Birthday yangu inakaribia, sina amani wala furaha, na sifurahii kitu

Kweli ndugu ... hiki kipindi ni cha kulinda tu akili isivurugwe. Kinyume na hivyo ni kuanguka mazima...
 
Hiyo nyumba tafuta mwanamke,Katoe rushwa bakwata wakupe cheti Cha ndoa Cha zamani zaidi na huyo mwanamke,Kisha mpange kuzuwia Mali zako kupigwa mnada,aseme mlitafuta wote
 
Pole sana stress kwa binadamu ni kawaida ila inabidi upambane nazo huko mbele mambo yatakua sawa ww siyo mkamilifu yatapita tu
 
Daa binafsi naanza kuhisi kitu siyo cha kawaida(kizuri/kibaya) kwa sisi tuliozaliwa machi&Aprl.

Mi pia nilizaliwa 31/03/....
lakini katika docs zangu huwa natumia 01/04/....(naomba pia mnishauri kama ni mbaya kiroho/kidunia,,,

Basi bwana,pia binafsi napitia kipindi kigumu kama mtoa mada anavyopitia,
Nikekopa kote,
Nimeuza vyote ili kujinusuru lakin bado wapi!
Zaidi ninadeni jingime baya mno!
Naomba wataalam tuelezeni,nini hiki jamani!!
Hata nimeshindwa kihudumia watoto,mama yao kawaficha anasema mpaka nikilipa gharama zake ndo ananiruhusu kuwaona
 
Pole sana mkuu
 
Watoto kwa ss wasikupe shida ,Kama walipo wanakula ,na wapo sawa isikupe taabu ,cha msingi kaa chini chora ramani ya madeni ,Kisha piga plan yakutoka kwa madeni
 
Mshikaji anapitia kipindi kigumu, anahitaji faraja na si kashfa. Kuna siku utapita njia anayoipitia jamaa, utazikumbuka hizo kashfa na dharau unazozifanya leo
Humu bana kila mtu anajifanya mjanja kwenye tatizo la mwingine..kuna mwingine humu alisha pitishwaga kwenye changamoto mpaka akaja kulia shida hapa ila leo badala ya kumtia moyo mwenzake anajifanya shujaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…