Bodi ya ligi mmeingia kwenye mtego mbaya sana,,kitendo cha kuahirisha mechi bila sababu za msingi na kikanuni kitawagharimu!

Makavuli

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2024
Posts
1,425
Reaction score
1,829
Naona kabisa bodi ya ligi imetengeneza tatizo juu ya tatizo,,bodi ya ligi ilitakiwa isimamie Sheria na kanuni walizoziweka zinazoendesha ligi na sio busara!

Kanuni ziko wazi kwa timu inayogomea mechi na kanuni ziko wazi kwa timu iliyozuiliwa kufanya mazoezi aikuwepo haja yoyote ya kutumia ata dk 10 kuamua hili jambo kwakuwa kanuni zinajieleza!
Bodi imeahirisha mechi kuwaridhisha Simba sasa iyo mechi watayopanga Simba atacheza na nani? Yanga washatoa statement yao Iko very clear awatocheza mchezo mwingine zaidi ya huu wa Leo kwakuwa akuna sababu za msingi zilizopelekea mechi kuahirishwa!

Sababu zinazoweza kufanya mechi iahirishwe zinajulikana ambazo zinakuwa nje ya uwezo wa kibinadamu na sio timu kugomea mechi kwasababu imezuiwa kufanya mazoezi!

Yanga na wao awatopeleka timu uwanjani mpaka bodi iwaambie ni kanuni ipi waliitumia kuahirisha mchezo wa kwanza usifanyike!
Tatizo liko hapo na bodi aitokuwa na maelezo yanayoeleweka!
Bodi ya ligi walitakiwa kuchukua hatua bila kucheka na kima ili kukomesha Aya mambo lakini wamegeuka kusigina kanuni zao walizotunga wenyewe!

Vipi ingekuwa ni kengold au Namungo ndio wamegoma kwa stahili hii bodi ya ligi wangeahirisha mechi?
Sasa wametengeneza tatizo jingine na yanga awatocheza mechi nyingine ili tuone ni hatua gani watachukua kwakuwa washayakanyaga!
 
UBAYA UBWELA
KACHEZENI HATA NA YANGA QUEENS,NAYO NI TIMU PIA
 
wamekiuka kanuni zao wenyewe SURA VII 22 NA 24
Kanuni zao azifanyi kazi inapotokea mkubwa Mmojawapo amepuyanga lakini zinafanya kazi kwa timu nyingine tofauti na hizo timu 2,,Sasa kwa stahili hii bodi aitokuwa na meno Wala mamlaka ya kuiadhibu yanga ikigomea mechi kwakuwa kanuni zao wamezisigina na yanga atachukua reference ya mchezo huu kukataa vile vile na awatofanywa kitu!
 
saa saba za usiku ndio malalamiko yanatolewa halafu asubuhi kikao kinakaa !!hii bodi ya ligi iwajibike
 
Gheto mtakuja tu hata iwe lini
Mngetaka tuje msingetuhujumu tusifanye mazoezi,nyie ndio mmetuogopa,mlijua mkituhujumu hakutakuwa na mechi na ndio pona yenu,hivyo kimsingi nyie ndio mmetukimbia
 
Mngetaka tuje msingetuhujumu tusifanye mazoezi,nyie ndio mmetuogopa,mlijua mkituhujumu hakutakuwa na mechi na ndio pona yenu,hivyo kimsingi nyie ndio mmetukimbia
Yaan mechi imetangazwa miezi miwili mmekaa tu hamfanyi zoezi afu mnalia lia kwa kudhan siku moja itawasaidia?🤣🤣
 
Kama yanga mmesema hamtacheza mechi nyingne tofauti na hii sasa mnalalamika nn?
Mbona tumeshawasikia na tunaheshimu mawazo yenu nyie msicheze hiyo tar nyingne chezeni leo mtafute points zenu 3
 
Reactions: 7ve
Yaan mechi imetangazwa miezi miwili mmekaa tu hamfanyi zoezi afu mnalia lia kwa kudhan siku moja itawasaidia?🤣🤣
Kwa hiyo walioweka hiyo kanuni ya siku moja kabla ya mechi ni wajinga?

Acheni uhuni,fuateni taratibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…