Binti wa miaka 17 ajinyonga baada ya kuachika mara tatu kwenye ndoa

Binti wa miaka 17 ajinyonga baada ya kuachika mara tatu kwenye ndoa

"Rebecca amefariki dunia baada ya kujinyonga hadi kupoteza maisha kwa kutumia kamba iliyosukwa kwa chandarua kwenye kenchi ya nyumba yake, chanzo alikuwa akilalamika kwamba kwanini kila akiolewa anaachika na tayari alikuwa ameshaachika mara tatu"
Miaka 17 kaachika mara 3, alianza kuolewa akiwa na umri gani?
 
Kuna kitu hakipo sawa kwenye jamii ambacho ndio kimepelekea maamuzi ya kujitoa uhai.

Miaka 17 mtu kuwa ameolewa mara tatu nalo ni jambo linafikirisha sana, kuwa ndoa zinyewe zinadumu kwa muda gani? Ni ndoa zinazotambulika kimila/kidini/kiserikali? Changamoto ya ndoa hizo kuvunjika ni ipi?

Ni mambo jamii yote kwa ujumla inapaswa kukaa chini na kuyatafakari vinginevyo tutakuwa tunapambana na matokeo kila siku badala ya kutatua mzizi wa shida yenyewe.
 
Leo tu hapa mtaani kuna brother kajinyonga kisa mapenzi. Mpaka muda huu naandika hii comment bado ananinginia juu ya mti polisi hawajafika kumtoa.
#Inasikitisha sana kujiua kisa mwanamke wakati wanawake wamejaa hadi wanamwagika🚶🚶🚶
 
Sasa tangu lini mtoto akaolewa na kumudu ndoa!?, apumzike tu.
 
Rebecca AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUJINYONGA hadi KUPOTEZA MAISHA.

Huko shuleni huwa mnaenda kusomea ujinga?
Uliza upate kupewa elimu.

Unajua kwanini hukumu ya kifo inatolewaga kwa maneno ya 'kunyongwa hadi kufa'?
 
Wazazi tujifundishe kuwakaribisha watoto wetu nyumbani baada ya divorce.

A divorced daughter is better than a dead daughter.

Jamii zetu za kiafrika zina shida sana mwanamke anapoachika sasa mabinti wanaweza kujikuta wanaingia kwenye ndoa ilmradi tu waonekane wameolewa.
Umenifanya nifikiri zaidi ya uwezo wangu. Ushauri mzuri Sana umetoa.
 
Back
Top Bottom