Birthday yangu inakaribia, sina amani wala furaha, na sifurahii kitu

Ulitangatanga mno, biashara ukigeuza mgongo tu umepigwa.
 
Pole Sana, Ila mkopo ni kifungo ,debt is good but lazima iwe sustainable, principle kubwa kila mtu anafaa kujifunza ni kuwa usikope kupita kiasi. Tujifunze kujua net worth yako na income .
Never take on a loan ambayo inapita 20% of both your net worth and income , hapa Incase mambo yakienda mrama ,bado uko fiscal space yakulipa Hilo deni .
My advice tafuta rafiki au wakili akusaidie na debt restructuring as quick as possible .
Otherwise utapoteza assets zote ambazo uliweka collateral
 
Sawa mkuu
 
Kukopa sio tabu ila tatizo watu mnakopa mikopo ya Riba tena riba kubwa hatariii

Mm kwa imani yangu Muislamu aisee Mungu aniepushe na kuja kuchukua mikopo ya riba katika maisha yangu kwani Mungu wetu ameshatuahidi wala Riba wote wataangukia pabaya mnoo na hili linajionesha kwako mtoa mada

Mikopo ya Riba haifaii ni kuumizana sio kusaidiana
 
Sawa mkuu
 
Kama alivyotangulia kusema ndugu Bandar Abbas utafute wakili wa kukusaidia kuokoa vinavyowezekana. Mimi kwa kuongezea tafadhali anza kumalizana na ile mikopo ambayo unaona sio mikubwa. Wanaodai hela ndogondogo huwa ni hatari sana wanavyodai. Pia achana na mambo ya birthday kwa sasa. Ukikumbuka umri huku unadaiwa inaongeza ukubwa wa tatizo. Mimi pia niliwahi kupitia hiyo hali kwahiyo naelewa stress yake.
 
Are u Teacher dawa ya deni ni kulipa
 
Sasa ikawaje?
 
Kuna moments kwenye maisha unaweza jikuta umepoteza Kila kitu....yani I mean Kila kitu.....biashara zitakufa zooote, Hela zitaisha zooote Hadi utaomba elfu 5 Kwa watu halafu sasa utapoteza na watu wooote uliokuwa unawaona wako karibu na wewe....ila katika hiyo Hali omba sana Mungu usipoteze moyo na akili yako maana Kwa uzoefu wangu hicho kipindi kitapita na utagundua umejifunza mengi sana ya thamani ambayo usingeweza kuyafahamu kama mambo yote yangeendelea kua sawa.......tunza moyo wako, hayo yatapita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…