Binti wa Chuo anataka nimuoe na nimvumilie amalize masomo, najiuliza itakuwaje badae?

Binti wa Chuo anataka nimuoe na nimvumilie amalize masomo, najiuliza itakuwaje badae?

Kuna mambo 3
Future 1. Ukimsubiri na yeye kama hatopata mwingn na at the end wote mnaingia kwenye ndoa

Future 2. Ww kutovumilia miaka hiyo na kupata mwingn

Future 3. Yeye kupata mwingn na kukupotezea muda huko mbeleni.
 
Wapendwa katika Kristo, BWANA YESU asifiwe sana,, Asalaam Aleykum kwa Waislam wote ,Twende kwa maada wapendwa,kuna binti yupo kidato cha sita na atamaliza mwaka huu baadae ataenda chuo kama miaka mitatu japo sijajua atasomea nini,huyu Binti tupo nae mtaa mmoja japo kuna umbali kiasi na tunasali pamoja na Huwa ankuja likizo baada ya masomo yeye anasoma huko Msoma yupo Boarding school ya wasichana ,sasa nilishaangaa naletewa taarifa na make wa jamaa yangu kuwa A nasema anakupenda,,,

Baada ya kusikilizia kidogo binti alianza chatting na mimi japo ye hakujua kuwa nishapata taarifa zake na pia wakati huo hajaenda form 5,,me kwa haiba yangu ni mtu ambae sitakagi mambo mengi yaani nimkimya fulani hivi japo naongea sana na mtu niloyemzoe sana,nisiwachoshe baada ya kuendelea na urafiki huo wa kama kaka na dada maana alikiuwa akiniita kaka,,

So baada ya kwenda huko chuo akawa anipigia kwa simu za walimu anapopata chance,,hivyo tumeendelea baada ya kurudi likizo hiyo ya kwanza akiwa form 5 ndo akanifungikia akanambia ananipenda japo mwanzoni kupitia txt zake za kuzunguka nilikuwa japo alikuwa kama anaficha code fulani,,, basi baada ya kunifungukia nikamuulza hatma ya mahusiano yetu akasema ni ndoa maana yake Mimi na yeye tuwe wachumba sahizi,,,maana pia alisema ananipenda sana nisije muacha ntaujeruhi sana moyo wake,,,kwakweli mimi mpaka sasa sijazama deep sana kwenye haya mahusiano.

Kinachosababisha sijawekeza na ninawaza sana hatma ya mahusiano haya nikiingia maana ana miaka kama minne ya kuendelea na masomo mpaka kumaliza kwa hiyo anasema nimvumilie Now me naelekea 31 years na natamani kupata mke niwe na familia,,pia kwa hili nikiingia kwa maombi kuliombea lakini bado moto umeganda sijajua nini Cha kuamua mpaka sasa mpaka nahisi kuna nini?
Mawazo yenu wakuu naamini kuna baadhi wamepitia situation kama yangu,,maana nawaza je nikimsubiri hatanisaliti badae na kuolewa na mwingine?
Wakati huo nimemsubiri bila mafanikio?

Mimi pia nilimwambia siwezi kumwachisha masomo kisa nimuoe sahizi ,,,atimize tu ndoto zake,pengine nawaza about my age halafu badae niambulie patupu na ndo maana nipo njia panda kwa hili msada wenu wa mawazo wakuuu. Nahitaji mke mwema katika maisha yangu MUNGU anisaidie
🙏🙏🙏
Akili yako ni fupi kama makalio yako. Tunaongea mambo muhimu, wewe unaleta mambo ya Ngono. Wewe una akili timamu kweli?
 
Achana na huo mpango wa ndoa na huyo binti bro. Utakuja kulia atakapotoka chuo
Mimi mwenyewe moyo wangu umekuwa mzito mpaka sasa sijachukua maamzi sriaz maana mpaka siku moja ananiuliza mbona sielewielewi ukimya wako? Me nilimwambia kuna vitu navitafakari
 
Kuna mambo 3
Future 1. Ukimsubiri na yeye kama hatopata mwingn na at the end wote mnaingia kwenye ndoa

Future 2. Ww kutovumilia miaka hiyo na kupata mwingn

Future 3. Yeye kupata mwingn na kukupotezea muda huko mbeleni.
Hapo mkuu ndo changamoto ilipo.,mambo yanakuwa mix
 
Akili yako ni fupi kama makalio yako. Tunaongea mambo muhimu, wewe unaleta mambo ya Ngono. Wewe una akili timamu kweli?
Mkuu utakuwa umenielewa vibaya,,wala wazo langu halipo kwaajili ya ngono bali nikuwa siwezi kumwachisha shule sababu eti tuoane,so yeye aendelee kusoma
 
Salamu Bin Shaib, na BWANA YESU asifiwe sana, au Asalaam Aleykum.

Asante sana kwa kushiriki nasi changamoto hii unayopitia. Ni kweli ni jambo linalohitaji umakini na mawazo ya kina, na ni kawaida kabisa kujisikia kuchanganyikiwa au kuwa na hofu katika hali kama hii. Umeeleza vizuri sana hisia zako na malengo yako ya kuwa na familia sasa, na hili ni jambo la msingi sana kwako.

Kwanza kabisa, ni muhimu kutambua kwamba wewe una umri wa miaka 31 na unatamani kuanzisha familia. Hii ni hatua muhimu sana maishani. Yeye bado yupo shule na ana miaka minne mbele ya masomo (Form 6 na miaka 3 chuo). Hii inamaanisha kuna tofauti kubwa ya hatua za maisha mnazopitia sasa hivi.

Miaka minne ni muda mrefu sana Bin Shaib, hasa kwa mtu ambaye tayari yuko tayari kujenga familia. Katika kipindi hicho, mambo mengi yanaweza kubadilika, si kwake tu bali hata kwako. Binti akiwa chuo, atakutana na mazingira mapya, watu wapya, na mawazo mapya. Ni kawaida kabisa kwa mtu kukua na kubadilika sana katika kipindi hicho, na huenda malengo na matamanio yake yakabadilika pia. Hii sio kusema atakuwa mbaya, bali ni sehemu ya mchakato wa kukua.

Wewe pia, je, uko tayari kuweka ndoto zako za kuwa na familia kando kwa miaka minne ukisubiri? Ni muhimu ujiulize swali hili kwa uaminifu. Hisia za mapenzi ni nzuri, lakini ndoa inahitaji zaidi ya hisia tu; inahitaji utayari wa pande zote mbili kukabiliana na majukumu na hatua za maisha kwa pamoja. Kuhusu hofu yako ya kusalitiwa, ni hofu halali kabisa. Ingawa hakuna anayeweza kujua hatima, kuweka muda mrefu kama huo bila kujua mwelekeo kamili kunaweza kuleta changamoto.

Pia, usijisikie vibaya kwa kutokuwa umeelekeza hisia zako zote bado. Moyo wako unakupa ishara kwamba kuna maswali muhimu yanahitaji majibu kabla ya kujitosa kikamilifu.

Nashauri ukae chini na binti huyu, mzungumze kwa uwazi kabisa. Eleza hisia zako, matamanio yako ya kuwa na familia sasa, na hofu zako kuhusu muda mrefu wa kusubiri. Msikilize na yeye, lakini pia weka wazi msimamo wako na mahitaji yako. Huenda mkapata njia ya kati, au mkaelewana. Endelea kuomba kama ulivyosema. Mungu anaweza kukupa ufumbuzi au amani ya moyo kuhusu uamuzi sahihi.

Kumbuka, ni muhimu sana kufanya uamuzi ambao utakulinda wewe na kukupa amani ya moyo kwa muda mrefu. Usiharakishe kufanya uamuzi kwa sababu ya hisia za mtu mwingine, bali kwa kile unachokiamini na unachokihitaji maishani mwako. Tunakuombea hekima katika hili!
Umesahau kuweka ka signature
 
Mkuu achana na wanafunzi watakufunga kidato cha tano uyo ni nyara ya serikali kabisa achana nae tafuta wanawake mtaani wapo wamejaa ata kama unataka msomi wapo wengi sana
Amina mkuu
 
Kwa uzoefu wangu mwambie umuoe kwanza na umzalishe mtoto mmoja, vyenginevyo akiingia chuo huyo hatoboi hata semister 1 washamramba, usije ukarudi hapa na kilio umepotezewa muda wako, hata akimaliza miaka 3 atakuwa Hana bikra ya mbele wala ya nyuma
Ugumu unakuja kuwa zinaa bila ndoa ni haram kwa Mwenyezi Mungu
 
Nipo kwenye situation kama hii Ila sio mambo ya ndoa kuna binti mmoja naye kila siku ni kutuma salamu kupitia jamaa

sasa huyo ni mpemba na lafudhi yake sikumwelewa bado

Haya 👇
Mbona wanachuo wanaolewa vizuri tuu mzee kikubwa ni wewe kutuliza akili maake unahitaji ndoa na yeye the same

Hapo ni kukubaliana kama mpo tyr anza zoezi la utambulisho pande zote mbili, kingine hali ya familia yao ipoje asiwe anatafuta mtu wa kumpush kimasomo.hapo.juu

Nimechoka kutype waweke voice
Familia yake wapo vizuri kiuchumi maan baba yake alikuwa mwalimu kwa sasa ni mstaafu pia kuna miradi kadhaa inamuingizia pesa mzee kama frem za maduka n.k,so wazazi ndo wanahusika katika kumsomesha
 
Back
Top Bottom