Birthday yangu inakaribia, sina amani wala furaha, na sifurahii kitu

Birthday yangu inakaribia, sina amani wala furaha, na sifurahii kitu

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2010
Posts
4,219
Reaction score
4,608
Sina mke licha ya kwamba nina watoto wawili kwa mama wawili. Nina madeni kila idara, biashara haziendi kabisa na sikopesheki tena.

Nadaiwa NMB, NBC na Benki ya Maendeleo Bank Bank ya kanisa.

Nina msongo mkali sana wa mawazo maana mpaka sasa malI zangu zimepotea kwa kuziweka kama collateral kwenye taasisi mbalimbali za kifedha.

Kila siku iendayo mbele, napoteza tumaini na furaha.
 
317713073_1173812113510071_2600445049318717617_n.jpg
 
Acha kuzaa kuzaa ovyo alafu jitahidi kujikita kwenye kazi tafuta kazi ya ziada itayokukeep bize zaidi. Haya masuala ya kuzaa huku mara kule usipokuwa stable utafilisika sana, heri ujipange maisha yako uje uchukue wanao
Asante dada. Mungu akuepushe na kupata watoto kama unadhani watoto ni chanzo cha kuanguka kwa biashara
 
Sina mke licha ya kwamba nina watoto wawili kwa mama wawili. Nina madeni kila idara, biashara haziendi kabisa na sikopesheki tena...
Mkuu Mimi pia birthday yangu inakaribia na ninapitia same situation, Madeni mengi sana, Nimepoteza mali nyingi, hapa nakaribia kupoteza nyumba ninayoishi kama sio leo ni kesho, Maana leo ndio ilikuwa mwisho..

Daah! Sijui hata nafanyaje.. Kwa kweli nimechoka sana na sijui nafanya nini ,
 
Sometimes kila kitu kina stuck.

Ulikopeshekaje benk zote ? kwani huwa hakina database ?
Kuna biashara nyingi nilikuwa nafanya. Kuna mkopo nilichukua kwa ajili ya kujenga nyumba za biashara, collateral ikawa ni hizo nyumba.

Kuna mkopo mwingine nilikopa against FDR, FDR zikawa ndio collateral. Pia kuna mkopo mwingine niliuchukua shamba la mbao ndio lika secure mkopo huo.
 
Mkuu Mimi pia birthday yangu inakaribia na ninapitia same situation, Madeni mengi sana, Nimepoteza mali nyingi, hapa nakaribia kupoteza nyumba ninayoishi kama sio leo ni kesho, Maana leo ndio ilikuwa mwisho..

Daah! Sijui hata nafanyaje.. Kwa kweli nimechoka sana na sijui nafanya nini ,
Kwa kweli mtu anaweza akatucheka na kutuona hatuna akili, sometimes ni upepo tu umebadili uelekeo
 
Back
Top Bottom