Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) yaja na 'Kampeni ya Fichua' kuwasaka wadaiwa sugu

Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) yaja na 'Kampeni ya Fichua' kuwasaka wadaiwa sugu

Kuna mtu nafanya nae kazi dada yake anafanya huko Bodi ya mikopo akaniambia niandae laki 4 jina langu lifutwe nikazembea aloo msako ukaninasa nikalipa hela zote nimeshamaliza ila yeye hata sumni hakatwi nikajiona mjinga mimi
😆😆😆😆
 
Mie nilimwambia magu kuwa hawa sio wakuwaongezea percent ya kulioa. Hawa ilikuwa unakamata na kunyonga tuu
 
Na majina hawajaweka waweke majina ya hao wadaiwa sugu na mwaka waliomaliza na chuo walichosoma na digrii walizosoma

Kuna taarifa kuwa walikuwa wakitoa mikopo hewa kwa wakopaji hewa zikiingia mifukoni mwao

Waweke list ya hayo majina na kiasi wanachodaiwa na ilete total ya hiyo pesa wanadai.Sababu kila jina na kiasi anadaiwa ukijumlisha lazima ilete hiyo jumla
Hawaweki sababu wanajua wana majina hewa wali create na kuyapa mikopo iliyoingia mifukoni mwao

Kusema tu watu wafichue ni utapeli

Wanaogopa nini kuweka wazi taarifa zao zote ? Vyombo vya habari ikiwemo website yao
Au watupeleke mahakamani!
 
Kazini wako kama wa-4 hawakatwi , mimi naona Safi tu, mlikopeshana wenyewe mtafutane wenyewe… snitches get stitches
 
Mimi nilipata boom baada ya kunji........ Nitafutene mpaka mnioate. Vinginevyo tukutane kwenye clearance ya kustaafu 2030
 
Back
Top Bottom