Bodi ya Nyama yasema Polisi waliteketeza nyama yote iliyokamatwa ila miguu ilichelewa kuungua ndio maana Meya wa Jiji aliikuta

Bodi ya Nyama yasema Polisi waliteketeza nyama yote iliyokamatwa ila miguu ilichelewa kuungua ndio maana Meya wa Jiji aliikuta

Ni aibu. Inabidi wazitapike kupitia kwenye matundu yote saba.
 
Aibu sana hii,
Kama kuna askari anasoma comment basi aone aibu kwenye nafsi yake, huwezi kulisha familia nyama ya dhuluma, aibu kubwa hii.

Bodi ya nyama mnaingia kwenye aibu, je nyama hiyo ilikuwa hatari kiafya? Kama jibu ni ndio je mlipima saa ngapi na kujua ni hatari kiafya? Kama haikuwa hatari kiafya kuna utaratibu wa kuteketeza kitu kisichokuwa hatari kiafya? Hicho kinapaswa kugawiwa kwa wananchi wa kawaida, vituo vya watoto yatima, shule, magereza n.k

Polisi oneni aibu hiyo laana ya kudhulumu watu haitawaacha salama.
Bodi ya nyama hakikisheni mnakula kile kilichohalali yenu msile vya dhuluma hamtakuwa tofauti na polisi kwenye kustaafu.
Itakuwa waliuza, eti miguu haiwezi kuwaka moto, inamaana sisi hatuchomi nyama? waongo wakubwa hao
 
ipo siku waungwana wataitia dawa ya kuharisha ndipo tutajua huwa inateketezwa au la
 
Bodi ya nyama nchini imesema siyo kweli kwamba polisi waligawana nyama iliyokamatwa vingunguti bali nyama yote iliteketezwa.

Mtendaji wa bodi ya nyama amesema wao ndio walioteketeza nyama hiyo pale kituo cha polisi Buguruni.

Kilichotokea ni kwamba nyama laini iliungua kwa haraka na miguu ambayo huchukua saa sita kuungua ilichelewa na alipofika Meya wa Jiji kuchungulia akaona kuna miguu tupu bila minofu na kidali ambayo ilishateketea.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Utaratibu wa kuteketeza chakula au bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu zikoje? Tuanzie hapo.....
 
IGP ana kazi kubwa sana ya kuimarisha kesho lake, na hapo atumbuliwi mtu mpaka bwana mkubwa atakapotoka huko alipo
 
Kazi yao kubambikizia kesi wananchi wa kawaida, ingekuwa maselule tu wakitaa tungenyea mbingu
 
Bodi ya nyama nchini imesema siyo kweli kwamba polisi waligawana nyama iliyokamatwa vingunguti bali nyama yote iliteketezwa.

Mtendaji wa bodi ya nyama amesema wao ndio walioteketeza nyama hiyo pale kituo cha polisi Buguruni.

Kilichotokea ni kwamba nyama laini iliungua kwa haraka na miguu ambayo huchukua saa sita kuungua ilichelewa na alipofika Meya wa Jiji kuchungulia akaona kuna miguu tupu bila minofu na kidali ambayo ilishateketea.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom