Nadhani tungetizama malengo ya kila mmoja halafu tutapata picha which is which.
Kampeni ya Israel ilikuwa na malengo makuu manne : kuitokomeza Hamas, kuwaachilia mateka, kuhakikisha Gaza haileti tishio tena kwa Israeli, na kuwarudisha wakaazi waliokimbia makazi yao Kaskazini mwa Israeli.
Israel imeshindwa kufikia malengo yake makuu, kama vile Marekani ilivyoshindwa huko Afghanistan na Vietnam.
Watu wanapaswa kuelewa: Kwa serikali kushinda dhidi ya wanamgambo kama Hamas au Hezbollah, nguvu haitoshi; unapaswa kushinda mioyo ya watu. Inabidi utoe mbadala bora kuliko hali ilivyo--katika kesi hii, Hamas. Inahitaji suluhisho la kisiasa, suluhisho la kiitikadi, sio la kijeshi. Lakini Israeli hawakushinda mioyo ya watu, kinyume chake kabisa. Israel na Marekani zilishindwa kuwaondoa kabisa kutoka Gaza--lengo lao kuu.
Hata Blinken juzi alisema Hamas imeongeza wapiganaji wengi zaidi hivi sasa kuliko walivyokuwa kabla ya vita.
Na vipi kuhusu mateka? Kuwaachilia mateka iliipaswa kuwa kipaumbele cha kwanza lakini Sio tu kwamba makumi yao bado wako mikononi mwa Hamas, lakini baadhi yao waliuawa wakati wa mashambulizi ya anga ya Israeli.
Badala ya kutokomeza Hamas, Israel imejifanya kuonekana kama taifa la kihuni, na Hamas wametoka katika hali hii wakionekana kama "watetezi" wa upinzani wa Palestina.
Sisemi Hamas hawana lawama, La hasha. Lakini jibu la maelfu ya mabomu hayakuitokomeza Hamas; iliimarisha masimulizi yao. Kila bomu lililoua raia, kila mtoto aliyetolewa kutoka kwenye vifusi, kila familia iliyokata tamaa iliyoachwa bila chakula au maji-yote hayo yalivhochea mashine ya propaganda ya Hamas.
Kijiografia, sifa ya Israeli imeharibika, limebakia sasa kama taifa pariah.Nchi nyingi (kama Uhispania, Ireland, Norway..nk) zimelitambua rasmi taifa la Palestina na hata kujiunga na kesi ya afrika kusini dhidi ya israel
Sifa ya Israel Kimataifa imechafuka. Viongozi wake wanatafutwa rasmi kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu. Wanajeshi wa IDF wamesimamishwa kote ulimwenguni. Kuna kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel na taswira yake imeharibiwa vibaya.
Kwa upande wa Palestina, ni wazi.. Gaza imeharibiwa. Zaidi ya 100k waliuawa na bado hakuna taifa la Palestina. Bado wanaishi bila utaifa chini ya vizuizi vya Israeli.
Hamas Walipata kabisa walichotaka. Walitaka kusalia madarakani, kurudisha sababu ya Palestina kuwa nchi huru, kuizuia mpango wa normalization wa Israel na Saudia na kusaidia wafungwa wa kipalestina kutoka jela.
Vita hivi vinaendea kwisha, lakini cha kusikitisha ni kwamba tatizo la Waisraeli na Wapalestina bado halijaisha. Mzozo utaendelea kwa miaka ijayo.