Binti (miaka 19) amepotea, naomba msaada kwa atakayemuona

Binti (miaka 19) amepotea, naomba msaada kwa atakayemuona

Taarifa ya mtu kupotea kiutaratibu inathibitika baada ya masaa 48, unatoa taarifa za awali kituo cha polisi halafu unaendelea kumtafuta sehemu mbalimbali, huwenda mtu alianguaka njiani kapoteza fahamu akakimbizwa hospitali, inatakaiwa muhusika/mtafutaji kwanza upite sehemu zote hizo, yaani mahospitali na kwengineko, baada kukosa majibu ndio unarudi tena kituo cha police na jalada la kupotea linafunguliwa baada ya masaa hayo 48. Ila kama unazo taarifa kamili za kutoroshwa au kuibiwa na kuna wahusika unawashuku hapo polisi wanafungua jalada muda huohuo.
Jamaa anataka usipomuona mtu masaa 10 polisi waanze msako 😂😂
Kumbe upo zako lodge unapiga uno fulani la kikonde,
Case ni kuwa mpaka masaa 48 yapite kama kweli upo salama lazima utakuwa umewasiliana na wale watu wako wa muhimu, kupita hayo masaa ndo kunaleta maswali hivyo tukutafute
 
Taarifa ya mtu kupotea kiutaratibu inathibitika baada ya masaa 48, unatoa taarifa za awali kituo cha polisi halafu unaendelea kumtafuta sehemu mbalimbali, huwenda mtu alianguaka njiani kapoteza fahamu akakimbizwa hospitali, inatakaiwa muhusika/mtafutaji kwanza upite sehemu zote hizo, yaani mahospitali na kwengineko, baada kukosa majibu ndio unarudi tena kituo cha police na jalada la kupotea linafunguliwa baada ya masaa hayo 48. Ila kama unazo taarifa kamili za kutoroshwa au kuibiwa na kuna wahusika unawashuku hapo polisi wanafungua jalada muda huohuo.
Kama hii ni sheria nitaifutilia mbali Sawa na ile ya kupata PF3 kwanza kabla ya kutibiwa, mtu akipotea tu TOA report police, na police wanatakiwa kuanza kumtafuta straight, kijukuu cha president JK kikipotea unataka kuniambia police watasubiri 48hrs kuanza kumtafuta?au hizi ni sheria zinazowa wahusu poor of the poorest wa lingusenguse?,wake up mkuu, achana na upumbavu huu
 
Habari ndugu zangu.

Ninaomba msaada, binti huyu ninaambatanisha picha zake amepotea tangu tarehe 27/08/2023.

Binti huyu anaitwa Antia Focas, nyumbani walizoea kumuita Nyakato. Ana umri wa miaka 19. Mkazi wa Mkundi Morogoro, japo ana miezi mitatu tu tangu ahamie mkundi, mwanzoni tulikuwa tukiishi Kihonda-Maghorofani. Mimi ni baba yake mdogo, nimekuwa nikiishi naye kwa muda wa miaka mitatu sasa tangu nimtoe kwa wazazi wake.

Niligundua kuwa amepotea tarehe 27/08/2023 muda wa saa 7:30 (saba na nusu) mchana, hii ni kwa sababu alikuwa akimpeleka mtoto shule alafu anapitia kujifunza cherehani, ikifika saa sita na nusu anakwenda shule kumfata mtoto, wanarudi nyumba muda wa saa 7:30. Siku hiyo ilifika muda huo hajarudi, ilipofika saa nane na nusu tukapiga simu shuleni na kugundua kuwa hata mtoto alikuwa hajachukuliwa pale shuleni, shule inaitwa WESLEY.

Tulipopiga simu kwa mtu aliyekuwa akimfundisha cherehani, alisema kuwa alifika tu asubuhi, akaaga kuwa anakwenda saloon, kuosha nywele na kusuka. Tulipofatilia saloon, tukaambiwa kuwa hakufika. Tulitoa taarifa katika kitua cha polisi cha Kihonda, tukaambiwa turudi baada ya masaa 48 kama hajapatikana, tuliporudi tukapewa RB namba na kuambiwa tuendelee kumtafuta.

Bahati mbaya hadi leo hatujampta, alikuwa na simu lakini tangu apotee haipatikani. Pengine ni rahisi kufikiri kuwa labda katoroshwa na mwanaume, lakini mazingira aliyoondoka yatia shaka, kwani hakubeba kitu chochote. Hakubeba hata nguo moja wala mkoba. Naomba msaada wenu kwa atakayemuona.

Simu 0766729127/0688746145.

Asanteni.

View attachment 2735961View attachment 2735963View attachment 2735964View attachment 2735973
Watoto umri huu ni hatari s ana na ndo wanasumbua mtaani kwa sasa. Huyu yupo chimbo watunzwa na wajuba anawatoa majasho tu
 
Nimempata. Alitoroshwa na huyu jamaa. Baada ya kumtorosha alimbadilishia namba ya simu, hadi sasa anatumia namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina la huyu jamaa. Kwa mujibu wao wameoana. Asanteni kwa michango yenu, mbinu nilizopata humu ndizo nilizozitumia kumpata. Asanteni sana.
Daah pole sanaa kawatesaa kumbe Mitiii imemfanya atorokee.. Ndo maana polisi kesi kama hizi huwa hawachukulii serious yani unaweza ripoti wakijua ni Binti age hizo bhasi wanakuwa kama hawajakusikia vilee wanaendelea na mambo yao labda urudi mara 3 au 4 hivi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Bora awe wa kiumee kidogo watashtuka. Vibiti hadi vya la darasa la saba vinatoroka kufata bakora siku hizii hatari sana. Juzi arusha kuna mama alikuwa anamuomba mwanae arudi nyumbanii.. mwingine moshi sijui hukoo[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Pole sana mkuu, ILA hawa police ni piece of shit, why wasubirie 48hrs?,hii sheria ya wapi?nchi hii kweli ni pithole one,mtu akiwa potea, police wanatakiwa waanze muda huo huo kumtafuta, 48 hrs ameshavuka hizi porous borders zetu ndio maana jeshi la police nitalivunja na all above 40 yrs nitawapa marching order, leta vijana wapya wenye ari mpya


Hata Marekani hungoja reasonable mda kabla ya kuanza kutafutwa, ni kawaida, mnapenda sana kubeza mambo ya nchi, siyo yote ni Mabaya.
 
Binti mdogo anajiita kaolewa!!, ,,mwache akafujike akishtuka tayari na watoto wawili ,singo maza mtarajiwa.


Hapo tayari kanaonekana kameshafubaa.
 
Back
Top Bottom