Binti wa Jacob Zuma achumbiwa na Mfalme Mswati III

Binti wa Jacob Zuma achumbiwa na Mfalme Mswati III

Nafarijika sana mnavonipambania kijana wenu nipate mwali, huyu bidada hapo ni mambo ya diplomasia yanasetiwa ila huyu ni fungu langu kabisa
Ngoja tuongee na wanadiplomasia nguli wetu wakupambanie umpate huyu mwali.

Tutatumia na ujasusi wa diplomasia,uchumi na kimahaba ili ushinde, sherehe hata mtu akichangia million 1 kama hana passport asisogee
 
Binti ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma alikuwa miongoni mwa mamia ya wanawake na wasichana waliocheza ngoma kwa ajili ya Mfalme wa Eswatini katika sherehe za kitamaduni siku ya Jumatatu, kuthibitisha uchumba wake na mfalme huyo.

Nomcebo Zuma, 21, alikuwa miongoni mwa watu 5,000 kutoka katika ufalme huo mdogo katika sherehe maarufu kama ‘Reed dance’ ya kila mwaka katika Kijiji cha Kifalme cha Ludzidzini huko Lobamba, kilomita 23 (maili 14) kusini mashariki mwa mji mkuu Mbabane.

Ijapokuwa sherehe hiyo ya siku nzima ni ya kitamaduni kwa mwanamke, imefanyika wakati ambapo Mfalme Mswati, 56, anaweka wazi chaguo lake la mke mpya.

Tayari ana takriban wake14, baadhi yao aliwaoa walipokuwa wadogo, na ana takriban watoto 25.

Wiki iliyopita, kaka yake Mswati alisema kuwa Nomcebo Zuma atahudhuria Ngoma ya Reed kama “liphovela”, ambayo ina maana ya mchumba wa kifalme.

Katika hafla ya jioni ya Jumatatu, alikuwa miongoni mwa mamia ya wasichana waliovalia mavazi ya kitamaduni ya rangi ya rangi, wengine wakiwa na mapanga na ngao za kuigwa, ambao walicheza mbele ya Mswati na msafara wa wanaume waliovalia ngozi za kitamaduni.

Baba yake Jacob Zuma, 82, pia ana wake wengi kutokana na mila zao na watoto takriban 20. Alilazimika kujiuzulu kama rais wa Afrika Kusini 2018 chini ya wingu la tuhuma za ufisadi.
Chanzo.Trt Swahili
 
Nomcebo Zuma, 21, atakuwa mke wa 16 wa Mfalme Mswati Il. Binti huyo alikuwa miongoni mwa mamia ya wasichana waliocheza ngoma kwa ajili ya Mfalme wa Eswatini katika sherehe za kitamaduni siku Jumatatu, kuthibitisha uchumba wake na mfalme huyo. Mfalme Mswati Ill ana umri wa miaka 56​

===============For English Audience============
Eswatini’s King Mswati III's plans to wed Nomcebo Zuma, the daughter of former South African President Jacob Zuma, as his 16th wife. Political analysts dismiss the union's geopolitical impact but see its potential in strengthening ties between the two leaders.

A royal delegation from Eswatini, also known as Swaziland, visited Jacob Zuma’s homestead at Nkandla in July in accordance with tradition, marking the start of Mswati’s marriage proposal to Zuma.​

SOURCE: VOICE OF AMERICA
Madingi Kwa madingi.....mafataki
 
Back
Top Bottom