Mbinu ya huyu mama ni kushika boda boda, kushika timu za mipira, na kushika waarabu.
Ili kipindi cha kampeni atumie washabiki wa timu kumpatia huruma ya ushindi.
2. Kushika boda boda ili wamuonee huruma wakati wa kampeni.
3. Waarabu wamwagwe pesa..
Watanganyika kuweni makini na huyu mama, ndiye anayejua kilichompata Jiwe.
Huyu tokea mwanzo, aliporithi kiti hakuchelewa kuanza kampeni, ila sasa naona kama anajihisi kuwa amechelewa, ndiyo maana anahangaika sana.
Alianza na kundi la "WASANII"..., ikawa kama kundi hilo halimsaidii sana.
Kaingia kwenye timu za mpira, nako hana lolote la maana linaloonekana kumsaidia kwenye harakati zake
Kajaribu hadaa za kila namna, kuwafanya akina Mbowe kuwa "MAGAIDI", halafu na kujifanya yeye ndiye mwokozi wao..., hili nalo likafikia mwisho bila ya kumpa heshima yoyote baada ya kuonekana kuwa ni mwigizaji tu ambaye hakuwa na nia thabiti ya kuleta maelewano katika jamii.
Kafanya kila aliloweza, aonekane kuwa yeye ni tofauti na aliyemrithi kwenye kiti hicho, ili avute hisia za waliokuwa wakimsema vibaya Magufuli; huko nako, pamoja na kuwapata watu, lakini akawa anapoteza kundi lililokuwa nyuma ya Magufuli.
Ili kulipoza kundi hilo, na aonekane bado anaye Magufuli, kaigiza "Kazi na iendelee...". Kazi itaendelea vipi wakati unanajisi aliyokuwa akiyasimamia Magufuli?
Kazunguka kila sehemu, aonekane kwa waTanzania kuwa kiongozi mzuri. Lakini kwa bahati mbaya kwake, alipokubali tu kutekwa na kundi/genge la akina Roast..., hapo akawa hana njia tena ya kujifichia
Ni mtu asiyekata tamaa kirahisi, bado anadhani anayo matumaini ya kukoga nyoyo za waTanzania, ndiyo sababu unaona vitendo kama hivi vya mapikipiki, na hii ya juzi ya kuwaingiza watu wa mitandao ya kijamii mbele ya waandishi wa habari. Tegemeo lake sasa ni kuwa, hao 'influencers' watamsaidia kuwavuta waTanzania.
Niseme hapa, huko asiwe na tegemeo kabisa.
Njia ya mwisho ambayo inaanza kujipambanua, ni kutumia nguvu, kama ilivyozoeleka miaka yote kutoka kwa CCM.
Watalazimisha Bandari, na kama baada ya hivyo watakuwa bado wapo madarakani, nguvu zote watazielekeza kunajisi 2024 na 2025.
Hivi kweli Tanzania itabaki salama na mipango ya namna hii safari hii?
Mimi nasema. Hapana. Safari hii CCM watalipata wanalolitafuta siku nyingi.