Bodi ya Ligi: Kama Yanga wameenda CAS ni kichekesho, busara itumike sio kanuni

Sasa kama mnajiamini kuifunga Simba kwanini mmekimbilia CAS kutafuta alama za mezani wakati hakuna procedures zilizofuatwa ili timu ipewe alama za mezani?

Je, jopo la waamuzi lilifika uwanjani kuwasubiri na baada ya Simba kutofika uwanjani refarii akamaliza mpira kwa mujibu wa kanuni?

Kama mnajiamini subirini tarehe mpya ipangwe mlete timu muone zahma itakayowakuta.
Je.!! Ni jukumu la Yanga kupeleka jopo la waamuzi uwanjani? Uzembe wa watu wengine kukamilisha majukumu yao, hakuwezi kuwa sababu ya Yanga kuonewa.
 
Ushafika CAS mkuu? Wenzako wanakula posho za safari ujue.
hv huko CAS kuna kesi yanga ameshawahi kushinda?maana kesi zote za huko wanaishia kupgwa faini tu na kufungiwa kusajili
 
Sasa kama mnajiamini kuifunga Simba kwanini mmekimbilia CAS kutafuta alama za mezani wakati hakuna procedures zilizofuatwa ili timu ipewe alama za mezani?

Je, jopo la waamuzi lilifika uwanjani kuwasubiri na baada ya Simba kutofika uwanjani refarii akamaliza mpira kwa mujibu wa kanuni?

Kama mnajiamini subirini tarehe mpya ipangwe mlete timu muone zahma itakayowakuta.
Yanga Nia yetu ni kuwaonyesha TFF na bodi ya ligi wawajue huko ulimwengumi

Lakini kuwafunga Simba tupo tayari kuwapiga 5 hata kesho
 
Je.!! Ni jukumu la Yanga kupeleka jopo la waamuzi uwanjani? Uzembe wa watu wengine kukamilisha majukumu yao, hakuwezi kuwa sababu ya Yanga kuonewa.
Kanuni zipo wazi ili timu ipewe alama za mezani maana yake lazima protocol zote zifuatwe sio unadai alama za mezani wakati hakuna hata protokali iliyofanyika.

Mechi iliahirishwa ili bodi ya ligi ijipe muda wa kutosha kufanya uchunguzi wa tukio la Simba kuzuiliwa kufanya mazoezi kwa mujibu wa kanuni kitu kilichopelekea Simba kufanyiwa vitendo vya uvunjifu wa amani.

Sasa mechi imeahirishwa kwa mamlaka waliyokuwa nayo bodi ya ligi kuu wewe unapeleka timu uwanjani huku ukijua mechi haipo halafu unataka alama tatu za mezani.

Kiukweli pale Yanga panahitajika mabadiliko ya kiuongozi kuanzia idara ya sheria hadi Rais wa klabu maana huwa wanafanya mambo kwa kukurupuka.
 
Najiuliza hivi, huyu bwana anasema bodi ya ligi hawajafanya maamuzi, kwani;
1. Kughairisha mechi siyo maamuzi?
2. Kutopeleka waamuzi uwanjani hayakuwa maamuzi?
kingine Kwenye barua yao ya bodi walisema mechi itapangwa tarehe nyingine, hayo si maamuzi tayali.
Hawakujali Mashabiki, Timu(Yanga), na media wametumia gharama kiasi gani sababu ya hii mechi, wao wameangalia upande mmoja tu wa simba, mimi nadhani wajitafakari na ikiwezekana wajiuzuru kabisa hao viongozi wa bodi ya ligi
 
Kanuni zipo wazi ili timu ipewe alama za mezani maana yake lazima protocol zote zifuatwe sio unadai alama za mezani wakati hakuna hata protokali iliyofanyika.

Mechi iliahirishwa ili bodi ya ligi ijipe muda wa kutosha kufanya uchunguzi wa tukio la Simba kuzuiliwa kufanya mazoezi kwa mujibu wa kanuni kitu kilichopelekea Simba kufanyiwa vitendo vya uvunjifu wa amani.

Sasa mechi imeahirishwa kwa mamlaka waliyokuwa nayo bodi ya ligi kuu wewe unapeleka timu uwanjani huku ukijua mechi haipo halafu unataka alama tatu za mezani.

Kiukweli pale Yanga panahitajika mabadiliko ya kiuongozi kuanzia idara ya sheria hadi Rais wa klabu maana huwa wanafanya mambo kwa kukurupuka.
Kwahiyo haya uliyoyaandika wewe mwenyewe ndo unaona umejibu swali langu?? Nakuuliza tena, Je.!! Ni jukumu la Yanga kupeleka jopo la waamuzi uwanjani?
 
Yanga Nia yetu ni kuwaonyesha TFF na bodi ya ligi wawajue huko ulimwengumi

Lakini kuwafunga Simba tupo tayari kuwapiga 5 hata kesho
Hamtafanikiwa maana hakuna protokali ya mchezo iliyofuatwa.

Mechi iliahirishwa kwa mamlaka iliyopewa bodi ya ligi kama ilivyopewa mamlaka ya kupanga ratiba vile vile ina mamlaka ya kupangua ratiba.

Idara ya sheria ya klabu ina shida sio bure.
 
Sasa kama mnajiamini kuifunga Simba kwanini mmekimbilia CAS kutafuta alama za mezani wakati hakuna procedures zilizofuatwa ili timu ipewe alama za mezani?

Je, jopo la waamuzi lilifika uwanjani kuwasubiri na baada ya Simba kutofika uwanjani refarii akamaliza mpira kwa mujibu wa kanuni?

Kama mnajiamini subirini tarehe mpya ipangwe mlete timu muone zahma itakayowakuta.
Yote mnaweka vitisho ili Yanga wasilete timu maana mnaogopa kitakachofuata. Mambo yakiwekwa sawa Yanga itacheza mechi ya derby bila shida. Tusubiri tuone hiyo Zahma
 
Kwahiyo haya uliyoyaandika wewe mwenyewe ndo unaona umejibu swali langu?? Nakuuliza tena, Je.!! Ni jukumu la Yanga kupeleka jopo la waamuzi uwanjani?
Utapelekaje jopo la waamuzi uwanjani wakati mechi imeahirishwa?

Wewe mzee vipi? Vitu vidogo kama hivi unashindwa kuvielewa?

Jukumu la kupeleka waamuzi uwanjani ni la TFF/Bodi ya ligi endapo tu mchezo husika upo ila kama hao hao wanaowajibika kupeleka waamuzi uwanjani wameahirisha mchezo watapelekaje waamuzi uwanjani?

Mbona ni suala la kutumia simple logic tu hili.
 
Hamtafanikiwa maana hakuna protokali ya mchezo iliyofuatwa.

Mechi iliahirishwa kwa mamlaka iliyopewa bodi ya ligi kama ilivyopewa mamlaka ya kupanga ratiba vile vile ina mamlaka ya kupangua ratiba.

Idara ya sheria ya klabu ina shida sio bure.
Mambo siyo rahisi kama unavofikiri
Mechi haihirishwi kama vicoba
Bodi ya ligi kutoleta match officials hilo haituhusu Yanga, kikubwa Yanga walitimiza jukumu lao kikanuni,
 
Utapelekaje jopo la waamuzi uwanjani wakati mechi imeahirishwa?

Wewe mzee vipi? Vitu vidogo kama hivi unashindwa kuvielewa?

Jukumu la kupeleka waamuzi uwanjani ni la TFF/Bodi ya ligi endapo tu mchezo husika upo ila kama hao hao wanaowajibika kupeleka waamuzi uwanjani wameahirisha mchezo watapelekaje waamuzi uwanjani?

Mbona ni suala la kutumia simple logic tu hili.
Yanga asiadhibiwe kwa makosa ya wengine. Hiyo unayoiita simple logic, ndo inasabaisha akina Karia kuropoka aliyoyaropoka
 
Sakata la kuahirishwa kwa mechi ya Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba, iliyokuwa ichezwe Machi 8, 2025, limechukua sura mpya. Awali, suala hili lilionekana kama masihara, lakini sasa linaonekana kuingia katika hatua nzito.

Mwananchi Digital imebaini kuwa Yanga imewasilisha rasmi kesi hiyo katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) jijini Lausanne, Uswisi, baada ya kutoridhishwa na majibu ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Soma: Yanga Yafungua malalamiko CAS dhidi ya bodi ya ligi

Licha ya hatua hiyo, hakuna kiongozi yeyote aliyekubali kunukuliwa kwa jina, wakidai kuhofia mamlaka za soka na serikali. Hata hivyo, inadaiwa kuwa CAS itawasiliana rasmi na TFF pamoja na Bodi ya Ligi ili kuthibitisha kupokea rufaa hiyo. Yanga inasisitiza kuwa haijaridhika na maamuzi ya ndani, hivyo imechukua hatua hiyo kutafuta haki kwenye chombo cha juu zaidi cha usuluhishi wa michezo duniani.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mnguto, amesema tayari wamejibu barua ya Yanga na hawana mamlaka ya kuwazuia kwenda CAS lakini kama wameenda CAS kwa kipindi hiki ambapo hawajasema kuwa hilo suala limeamriwa vipi itakuwa ni kitu cha kuchekesha, akisisitiza kuwa maamuzi ya mwisho ya bodi bado hayajatolewa, akiamini kuwa suluhu inaweza kupatikana kupitia vikao vya ndani. Ameeleza kuwa busara na hekima zinapaswa kutumika ili kila upande uridhike badala ya kupeleka suala hilo nje ya nchi.

Chanzo: Mwananchi
Matumizi ya busara Ndiyo yamesabisha yanga sc waende mahaka ya usuruhishi CAS
 
Sidhani kama watu wengi wamemsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi; kimsingi amesema ile mechi imeahirishwa kwa busara ili Simba isishushwe daraja. Amesema inabidi busara itumike sababu timu zimelelewa vibaya toka zamani kwa hiyo kuna wakati kanuni lazima ziwekwe pembeni.
 
STEVEN MNGUTO: LAZIMA HEKIMA NA BUSARA ITUMIKE.

—[emoji2424] MWENYEKITI WA BODI YA LIGI STEVEN MNGUTO

(MSIKILIZE ZAIDI HAPO [emoji116][emoji116])

CC @mwananchi_official

" Hivyo ndivyo tunaweza kusema kuwa hekima na busara lazima itumike.....kanuni na Sheria ndio zipo lakini lazima pia hekima na busara lazima itumike.....huyo asiyetaka kutumia busara all out hayupo tayari kutatua tatizo means yupo kwaajila ya kuleta confusion ambayo Haina maana yeyote"""""

NB: Daah hii Ngoma ngumu ....bado yanga wanasukuma kete Kwa akili sana[emoji23][emoji23]
Screenshot_20250319-120311.jpg
 
Anasema kitu cha kuchekesha wakati moyoni anaogopa anajaribu kututisha sio 😅
 
Back
Top Bottom