Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Mimi nilidhani anapika makamde stendi kumbe makande ya kisasa wanauza supermarket
 
Sawa. Sio kila mtu anaweza kwenda kuwa mfagia choo huko. Mwache dada aanze mdogo mdogo kesho akimiliki 5 star hotel mtaanza aaa kahongwa. Usilo lijua kuhusu kazi hizo wanafanya huko nje basi ungebadili msimamo wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpishi wa kishua.... Makande ya kishua yanaliwa na washua any way thanks kwa idea Dem wangu alikuwa anahangaika biashara ya kufanya
 
Sawa. Sio kila mtu anaweza kwenda kuwa mfagia choo huko. Mwache dada aanze mdogo mdogo kesho akimiliki 5 star hotel mtaanza aaa kahongwa. Usilo lijua kuhusu kazi hizo wanafanya huko nje basi ungebadili msimamo wako

Sent using Jamii Forums mobile app
May be jamaa yangu. Lakini huyo mpaka hapo sina uhakika kama haja-feal maisha mpaka hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo kuuza makande wala sio hoja,hata Mimi ningekuwa mtoto wa Bakhressa,ningeweza kufungua hata genge!!we unafikiri anaendesha maisha yake kwa kutegemea Mapato ya hayo Makande?Kuna finance base na connections kubwa ya familia yake inayomsapoti,mfano akipika hayo Makande,harafu akapewa tenda ayapereke Sheraton hotel,au white sand,unafikiri utalingana naye?
Na hayo makande hapikii huku kwetu uswazi,ubungo,tabata,manzese,akiyapikia mikocheni,harafu yanafatwa na gari kupelekwa Sheraton,!!kila MTU anaweza kufanya hivyo akipewa mchongo.
Kijana gani wa Bongo,umwambie kuna tenda,ya kusafisha swimming pools,masaki,na mikocheni,kila wiki,na kila swimming pool,unalipwa 300K,nani atakataa?
Watoto wa kishua,kwa kutumia connections za wazazi wao,wanaweza kutoka hata wakiuza maji,
Sio kitu cha ajabu,
Nina jamaa yangu,anatenda ya kusupply nyanya,mboga za majani,nk kwenye mahotel makubwa huko Dar,hana gari,anatumiwa mahitaji kila siku jioni,asubuh,anaenda Kariakoo,anachukua mzigo,anatia kwenye teksi,anapereka,
Saaa sita mchana,ameishalipwa chake,anaweka miguu juu,nani hawezi kufanya hivi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuelewe kwanza:-
  1. kuna watu wanatamani kuwa wajasiriamali,lakini tatizo ni mtaji.
  2. kuna wengine mtaji upo ila hawana asili ya kufanya biashara/ujasiriamali
  3. kuna wengine wanafanya biashara/ujasiriamali kwa sababu ya kukosa ajira
  4. wengine hawapendi kuajiriwa lakini wanatafuta mtaji wajiajiri.
Kwa hiyo,kuwa na wazo ni hatua ya mwanzo,na kulitekeleza wazo ni garama(fedha) nikiwa na maana;kununua vitendea kazi,ofisi,kutafuta masoko,vifungashio,kupata vibali n.k
 
Connection ni muhimu ili kupata soko la uhakika, vinginevyo utawekeza pesa soko hakuna.
 
Kuna point ya msingi sana kaongea ambayo Wengi wenu hamuitilii maanani. Kasema hivi fanyeni kitu mnachokipenda. Ofcoz yeye anapenda kuuza makande it doesn’t matter imemchukua miaka mingapi kutambua kwamba anapenda kuuza makande. Mbona kuna watu ni na professor kitambo but wamekuja jitambua juzi kuwa kumbe ni wanasiasa. We jiulize mpaka sa hivi hapo ulipo are happy with your job? Au ndo hivo tonge kinywani. If you do what you makes you happy money will come naturally. Na Ndo maana unaona kuna mtu ni mpiga picha na Ana passion nayo anatoboa ila we unaepiga picha sababu huna option hutakaa utoboe. Hii story itumie kujiaccess wewe zaidi kuliko huyo dada, after all nani kasema kapoteza muda? Kwani anawahi wapi?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Branding inakula hela kuliko bei ya gunia na maharage
 
Ni nyingi kama una mtaji wa maana. Bila hivyo utapoteza mda mrefu huku ukikua slow sana kimaisha. Atleast kwa mtaji wa 15-20m unaweza fanya kitu cha kueleweka kwenye mojawapo ya majiji ya Tanzania ukapiga hela. Ila mikoani hela hamna!
 
nimecheka kwa saut
Eti "kande la kisasa"
kwan kande la kisasa likoje mkuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Freelancer unakosea!

Hapa wadau hatutaelewa popoma ni nani kati ya wanaomsifia au wanaomkosoa,wewe unaona yupo sahihi kwa elimu yake hiyo kufanya biashala ya chakula?

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Tutumie muda mwingi kutafakari kuhusu maisha yetu na si kuanza kudhihaki kuhusu maisha ya wengine
 
Upumbavu mtupu... una masters halafu unauza makande? Ulisomea kuuza makande? Ulienda shule kufanya nini sasa!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe tuambie kiwango chako cha elimu na shughuli unayofanya kwa sasa .Inategemea unauzaje hayo makande? Namna unavyouza hayo makande ndiyo itaonyesha kama elimu inakusadia au haikusaidii. Mnakurupuka tu kuandika ujinga lakini hamna mnachojua
 
Nishamjua huyu dada , binti wa lema muuzaji wa spare za magari pale stendi ya igoma miti mirefu.
 
Tatizo mtaji pia, sio kwamba watu hawapendi kujiajiri

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukisubiri kupata mtaji utakaa hadi unazeeka bila kupata mtaji. Wafanyabiashara wengi wakubwa wameanza na mitaji midogo tu. Tatizo watanzania siyo wabunifu kabisa. Tanzania ni kati ya nchi chache sana Afrika zenye fursa nyingi unaweza kuzaliwa maskini wa kutupwa lakini ukaja kuwa tajiri mkubwa baadaye. Wasiasa wetu wanawadanganya sana vijana eti hali ngumu, hakuna ajira. Ukiamua kuwatumia wamachinga pekee waliotapakaa Dar es Salaam yote ni fursa tosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…