Ila vijana wa sasa ni wa hovyo sanaa, wavulana wanapenda vya Bure kwakua wasichana wameamua kujirahisisha.
Feminism imetafsiriwa tofauti na ilivyo. Ni muhimu kwa mwanamke kujitambua na kujua thamani yake sio kwaajili ya kupata sponsorship Kwa wanaume Bali kutunza utu na heshima yake katika jamii.
Kuna tukio lilinitokea kitambo kdgo, kijamaa kimejileta twende out kufika akaagiza chipsi na mishikaki na maji, binafsi nikienda out lazima niwe na pesa zangu mfukoni ili hata akizingua najilipia nasepa, etii baada ya kulipa bill namskia twendee basi guest, nimebanwa mwenzio, Whaaaaat!!? Hivi umenionaje yaani!?. Kwamba maji mara Moja!?, nikamwambia siendi na hapa narudi nyumbani, akajua utani , akajifanya kutangulia huko guest akajua ntamfata nyuma, mie huyo nikaondoka zangu nyumbani mdogo mdgo , akakata na mawasiliano ..... Mxieeeeee!!!!!. Yote yanatokea kwakua mabint wameamua kujirahisisha, ukitongozwa basi shida zako zoteeee unazitoa , sijala, sijasuka mara Kodi, mtu ataachaje kuona unajiuza kwa style hiyo!?.