Bodi ya Ligi yaijibu Yanga "Hakuna points 3 za bure"


1) Unasema Simba hawakufanya mazoezi siku 2 halafu unategemea mazoezi ya masaa kadhaa ndio yaongeze utimamu wa wachezaji tena kwa kwenda kuanza mazoezi usiku hilo ni uzushi na kama ni ukweli juu ya hilo basi kupitia ulichosema unanipa picha halisi ya kuwa Simba wametengeneza muvi ya kukimbia mechi na huenda hao wanaosemekana ni mabaunsa wa Yanga hawakuwa na uthibitisho kuwa ni wa Yanga.

2) unaweza kunionesha kwa mfano halisi ni lini iliwahi tokea Simba kwenda uwanja wa Mkapa kuelekea kwenye derby, kwaajili ya kufanya maandalizi ya mechi? Sikumbuki kama kuna huo utaratibu huo hapo kabla, ila kwanini ifanyike sasa sio mazingira ya ukimbiaji wa mechi?

3) Uwanja wa Mkapa unalindwa na walinzi wa serikali, hao mabaunsa hawawezi kuizidi serikali au maofisa wa mechi na mechi kama kuna kanuni inatakiwa kutekelezwa, lakini bodi ya ligi ilikiri wazi kuwa Simba hawakufanya mawasiliano na maofisa wa mechi wala meneja wa uwanja kwaajili ya kuwekewa mazingira rafiki, mbona hili linakwepwa kama moja ya sababu ya wao Simba kufanya uzembe? Tena hili la uzembe ndio chanzo kikubwa sana na ilipelekea hizo fujo zinazosemwa. Je vipi kama waliona wasitoe taarifa kwa wahusika ili mradi wasistukiwe muvi wanayocheza ya kupakazia mabaunsa wa Yanga kumbe ni sehemu ya wahuni waliowapa wenyewe maelekezo?

4) Sheria kama ipo ya timu inapofanya kosa la kumnyima mgeni kufanya mazoezi yake kwenye uwanja unaotumika kwa mechi, kulikuwa na haja gani ya kukutana kwa dharura?
 
Smt016 unadhani wanaostahili kulaumiwa kwa mechi kutofanyika ni Simba au bodi ya ligi?
Mbona hoja yangu ipo wazi tu, ni bodi ya ligi ndio wameonesha udhaifu sio Simba. Simba wao wameandika barua ila kwa vyovyote vile walikuwa wako tayari kwa lolote kulingana na maamuzi ya bodi ya ligi/ TFF. Hili swala hata ukiligeuza upande wa pili ( mfano Yanga ndio wangezuiwa kufanya mazoezi na Simba kisha kuamua kugomea mechi) bado maamuzi ya bodi ya ligi yangekuwa ndio hayo hayo tu ya kuahirisha mechi. Sheria na kanuni za kunyang'anywa point zipo tu kwaajili ya timu ndogo ila sio kwaajili ya Simba na Yanga.
 
Watetezi wa Yanga kwenye hili suala wanachekesha sana,kuna mchambuzi mmoja amesema kosa la Simba ni kutotoa taarifa hivyo wenyeji Yanga hawakujua kama wataenda kufanya mazoezi,alipoulizwa kama hawakuwa na taarifa hao mabaunsa wamepataje taarifa kuwa Simba wataenda uwanjani usiku ule kisha wakaenda kuwazuia akabaki anang'aa macho.Ameulizwa ni kanuni gani inataka timu mgeni iwasiliane na wahusika amebaki ooh sijui kuna miongozo,kaulizwa iko wapi miongozo,akadai iko TFF,kaja wakili Mgongolwa kamaliza ubishi kwa kusema hakuna cha miongozo kanuni inajitosheleza.Haya watetezi wa Yanga humu JF tuelezeni NI KANUNI NAMBA NGAPI INATAKA TIMU MGENI KABLA YA KWENDA KUFANYA MAZOEZI IWASILIANE NA WAHUSIKA?
 
Tarehe mpya itakapotajwa, Yanga mtuambie mapema kama hamtapeleka timu ili na sisi tusipeleke. Hatupendi kupoteza wese hovyo.
 
Taja kanuni iliyokiukwa na tff/ bodi ya ligi au kanuni iliyokiukwa na simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…