Wameoana[emoji1787][emoji1787]

Uyo jamaa sio dereva wa boda kweli mana ndio michezo yetu sisi..,mabeki tatu,mama ntilie,hao wa kushona yan mademu flan vitonga
Boda boda huyo huoni hiyo picha hapo wamekaa kwenye boda boda
 
Nimempata. Alitoroshwa na huyu jamaa. Baada ya kumtorosha alimbadilishia namba ya simu, hadi sasa anatumia namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina la huyu jamaa. Kwa mujibu wao wameoana. Asanteni kwa michango yenu, mbinu nilizopata humu ndizo nilizozitumia kumpata. Asanteni sana.
Kumbe umempata, okay
 
Back
Top Bottom