Heshima Zenu wakuu🙏
Wakuu huku Kanda ya Ziwa jambo kuwa na mganga /mtaalamu wako ni kawaida kabisa kama ninyi huko kuwa na Daktari wako Ambae shida yoyote ikijitokeza basi unamwelezea hata simu ndo akuambie nenda kapime hiki na kile then majibu unitumie.
Kanda ya Ziwa Sasa nao wako hivyo Kwa kinyume chake badala ya madaktari wao Wana waganga kalumanzila au sangoma Kwa majina maalufu.
Naungana na Uzi wa
PharaohMtakatifu ulikuwa unasema.
Kanda ya Ziwa Kila familia Ina mganga wake.(Sijui kuuleta hapa Uzi naomba
Moderator mlete hapa pia huo Uzi yaani link yake tu)
Na sema hayo nikiwa mwenyeji wa huko wa kuzaliwa na kuishi huko pia. Ule Uzi una ukweli 100%
Ule Uzi umeelezea matukio kadhaa kausomeni mtaona mengi sana na sitaki kuyaleta hapa.
Sasa huku Kanda ya Ziwa alichokisahau Mr
PharaohMtakatifu ni kuwa Kuna shule za kufundishwa uchawi,ushirikina Kwa tiketi ya uganga wa kienyeji na kunakuwa na leseni kabisa. Na Kila mwaka wahitimu zaidi ya 300 wanahitimu uganga.
Kwa kifupi mganga na mchawi ni mapacha waliofanana kabisa yaani kulwa na dotto. Asikudanganye mtu kuhusu hili nimeishia Kwa waganga najua sehemu kubwa sana.
Kuna kitu huitwa shingila(yaani ni kitu fln ama kiungo Cha Mnyama ama mtu huhitajika Ili kuifanya dawa Ile ikamilike na kufanya kazi) hapo ndo utasikia unaambiwa katika dawa hiyo kalete mchanga wa baharini ama kalete jino la mtu aliyepata ajari ama hata damu ya kondoo mweupe mwili mzima au nywele za maiti. Hizi ndo huitwa shingila sijui jina lake Kwa kiswahili.
Piga picha watu wanahitimu zaidi ya 300 Kila mwaka kwenda kuanza uganga wee unadhani hii ni idadi ndogo?
Tuyaache hayo .
Sasa ijue Dawa ya (msalaba) Bhunganga wa Nsalaba.
Hii Dawa wengi sana wamekuwa wakiitumia wenye uchu wa kupata Mali kwani wanasema masharti yake ni nafuu sana na Haina masharti makali kama kuua na kafara za watu.
Baadhi ya masharti ya Bhunganga wa Nsalaba ni:-
Hutakiwi kuchepuka. Moja ya shart gumu ni hili hupaswi kabisa kuwa na mchepuko hata mmoja au hata Kwa bahati mbaya hutakiwi.
Badala yake unaruhusiwa kuongeza mwanamke mwingine kadiri uwezavyo isipokuwa tu kuzini. Mara ukifanya hivyo basi utajiri wako utaisha ghafla sana.
Haitakiwi uwe mchafu. Dawa hii inakulazimu uwe msafi muda wote. Mara zote inatakiwa nguo ziwe safi na unyunyu Kwa mbali kama utaweza. Hata kama unafuga ngo'mbe,kuku nk hutakiwi kiwanja kiwe na mavi muda wote hapana haipendi hivyo hiyo dawa.
Dawa hii inakulazimu usitumie dawa nyingine yoyote ya kienyeji.
Mara tu ukianza kutumia hii dawa basi hupaswi kabisa kuwa na dawa Nje ya dawa hiyo!!
Iwe ni shambani,biashara nk tumia Dawa hiyo hiyo hata kama wewe ni kiongozi kupanda cheo nk tumia hiyo hiyo usiende huko na kule kutafuta dawa nyingine.
Dawa hii inataka kafara za wanyama. Hii itakulazimu Kila mwezi utoe kafara ya damu kama. Ni njiwa ama wanyama. Hutegemea na mhusika alivyo.
Hii dawa mara zote wahusika Huwa na kanzu na vibaragashia sijui kama Kuna uhusiano na dini fln maana hata wanawake hufunika vichwa vyao
Kwa uchache ndo hayo baada ya kumuuliza mmoja wao aliyetoka kujifunza uganga wa jadi kahama huko ndani ndani.
View: https://youtu.be/QMVdjPJB3k8?si=E9z0zRx38Ri_K5c0
Zipo nyingi sana lakina nakuacha na hizi chache
Msanii huyu anaitwa Gude gude huimba nyimbo za kutukuza sana Ile dawa ya Nsalaba. Kama lugha ya kiratino unapanda ingia ukamtazame .
View: https://youtu.be/y-dP_sxB0i8?si=rDT0qOv91NdO8hZj
View: https://youtu.be/QMVdjPJB3k8?si=fXMk1xpu2OkKMtbC.
Shimba ya Buyenze bila shaka ushawahi sikia hili.
Kwenye picha ni baadhi ya wahitimu
Manyanza View attachment 3143145View attachment 3143146