Manjagata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 13,942
- 15,371
Hujawahigi kusikia ndoa za utotoni wewe?Kumbe miaka 17 mabinti wameshaanza mapenzi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hujawahigi kusikia ndoa za utotoni wewe?Kumbe miaka 17 mabinti wameshaanza mapenzi
Miaka 17 ndoa 3? Huyu kuna roho mbaya ilikuwa inamuwinda kupitia mapenzi na imefanikiwa.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema Rebecca Benjamini Mkazi wa Kata ya Izunya Wilaya ya Nyang'hwale mwenye umri wa miaka 17 amefariki dunia kwa kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo baada ya kuwa anaachwa kila anapoolewa "Ameachika mara tatu kwenye ndoa"
Mwaibambe amesema hayo alipokutana na Kamati ya Amani na Maadili ya Mkoa wa Geita, ambapo amesema chanzo cha kifo cha Rebecca ni msongo wa mawazo ambao ulikuwa ukisababishwa na yeye kuolewa na kuachika mara kwa mara.
"Rebecca amefariki dunia baada ya kujinyonga hadi kupoteza maisha kwa kutumia kamba iliyosukwa kwa chandarua kwenye kenchi ya nyumba yake, chanzo alikuwa akilalamika kwamba kwanini kila akiolewa anaachika na tayari alikuwa ameshaachika mara tatu"
Baadhi ya Viongozi wa Dini aliokutana nao leo kutoka katika Madhehebu mbalimbali ili kutokomeza matukio ya Watu kuua na kujiua, wamesema Wananchi wanatakiwa kuwa na hofu ya Mungu.
Millard
Nashkuru nimepata mzazi (baba tofauti kidogo)ananiambiaga hivi ndoa ni mapenzj na huruma kama hakuna usiruhusu kunyanyasika sikukusomesha uwe mjinga na kukubali kua mtumwa be responsible woman but not stupid!Wazazi tujifundishe kuwakaribisha watoto wetu nyumbani baada ya divorce.
A divorced daughter is better than a dead daughter.
Jamii zetu za kiafrika zina shida sana mwanamke anapoachika sasa mabinti wanaweza kujikuta wanaingia kwenye ndoa ilmradi tu waonekane wameolewa.
Wasukuma wanaolewa na miaka 12 mbonaKuna kitu hakipo sawa kwenye jamii ambacho ndio kimepelekea maamuzi ya kujitoa uhai.
Miaka 17 mtu kuwa ameolewa mara tatu nalo ni jambo linafikirisha sana, kuwa ndoa zinyewe zinadumu kwa muda gani? Ni ndoa zinazotambulika kimila/kidini/kiserikali? Changamoto ya ndoa hizo kuvunjika ni ipi?
Ni mambo jamii yote kwa ujumla inapaswa kukaa chini na kuyatafakari vinginevyo tutakuwa tunapambana na matokeo kila siku badala ya kutatua mzizi wa shida yenyewe.
Please say u r jokingWasukuma wanaolewa na miaka 12 mbona
Wala sitanii ni ukweli kabisa! Nina uzoefu nishafundisha usukumani kule mtoto wa kike akiwa mweupe kusoma atakusikia kwenye bomba tu, nishawahi ishi na watoto wawili wa kike Shinyanga hukoo walitelekezwa na wazazi wao kwa kuwa wamefaulu std 7 na waliambiwa wasifaulu std 7 wakafaulu hivyo wazazi wakasusa kusomesha maana walikuwa washakula mahari za ng'ombe tayari..nawakumbuka mpk majina!please say u r joking
Mnashangaa hayo? Niliyaona Kibiti, binti wa Kindengereko ana umri wa miaka 15 na keshaolewa mara nne na sasa yupo chungu cha tano. Walijua hilo!17 ndoa tatu duuh......labda kama ni typing error
Sasa katika tukio hili jamii imehusikaje?! Yaani mtu awe depressed kwasababu zake binafsi lawama tupewe wanajamii?!Wazazi tujifundishe kuwakaribisha watoto wetu nyumbani baada ya divorce.
A divorced daughter is better than a dead daughter.
Jamii zetu za kiafrika zina shida sana mwanamke anapoachika sasa mabinti wanaweza kujikuta wanaingia kwenye ndoa ilmradi tu waonekane wameolewa.
Hata mwakiyembe alibisha mandishi Yake mwenyewe kipindi cha bunge la katibaUnabishana hadi na maandishi mkuu
Bila shaka umeamka na marue rue ukakimbilia kujibu bila kutafakari.Sasa katika tukio hili jamii imehusikaje?! Yaani mtu awe depressed kwasababu zake binafsi lawama tupewe wanajamii?!
Hebu mtupumzishe muda mwingine wanajamii tunalaumiwa hata na vitu visivyotuhusu. Miaka kumi na saba sio umri wa kulaumiwa kwa kukosa ndoa baada ya kutalikiwa.
Wanaweza koseaUnabishana hadi na maandishi mkuu
Usione anakusaidia hapo anakuandaa kuwa kiburi kwenye ndoa mwisho wake utaishia kuwa single mama, ndoa ni utumwa huru.Ukoa sahihi kabisa DadaNashkuru nimepata mzazi (baba tofauti kidogo)ananiambiaga hivi ndoa ni mapenzj na huruma kama hakuna usiruhusu kunyanyasika sikukusomesha uwe mjinga na kukubali kua mtumwa be responsible woman but not stupid!