Bisho Ntongo namuona kwenye kona, inasikitisha sana, wametoboa mtumbwi sasa

britanicca

Platinum Member
Joined
May 20, 2015
Posts
18,261
Reaction score
48,864
Hapumui vema, halali Usingizi ukaja, Kibubu kinapukutika kwa kasi sana, Mtungi wa maji unatoa sauti ya kukanyagwa juu na panya na sauti inaogofya sana kuna ishara hata maji hakuna Tena.

Wale wale walotaka kutunyula burunji naye nao wameangalia pembeni Kama hawamuoni.

Kilemba chawasha kichwani Kama aliyesukwa na mkono wa kushoto, Mambo si mambo bundi anatoa mlio wa kuku kumsogeza karibu, kumbe ni bundi, Bisho bisho bisho.

Sauti za faragha kutoka kwenye minong’ono ya Mahaba ndio inamuongoza jinsi ya kuyachota maji mtoni.

Kinachoniliza sana ni mto anaoekekea njia anayoelekezwa kuna Chatu, kwenye mto husika kuna mamba, cha kushangaza zaidi ndoo aloambiwa atumie imejaa siafu na ameweka kichwani bila kuikagua,

Cha kulia na kulilia kabisa kabla hajafika ambako kuna Chatu hapo kati kwenye msitu kuna njemba zinazobaka akina mama.

Safari na matukio yamejaa Giza,

Namsihi aitue ndoo haraka na asiendelee kule kuchota maji, kitakachomsumbua ni siafu tu watakao kuwa wameshaingia kwenye nguo za ndani Ila ni vema kuliko kubakwa, kumezwa na chatu au mamba

Britanicca
 
Hapumui vema, halali Usingizi ukaja,
Kibubu kinapukutika kwa kasi sana,
Mtungi wa maji unatoa sauti ya kukanyagwa juu na panya na sauti inaogofya sana kuna ishara hata maji hakuna Tena,
Wale wale walotaka kutunyula burunji naye nao wameangalia pembeni Kama hawamuoni,
Kilemba chawasha kichwani Kama aliyesukwa na mkono wa kushoto,
Mambo si mambo bundi anatoa mlio wa kuku kumsogeza karibu, kumbe ni bundi ,
Bisho bisho bisho,
Sauti za faragha kutoka kwenye minong’ono ya Mahaba ndo inamuongoza jinsi ya kuyachota maji mtoni

Kinachoniliza sana ni mto anaoekekea njia anayoelekezwa kuna Chatu, kwenye mto husika kuna mamba, cha kushangaza zaidi ndoo aloambiwa atumie imejaa siafu na ameweka kichwani bila kuikagua,

Cha kulia na kulilia kabisa kabla hajafika ambako kuna Chatu hapo kati kwenye msitu kuna njemba zinazobaka akina mama

Nimetoka kapa japo nahisi ni dongo la kisiasa kwa nanii mgawa fedha
 
Hana picha
 
Wewe unatania. Akina Waziri, Abdul na jeshi zima la "Genge" hawawezi kuruhusu aishie njiani. Utamu wa madaraka umekwisha waingia ndani ya mifupa.

Safari ni safari tu, hadi mtoni wakapambane na mamba huko huko! Kwani chatu ni kitu gani?
 
Back
Top Bottom