Jifunzeni kuheshimu kazi za watu, msipende kujudge, kudhihaki na kutusi kazi fulani kwa kuangalia kundi dogo.
Wapo boda waruru na hovyo pia wapo boda makini na wastaarabu, kama zilivyo kazi nyingine.
Tukubaliane kwamba katika kila kundi la kazi au fani flani kuna kundi la watu makini na kuna kundi la watu wa hovyo, hivyo kukutana na mtu wa hovyo katika kazi haimaanishi kuwa wote ndio wako hivyo.
Nazungumza haya maana kuna bodaboda kadhaa ninao fanyanao kazi ni watu makini na wanaojielewa, miongoni mwao wamejenga na kuanzisha biashara nyingine kupitia boda.