Watetezi wa Yanga kwenye hili suala wanachekesha sana,kuna mchambuzi mmoja amesema kosa la Simba ni kutotoa taarifa hivyo wenyeji Yanga hawakujua kama wataenda kufanya mazoezi,alipoulizwa kama hawakuwa na taarifa hao mabaunsa wamepataje taarifa kuwa Simba wataenda uwanjani usiku ule kisha wakaenda kuwazuia akabaki anang'aa macho.Ameulizwa ni kanuni gani inataka timu mgeni iwasiliane na wahusika amebaki ooh sijui kuna miongozo,kaulizwa iko wapi miongozo,akadai iko TFF,kaja wakili Mgongolwa kamaliza ubishi kwa kusema hakuna cha miongozo kanuni inajitosheleza.Haya watetezi wa Yanga humu JF tuelezeni NI KANUNI NAMBA NGAPI INATAKA TIMU MGENI KABLA YA KWENDA KUFANYA MAZOEZI IWASILIANE NA WAHUSIKA?