uko sahihi. Tanzania tuna tatizo la mafundi si magari yenyewe. Na ni Tz tu tulioingizwa kwenye maisha ya toyota mno tangia uwepo wetu. Hata Burundi wanatuzid kuyaelewa haya magari.
Lakin ukweli ni kuwa huwezi linganisha ubora na raha ya eurocars dhidi ya Toyota.
Nina kisa kama chako. Jamaa aliniuzia x3 m9 kisa haitengenezeki kwa tatizo la nguvu na dashboard inawaka kama yote. Fundi yule yule wa mazoea ya kifamilia.
Sasa nikahangaika nayo ikafkisha m4 nanunulishwa kila spare za kuagiza tena mwenyewe kila wakipima ni mfumo wa hewa mara air mass, mara censors, had nikajua kila part ya injini.
Ndipo fund wa 7 akaja kugundua ni exhaust tu zimeziba eneo la masega (haitumii unga). At 30km/h inazima. No power. Ndo ikapona kwa 120k nimeshatumia zaid ya 4m.
Ndo nikajua wap tunakwama. Mafund wetu si proffessional na hawana vitendea kaz vya kisasa kugundua hitilaf. Lakin kwa sasa kuna improvements.
Mwaka 2012 horn ya benz E class iliacha kufanya kazi niko mkoan. Pengine kote ikiwa nzima kabsa. Fund akaloop tu na ikapiga. Ajab gari haikutoka had leo. Haikuwaka had kustart. Inalia tu. Mara ooh control box imeshot. Mara censor ya mafuta inaachia yote. Ilipofika m3 nikaachana nayo mana nilishauriwa kuweka injini ingine au ya toyota 3s.