Bodi ya ligi haitanii, yatoa ratiba ya derby ya Kariakoo. Sasa kupigwa Juni 15, 2025

Bodi ya ligi haitanii, yatoa ratiba ya derby ya Kariakoo. Sasa kupigwa Juni 15, 2025

Joined
May 4, 2024
Posts
37
Reaction score
190
Bodi ha Ligi imetoa ratiba za viporo vilivyobaki, huku ikifanyia pia marekebisho ya tarehe kwa baadhi ya michezo.

Jambo kubwa zaidi ni kuwa derby ya Kariakoo bado ipo palepale, itapigwa Juni 15, 2025, saa 11:00 Jioni uwanja wa Benjamin Mkapa.

Hii inajiri masaa machache baada ya Klabu ya Yanga kuweka msimamo kuwa hawachezi mechi husika baada ya kudondokea pua kule CAS.

1000333141.jpg


Pia soma Bodi ya ligi kupanga ratiba mpya ya derby ni kudharau maamzi ya CAS
 
KARIAKOO DERBY: Bodi ya Ligi Tanzania imetoa ratiba ya mechi zilizosalia kwenye NBC Premier League pamoja na CRDB Bank Federation Cup, ambapo mchezo kati ya Yanga dhidi ya Simba, sasa kupigwa Juni 15, 2025 majira ya saa 11:00 jioni katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Ligi hiyo inatarajiwa kumalizika Juni 22, 2025 huku fainali ya CRDB Bank Federation Cup kupigwa kati ya Juni 26-28.

1746503206708.jpg
 
Wakuu

Taarifa zinaeleza kuwa mchezo wa Kiporo kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC umepangwa kufanyika June 15, 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa saa kumi na moja jioni (17:00 pm).

Bodi ya ligi imefanya maboresho ya ratiba ya ligi kuu ya NBC na sasa ligi itaisha June 22, 2025.

Je, Yanga kubaki na msimamo wao wa kutopeleka timu uwanjani?

IMG_4708.jpeg
 
Watatema ndoano hao bodi ya league hizi timubl Zina nguvu kuliko Chadema na ccm na hakuna virungu maana hata hao ma Police ni sehemu ya hizi team, ni wakati sqsa Young Africans wauonyeshe ulimwengu kwamba bodi ya league sio kila kitu
 
Wakuu

Taarifa zinaeleza kuwa mchezo wa Kiporo kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC umepangwa kufanyika June 15, 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa saa kumi na moja jioni (17:00 pm).

Bodi ya ligi imefanya maboresho ya ratiba ya ligi kuu ya NBC na sasa ligi itaisha June 22, 2025.

Je, Yanga kubaki na msimamo wao wa kutopeleka timu uwanjani?

View attachment 3325755
Yanga mwaka wa taabu
 
Back
Top Bottom