yaani ajira wanagawana wao maofisini, wanawekana ndugu kwa ndugu, ukija kwenye miundombinu nayo utakuta wanatengeneza barabara moja ya lami inaenda kwa kiongozi mmoja inaishia hapo..alafu maeneo ya wananchi waliowengi unakuta barabara za vumbi tu hawana habari.
Unakuta viongozi ni wezi, waongo...wanatumia magari ya serikali, wengine wanaiba na mafuta wanayoweka kwenye magari hayo...bado wanatengenezewa barabara za lami hadi majumbani kwao...lakini uswahilini barabara hazipitiki ni vumbi na makorongo......uchaguzi unakuja wanakuja uswahilini wanakwangua barabara wanaacha mavumbi wanataka muwape kura...waje tena wawaibie pesa tena, waibe mafuta ya magari ya serikali, wajichongee barabara za lami hadi majumbani kwao, waendelee kuiba tena..
Wameituma bodi ya mikopo kwenda uswahilini ambako kumechoka, barabara zimechakaa, waende wakadai pesa kwa watu ambao hawataki kuwaajiri wanataka wajiajiri ili hata kidogo wanachopata wawe busy kulipa madeni....na wao waendelee kujineemesha. Jamani jamani!. naamini wangewasaidia wawe wanaajiriwa kwa haki na upendo wangekuwa wanalipa madeni yao wenyewe bila kukumbushwa wala kusukumwa. Wezi wameshindwa kudhibitiwa huko juu, wanalindana na kauli zao za kuwaruhusu wale kwa ulefu wa kamba zao, maana yake hata ajira wawe wanawekana kwa undugu tu hamna shida, taifa langu linaangamia.
Mikopo wanajitahidi wengi wapate ila ajira wanataka ndugu zao tu ndio waendelee kuwekwa humo, kulipa deni anatafutwa yule ambaye hawahitaji kumuajiri ndio awe kipaumbele cha kurejesha deni....sawa kuna siku tutafika wanapopataka...itakuwa too late!!.
wasomi wetu lipeni madeni ya bodi ili watu wasome, waibe, na wajipendelee katika maendeleo yao!!