Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) yaja na 'Kampeni ya Fichua' kuwasaka wadaiwa sugu

Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) yaja na 'Kampeni ya Fichua' kuwasaka wadaiwa sugu

Ushauri wa bure kwa Raisi Samia
Wizara ya Elimu ndie Msimamizi wa bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu mwite Professor Mkenda mwambie kitu kimoja tu kuwa akuletee list ya wadaiwa wote ,majina yao na vyuo walivyosoma na course walizosoma na miaka waliyomaliza na madeni wanayodaiwa

Wakuletee ndani ya wiki moja mpe wiki moja tu yaani siku saba za kazi asije kuwa msabato au katoliki kuwa umemnyima uhuru wa kuabudu jumamosi au jumapili

Asipoleta mtimue uwaziri na hata ubunge asirudi chama kisimpe nafasi na uvunje bodi yote ya HESLB na Mkrugenzi mkuu mtimue na usimpe cheo chochote na wa chini watendaji waham8shie hata halmashauri za Tandahimba huko uchunguzi ukiendelea vyombo vyote vya dola
unawasikiliza na siasa hizo utawadai watu wakati hakuna kazi na hakuna mifumo mizuri ya uchumi kwenye nchi..mambo ya ajabu isee!
 
Kwa mfano mimi ndiyo rais wa nchi alafu hiyo bodi ya wapuuzi wanaongea kituko kama hichi nafuta kazi wote na uchunguzi unafanyika kwamba ilikuwaje wanadai watu wasiowafahamu anayehusika hata kama amestaafu atachukuliwa awajibike

Kwa mpango huu hii nchi itaendelea kuwa masikini mpaka dunia iumbwe tena hapo hakuna kiongozi anayeona kwamba hili ni tatizo
 
Bila kulipa wengine hawata pata mikopo
View attachment 3031540

Muwe na siku njema ,Kuwa hero wa Madogo .

Wekeni dau,mfano mseme mtoa taarifa, atalindwa na kila mtoa taarifa anaweza ama kushinda nyumba ya family size,gari ya angalao 30m,ama boda ama bajaji,kwa namna hiyo mtakuwa na mchango kwa jamii na kusaidia kupunguza ugumu wa maisha,hili ni sawa na TRA wanavyo kosa mapata,iwe ni kupitia rushwa ama kushindwa ubunifu mdogo mdogo kwa kisingizio cha sheria za kodi ambazo mara nyingi zina lenga kunufaisha ama kulinda makundi fulani fulani.
 
😆😆😆😆mdaiwa anadaiwa 13M wewe upewe 30m ?
 
Kuna mtu nafanya nae kazi dada yake anafanya huko Bodi ya mikopo akaniambia niandae laki 4 jina langu lifutwe nikazembea aloo msako ukaninasa nikalipa hela zote nimeshamaliza ila yeye hata sumni hakatwi nikajiona mjinga mimi
 
Back
Top Bottom