Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Hata mimi nilikua kama wewe.
Nilikua napenda kulalamika na kuwalaumu watu wengine.
Nilikua nasubiri nifanyiwe ili nije nipate mtaji.
Lakini akili ilipofunguka na kujua hii dunia inataka mtu mwenye akili nyingi, ndipo maisha yangu yalipo badirika.
Nikajua kuwa biashara sio mtaji ila ni wazo.
Wazo la biashara unalipata kulingana na hali yako.

Hakika nakuambia hata leo hii ukipewa mil 100, huwezi ifanyia kitu kama akili yako inadhani biashara ni mtaji
 
Mkuuu mi sidhani hata akisema itakusaidia kitu kama umepanga kitu chako haijalishi unamtaji kiasi gani kama uko comited basi hata kwa mtaji wa laki1 utaweza kufanya tu ila ukisema uangalie nani kafanya kwa mtaji gani ndugu utachelewa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani unaongea vitu vya kwenye vitabu na madaftari,huzungumzii maisha halisi ya hapa Tanzania.
 
Hayo mandhari umeyaangalia lakini yana ghalimu mtaji bei gani au unaongea tu kwa sababu unakula kwa mama wewe dada?
makande yanahitaji mtaji kiasi gani?wabongo kwa visingizio

Sent from my TECNO WX3 using Tapatalk
 
Hongera kwa kujishughulisha lakini kama nchi inabidi kubadili mtazamo naona nchi hii tumeweka malengo chini sana kwa vijana....mtu akifanya kitu kidogo anasifiwa kana kwamba amefanya jambo kubwa wakati jamii ilipaswa iweke matarajio makubwa zaidi kwa vijana....ukiwa na ujuzi wa kupika hata kama darasa la saba ukafanya mama ntilie hupaswi kusifiwa hivyo kwasabu ni kile kinatarajiwa angalau ungeweza kufanya....

Lakini tofauti na majirani nchi hii kijana wa kawaida anatarajiwa kutofanya chochote...akifungua hata banda la juisi basi huyo amefanikiwa....kama taifa yatupasa kutamani makubwa na kuwaza makubwa
 
Hongera sana kwake!!! Na tunakoelekea..... Watajitokeza wengi tu.... Maisha yamekaza hayataki kuremba sasa hivi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna ufara basi huu wako ni wa kiwango cha SGR. so tafsiri yako ya kuishi nje ni mafanikio. Braza kama hujawahi enda huko tulia. Hao wanaoishi nje ni Mungu wao na wao ndo wanajua.
Our mental liberation s pre-requisite to the future prospect

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuongezea : tatizo nanba moja la watanzania ni kupoteza muda mwingi kusomea vitu visivyo kua na msaada kwenye maisha yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo vijana wakishasoma ulaya wamebadilika kabisaa!!! nimewaona wengi wanafanya vibiashara vya ajabu ajabu ona sasa hata mwandiko wake umebadilika anaandika handwriting ya kizungu
 
Ufara utakuwa unao wewe,kama umeenda kusoma ulaya halafu ukarudi mikono mitupu,wapo wengine wa aina yako,unaenda ulaya iwe kusoma au vyovyote halafu unaanza kufuata maisha ya wenyeji,ile starehe wanazofanya,na wewe unataka utimize tu kile ulichofuata bila kuangalia fursa zingine nyingi zilizopo kule. Wanaoshindwa kule ni ksbb tu kujifanya nao mabishoo,nao hawataki kazi za chini kama wenyeji japo zina kipato kizuri kuliko huku. Mimi nisingekuwa na maisha yangu ningeenda kule,nakuhakikishia 100% narudi na hela mbayaaa mkuu,sibahatishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Then what next ukirudi na hela! Nakuona limbukeni fikra zako ni kuwa kwenda nje ni kuwa na maisha bora. Braza kuna watu wana make mpunga hapa hapa kwa magufuli na sio hizo za kwenda kuosha mbwa wa wazungu. Tuliza kichwa mtaalamu. Kuna mana gani kupata hela kwa kufanya kazi hata ambayo mwenyewe unaona inakushushia utu wako. Wengi wanasema wako nje ila nakuapia ni mahouseboy tu huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina bro tumetoka kijiji kimoja ni afisa wa ubarozi nchi fulani za Scandinavia,yuko huko kikazi kuanzia kipindi cha mkapa. Wakati anaenda kule alikuwa na vijana wawili,halafu kule akaenda kuzaa mtoto mmoja,hao watoto sasa wana uraia wa huko,ni wakubwa sasa. Mafundisho yake kwa watoto ilikuwa ni namna ya kutumia fursa za kuwa kwao kule. Mpaka sasa hao watoto wana akaunti ya pamoja,lakini ina hela ya kutosha. Ksbb wote wakitoka masomoni wanapumzika then wanaingia kazini masaa mengine yasiyo ya masomo na siku zisizo za masomo. Ila kwa nyie mnaoenda mnaiga maisha ya kule badala ya kufikiria na kutumia fursa vizuri hiyo. Mnadharau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mnhhhhh hii ni prove tosha,wazazi wa change mind set zao,nina uhakika huyo binti angesema anaenda kusomea upishi wazazi wangekataa kumsomesha….

Anyway tusidanganyane,huyo binti amecheza na fursa ...ameangalia nini cha kufanya kwa wakati huu..hii haimpunguzii lolote,in the future anaweza kupata kazi inayoendana na kipato chake,cha muhimu ana degree yake under the belt....

Katika nchi yetu,swala la passion halipo,watu wanasoma kutoka na nafasi chache zilizopo katika soko la ajira,mambo ya passion/interests/talents halipo katika nchi yetu…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…