Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Binti wa kishua, mwenye shahada toka Marekani amejiajiri kuuza makande, dada zetu maskini wanachagua kazi

Mimi nna degree ya SAUT nachoma mahindi hapa darajani hapa Mbeya.Huyo hafanyi biashara anajitangaza,tupo wengi huku tunatokea kwenye familia maskini mnoooo nadhani ndiyo maana hamtutangazi.....HAKUNA MTU HAPENDI KUFANYA KAZI,HAKUNA MTU ANAPENDA KULA BURE,SHIDA NI MTAJI NA KUPATA KAZI YENYEWE.
Kahiyo hoja yako ni nini unataka Ayo Tv aje
 
Kwenye maisha haya, MTU UKIWEZA KUIUA KITU INAITWA EGO... utafanikiwa zana
Hii inaturudisha nyuma sana mkuu, unaweza tengeneza hata 50K ya kwenye kabiashara kasikofika hata laki 5 ila tatizo EGO!

Yani na degree niwe fundi kushona? Yani na degree niwe shoe shine? Yani na degree niuze matunda?

Hahah tutabaki kulalamika jf tu mpaka uzee utukumbe!
 
Ni vizuri kukosoana ila kwanini nisichague kazi? Swali langu la msingi ni kwanini watu tunawabana hadi kwenye kuchagua kazi.

-Acha watu wawe wanavyotaka wawe nawe kuwa unayetaka kuwa.

Hii dunia ipo fair saana.
Umeongea point sana, kila mtu awe vile anavyotaka kama wewe graduate unafanya shughuli fulani sio lzm wote tufanye hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
makande yanahitaji mtaji kiasi gani?wabongo kwa visingizio

unafikiri angepikia mtaani kwenye vumbi huko hayo makande yangelika???

Umetizama kitchen yake lakni au umeamua kuongea tu suala la mtaji? Jaribu kuona ofisi yake jinsi ilivyo amepanga ghorofani huko na kodi za mwanza nadhani unajua bei yake?

Huyo kawezeshwa vya kutosha na familia yake na hapiki tu makande
 
Kuna Vijana wengi sana Wenye good business plans ideas ila wana kwama njiani kwa sababu hawana Mitaji "...

Wapo wengine ambao walikuwa hawana mitaji na wakafanikiwa ' lakini iliwachukua muda mrefu sana kuweza kufika mahali walipo " kwa sababu waliamua kwanza kufanya kazi ili waweze kupata Mitaji ....

Nampongeza sana huyo dada " Lakini tusiwabeze watu pia " kwa sababu hatujui wanapitishwa katika magumu ya kiasi gani na maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ndo huww mnatumia kama Ngao?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbona unashindwa kujiongeza, umeshaambiwa ni mtoto wa kishua hata wazazi wake walishangaa why aingie kwenye kupika vyakula wakati mtoto katoka USA kusoma...

Mwisho wa siku ilibidi wampe support tu ndio kitu alichopenda, thats why wazazi walimwezesha...

Kubali kataa ni watu wachache sana wanaanzia zero, wengi wao kama huyu binti wanaaishiwa kuwezeshwa ndio maana wanatoka kimaisha.
 
Habari wadau...

Nimekutana na habari ya Nancy Lema wa Mwanza nikaona ku-share nanyi wadau mtoe maoni.. je binti yupo sahihi au wrong?

Kafanya Shahada yake St Marys University of Minnesota na masters university of Minnesota huko USA.

Baada ya kumaliza masomo yake akaamua kurudi nyumbani kujiajiri kwa kuuza makande kisasa na kwao ni mambo safi hasa hasa...

Nawaza tu why dada zetu maskini hawapendi kujishughulisha huku washua hawachagui kazi.

Nimemkumbuka na Mercy Kitomari Nelwa Gelato naye ana degree ya U.K ila amerudi Tanzania anauza ice cream tu kisasa

Kwahiyo wadada wote wasomi wa kishua wauze makande?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitaki kuongea mengi lakini niko na shaka kubwa kwa hii masters degree ambayo huyu binti anaye, kwanza amesema hi ya finance, hii ndio ukweli , marekani ukiwa na masters in finance kazi ni tele, na pia kupata kibali cha kuishi huko amerika sio shinda, ukiajiliwa ile kamupuni au mtu alikuajili ana haki ya kwenda na kukuezesha upate resident permit sababu uko na kazi,lakini kando na hilo, sioni ANY MOTIVATION, huyu dada anawapa watu wanaotafuta ajira, kaa hii ni masters ya toka mzumbe au dar, hio singeona shinda kubwa nae, lakini huwezi kwenda toka tz mpaka usa ukapata masters, ukapata all that knowledge toka first world, ukawa exposed to all that technology, innovation and yale yote ambayo hufanyika pahali kaa marekani and for sure you came back to bongo to sell makande!!!!!!!!!!,sasa hata huko marekani angekuwa amepata ujuzi na maarifa ya kufanya kitu ambacho kitakuwa tofauti na mtu ambae amesoma tu bongo, yaani angeazisa hata micro finance credit inst, hata kaa sio kubwa kutumia hio ujuzi wa finance education ako nae,au hata kaa hana mtaji, then angeaza a consultancy firm ya kuwapa ushauri wale wanataka kuaza biashara ndogo au kubwa,au hata achukua hii nafasi ya ile kitu kinaitwa AGOA aaze ku export vitu huko amerika, mimi naona ajabu sana na huyu binti yetu, na ndio ninasema niko na mashaka makubwa kuhusu hii masters yake, this is not the way a person who trained in usa , who has a masters should be doing things, she ought to do something innovative and mordern in tech ways,
Utaambiwa wewe ni mvivu wa kufikiri!! From US to TZ for makande!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka watu wakupigie makofi basi wape wazo lako la kuendelea kuwa ndani ya Confort zone hapo utashangiliwa sana.

Dada wa MWANZA angekuja na Idea ya Kufungua Duka kali la Urembo angeshangiliwa sana, Duka la Nguoa watu wangeshangilia mno, Salooni kari ya kike watu wangeshangilia sana, Baa tungeshangilia sana.

Tungeshangilia kwa sababu ni vitu vya Confort zone zetu.


Ukitaka ukamwe basi waso lako la nje kabisa ya Confort zone wapelekee watu wa ndani ya Confort zone. Hahaaa hapo unakamwa milele

DADA MWENYE BIASHARA YA KANDE MWANZA nazani aliomba ushauri kutoka kwa watu wa walio kwisha toka kabisa nje ya Confort zone zao. la sivyo asingefanya ile biashara. yaani angeomba ushauri kutoka kwa watu kama sisi tungeishia kumwambia anajiabisha.


Nisha wahi kuleta Habari ya Dasa muuza Uji anaye soma Chuo watu waliponda sana wanaponda kwa sababu dada katoka nje ya Confort zone na si vinginevyo.


Wanao pondea Dada wa Mwanza ni kwa sababu yule Dada katoka nje ya Confort zone walizo zizoea wao. sasa hii ni tatizo kwetu watu wa Confort zone.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NGOJA NAMI NICHANGIE KIDOGO...
Tusipende sana wasomi kufanya mambo tofauti na carrier zao...
AFRIKA NI MASIKINI KWA SABABU WASOMI WENGI HAWAFANYI VILE WALIVYOSOMEA.. UNAKUTA KASOMEA IT LKN ANAUZA NGUO...
TUKUBALI KUWA TUMEPOTEA....
KAMA ALISOMEA UJASIRIAMALI BASI AMEPATIA SANA NA ANAFANYA KILE AMBACHO ANAPASWA KUFANYA ILA KAMA KASOMEA TOFAUTI NA HAPO YUKO WRONG NA HII NI KWA SABABU YA UMASIKINI WETU.
WASOMI WETU WAANGALIWE VIZURI NA KAMA NCHI LAZIMA TUWE NA SERA MADHUBUTI ZA KUWAWEZESHA HAWA WASOMI... TUSICHEKELEE UPUUZI HUU.. MTU KATUMIA GHARAMA KUBWA AFU ETI UNAMSIFIA KUUZA KANDE?? SI BORA ANGEANZA KUUZA TANGIA ZAMANI?? HAKUNA MWENYE KUSOMA AKAWAZA HAYO MAMBO.. ALWAYS HUTOKEA MARA BAADA YA KUSHINDWA KWA SERA ZETU ZA KUIINUA WASOMI WETU...
NCHI YA HOVYO SANA HII.. NA NI AIBU KWA TAIFA KWA WATU KUFANYA VITU AMBAVYO HAWANA UTAALAMU NAVYO..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nna degree ya SAUT nachoma mahindi hapa darajani hapa Mbeya.Huyo hafanyi biashara anajitangaza,tupo wengi huku tunatokea kwenye familia maskini mnoooo nadhani ndiyo maana hamtutangazi.....HAKUNA MTU HAPENDI KUFANYA KAZI,HAKUNA MTU ANAPENDA KULA BURE,SHIDA NI MTAJI NA KUPATA KAZI YENYEWE.
Degree ya SAUT ndio degree gani hiyo? Au ulimaanisha nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom