Bodi ya Ligi yaijibu Yanga "Hakuna points 3 za bure"

Kwenye barua hawakusema kuwa sababu ya kuahirisha mechi ni sababu ya kiusalama bali wamesema ni sababu ya kupata muda wa kufanya uchunguzi wa ripoti ya afisa usalama.
 
Na huu ndio ukweli halafu kuna watu wanajilazimisha kuamini kuwa Yanga watapewa points 3 za dezo
Linapokuja suala la sheria na kanuni Yanga huwa wanajichanganya sana. Ukimsikiliza Karia Jana utaelewa kuwa Yanga wamejichanganya. Yale maneno yake ukiyasikiliza kwa kutulia utaelewa kuwa lawama zote za mechi kuahirishwa wanabebeshwa Yanga.
 
Kuokoa muda(ingawa sikubaliani na wewe)!

Hayo yote uliyosema yameshatokea, mechi imeahirishwa, sasa unapewaje point kwa mechi iliyoahirishwa?
 
Yale maneno yake ukiyasikiliza kwa kutulia utaelewa kuwa lawama zote za mechi kuahirishwa wanabebeshwa Yanga.
Ndiyo wanastahili lawama zote, maana wao ndio root cause ya yote hayo. Wasingezuia Simba kufanya mazoezi hayo yasingetokea, sasa kwa nini wasibebe lawama
 
Kuokoa muda(ingawa sikubaliani na wewe)!

Hayo yote uliyosema yameshatokea, mechi imeahirishwa, sasa unapewaje point kwa mechi iliyoahirishwa?
Achana na mambo ya Yanga kudai point 3, embu tujadili mpira kama watu wa mpira. Je wewe umeona walichokifanya bodi ya kukutana kumjadili aliyegomea mechi ni sawa? Kwani kanuni zimewekwa za nini kama mnakaa vikao vya dharura kwavitu ambavyo vinaongozwa na sheria na kanuni.

Umeona wenzetu Africa, chama cha soka cha Misri walivyo smart? Hawakuangaika kuitana bali wakaacha taratibu zote ziendelee kama zilivyo kisha mambo yote yataishia kwenye kanuni zao. Kwisha
 
Ndiyo wanastahili lawama zote, maana wao ndio root cause ya yote hayo. Wasingezuia Simba kufanya mazoezi hayo yasingetokea, sasa kwa nini wasibebe lawama
Wengi hasa mashabiki wa Yanga wanakwepa hii sababu kubwa na ya msingi, mabaunsa wa Yanga wasingewafanyia vurugu Simba haya yote yasingetokea
 
Bodi ya ligi nawaona kama mzazi aliyefeli maisha na bado umri unaruhusu anaamua kumsiginia kunguni mwanaye anayepambana na kuonyesha mwanga wa maisha
 
Yanga wahamie ligi ya zanzibar mpaka uongozi uliopo madarakani utakapomaliza muda wake
 
Kwa maoni yangu bodi ipo sahihi. Ilipata muda wa kuisikiliza timu iliyonyimwa haki ya kikanuni ikaridhika na kuahirisha mechi.

Mwanzo niliona kama viongozi wa Simba wamekurupuka. Baadae nikapata ripoti kwamba Fadlu aliwashauri viongozi kutopeleka timu uwanjani unless waende wakijua wanaenda kula za kutosha. Walikuwa wanaingia kwenye mechi bila kufanya mazoezi siku 2. Kwa hiyo tizi ya siku ile ilikuwa muhimu kwa utimamu wa miili ya wachezaji. Nawaunga mkono viongozi wa Simba kugoma.

Jambo la msingi kabisa hapa ni kuangalia sababu ya kushindikana kwa mechi-Yanga na mabaunsa wametukosea sana wana soka. Kama nitafanikiwa kuacha kufuatilia mpira wa Tz kama nilivyoamua basi sababu itakuwa ni Yanga kuachwa wafanye huu upuuzi
 
Mkuu wewe tulia huu mchezo auhitaji hasira ndio kwanza kumekucha,,yanga walisubilia kwa hamu wajibiwe na bodi ya ligi maana wasingeweza kusonga mbele kabla bodi aijajibu barua yao na kutoa sababu za kikanuni, sasa kama ni kweli wamejibu hivyo inavyoelezwa hapo kimaandishi na sababu zenyewe zikiwa ndio hizo Kuna jambo zito litakwenda kutokea uko mbeleni wewe tulia na yanga awawezi kupeleka timu uwanjani kwa stahili iyo!
 
Tuliwaambia humu,watageuziwa kibao sababu ya kiherehere chao!

Iwapo watagomea hiyo mechi no 184 kwa tarehe itakayopangwa basi wao ndiyo wataadhibiwa vilivyo!

Stay tuned.
 
Mkuu Wala usiumize kichwa chako na hili suala,,yanga walisubilia bodi ijibu barua yao na kama ndio wamejibu ivyo inavyoelezwa kuna kitu kizito kinakuja ni suala la muda tu itunze hii risiti
 

Unajua Simba ilipeleka ushahidi wa Video na barua maelezo kutishiwa usalama wake.
Mechi iliahirishwa Kwa sababu za kiusalama.

Ofisa usalama wa mchezo ambae ni polisi alipeleka ripoti kwa Bodi ya ligi

Hizo sababu mbili Ndio zilipelekea kuahirisha mchezo

Nanukuu

“” Kwasababu Bodi ya Ligi ilipokea taarifa ya usalama kutoka kwa ofisa usalama wa mchezo ambayo imeainisha matukio kadhaa yaliyo ambatana na tukio la club ya Simba kishindwa kufanya mazoezi na kwamba baadhi ya matukio yanahitaji uchunguzi ambao hauwezi kukamilika kwa wakati,Bodi ya Ligi kupitia Kamati yake ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi imeamua kuahirisha mchezo tajwa hapo juu””

Mwisho wa kunukuu.

Kaa tulia soma hii barua majibu utayapata,nimesoma hii barua zaidi ya Mara 10
 

Attachments

  • e3b8fcda-05ea-4f6f-9b3c-3ef54cca4792.jpeg
    66.5 KB · Views: 24
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…