Bodi ya Ligi: Kama Yanga wameenda CAS ni kichekesho, busara itumike sio kanuni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Sakata la kuahirishwa kwa mechi ya Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba, iliyokuwa ichezwe Machi 8, 2025, limechukua sura mpya. Awali, suala hili lilionekana kama masihara, lakini sasa linaonekana kuingia katika hatua nzito.

Mwananchi Digital imebaini kuwa Yanga imewasilisha rasmi kesi hiyo katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) jijini Lausanne, Uswisi, baada ya kutoridhishwa na majibu ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Soma: Yanga Yafungua malalamiko CAS dhidi ya bodi ya ligi

Licha ya hatua hiyo, hakuna kiongozi yeyote aliyekubali kunukuliwa kwa jina, wakidai kuhofia mamlaka za soka na serikali. Hata hivyo, inadaiwa kuwa CAS itawasiliana rasmi na TFF pamoja na Bodi ya Ligi ili kuthibitisha kupokea rufaa hiyo. Yanga inasisitiza kuwa haijaridhika na maamuzi ya ndani, hivyo imechukua hatua hiyo kutafuta haki kwenye chombo cha juu zaidi cha usuluhishi wa michezo duniani.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mnguto, amesema tayari wamejibu barua ya Yanga na hawana mamlaka ya kuwazuia kwenda CAS lakini kama wameenda CAS kwa kipindi hiki ambapo hawajasema kuwa hilo suala limeamriwa vipi itakuwa ni kitu cha kuchekesha, akisisitiza kuwa maamuzi ya mwisho ya bodi bado hayajatolewa, akiamini kuwa suluhu inaweza kupatikana kupitia vikao vya ndani. Ameeleza kuwa busara na hekima zinapaswa kutumika ili kila upande uridhike badala ya kupeleka suala hilo nje ya nchi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa hili Bodi ya Ligi na Simba waliyumba sana. Zipo kanuni nyingi za ligi, sasa haiwezekani kila timu pinzani inapokiuka kanuni mojawapo kuelekea mchezo hitimisho liwe kuahirisha mchezo husika. Kuna timu ililazimishwa kucheza bila ambulance kinyume na kanuni na baadhi ya viongozi wao walifungiwa; inakuwaje Simba "kuzuwiwa tu na vibaka" kufanya mazoezi mechi inaahirishwa? Yapo mazingira yanaweza fanya mechi kuahirishwa lakini hili la Simba sidhani kama ni miongoni. Kwa mazingira ya Tanzania na kwa ligi yetu TFF na Bodi ya Ligi wanajitengenezea mazingira magumu huko mbeleni na inaweza kuja kuleta mgogoro mkubwa zaidi. Msimu uliopita kule Kaitaba Azam hawakuwashiwa taa za uwanjani wakati wa kufanya mazoezi na iliwalazimu kutumia taa za magari.
 
Huyu mzee anazeeka vibaya,why atie tie huruma na sheria anazo.

Anzia pale barua ya bodi ya Ligi
ilipoishia kisha uone nani haleti Team baada ya kutangaza tarehe mpya.
Gawa point maisha yaendelee.
 
Sakata la kuahirishwa kwa mechi ya Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba, iliyokuwa ichezwe Machi 8, 2025, limechukua sura mpya. Awali, suala hili lilionekana kama masihara, lakini sasa linaonekana kuingia katika hatua nzito.

Mwananchi Digital imebaini kuwa Yanga imewasilisha rasmi kesi hiyo katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) jijini Lausanne, Uswisi, baada ya kutoridhishwa na majibu ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Soma: Yanga Yafungua malalamiko CAS dhidi ya bodi ya ligi

Licha ya hatua hiyo, hakuna kiongozi yeyote aliyekubali kunukuliwa kwa jina, wakidai kuhofia mamlaka za soka na serikali. Hata hivyo, inadaiwa kuwa CAS itawasiliana rasmi na TFF pamoja na Bodi ya Ligi ili kuthibitisha kupokea rufaa hiyo. Yanga inasisitiza kuwa haijaridhika na maamuzi ya ndani, hivyo imechukua hatua hiyo kutafuta haki kwenye chombo cha juu zaidi cha usuluhishi wa michezo duniani.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mnguto, amesema tayari wamejibu barua ya Yanga na hawana mamlaka ya kuwazuia kwenda CAS lakini kama wameenda CAS kwa kipindi hiki ambapo hawajasema kuwa hilo suala limeamriwa vipi itakuwa ni kitu cha kuchekesha, akisisitiza kuwa maamuzi ya mwisho ya bodi bado hayajatolewa, akiamini kuwa suluhu inaweza kupatikana kupitia vikao vya ndani. Ameeleza kuwa busara na hekima zinapaswa kutumika ili kila upande uridhike badala ya kupeleka suala hilo nje ya nchi.

Chanzo: Mwananchi
Najiuliza hivi, huyu bwana anasema bodi ya ligi hawajafanya maamuzi, kwani;
1. Kughairisha mechi siyo maamuzi?
2. Kutopeleka waamuzi uwanjani hayakuwa maamuzi?
 
Kwa hili Bodi ya Ligi na Simba waliyumba sana. Zipo kanuni nyingi za ligi, sasa haiwezekani kila timu pinzani inapokiuka kanuni mojawapo kuelekea mchezo hitimisho liwe kuahirisha mchezo husika. Kuna timu ililazimishwa kucheza bila ambulance kinyume na kanuni na baadhi ya viongozi wao walifungiwa; inakuwaje Simba "kuzuwiwa tu na vibaka" kufanya mazoezi mechi inaahirishwa? Yapo mazingira yanaweza fanya mechi kuahirishwa lakini hili la Simba sidhani kama ni miongoni. Kwa mazingira ya Tanzania na kwa ligi yetu TFF na Bodi ya Ligi wanajitengenezea mazingira magumu huko mbeleni na inaweza kuja kuleta mgogoro mkubwa zaidi. Msimu uliopita kule Kaitaba Azam hawakuwashiwa taa za uwanjani wakati wa kufanya mazoezi na iliwalazimu kutumia taa za magari.
Utopolo nyie mbona mliahirisha mechi kusogezwa dakika 60 tu
 
Utopolo nyie mbona mliahirisha mechi kusogezwa dakika 60
 
Mkileta timu tunamtuma edna Lema awafunge na Yanga Princess

Yaani hamtakimbia kufungwa na Yanga Kwa mara ya 5 mfululizo
Sasa kama mnajiamini kuifunga Simba kwanini mmekimbilia CAS kutafuta alama za mezani wakati hakuna procedures zilizofuatwa ili timu ipewe alama za mezani?

Je, jopo la waamuzi lilifika uwanjani kuwasubiri na baada ya Simba kutofika uwanjani refarii akamaliza mpira kwa mujibu wa kanuni?

Kama mnajiamini subirini tarehe mpya ipangwe mlete timu muone zahma itakayowakuta.
 
Back
Top Bottom