Bodi ya Nyama yasema Polisi waliteketeza nyama yote iliyokamatwa ila miguu ilichelewa kuungua ndio maana Meya wa Jiji aliikuta

Bodi ya Nyama yasema Polisi waliteketeza nyama yote iliyokamatwa ila miguu ilichelewa kuungua ndio maana Meya wa Jiji aliikuta

Nitawaamini Fisi kuliko Polisi kwenye hii Nyama
 
hhahaha embu madam aanze kaz araka lbd mambo aya yataisha
 
Bodi ya nyama nchini imesema siyo kweli kwamba polisi waligawana nyama iliyokamatwa vingunguti bali nyama yote iliteketezwa.

Mtendaji wa bodi ya nyama amesema wao ndio walioteketeza nyama hiyo pale kituo cha polisi Buguruni.

Kilichotokea ni kwamba nyama laini iliungua kwa haraka na miguu ambayo huchukua saa sita kuungua ilichelewa na alipofika Meya wa Jiji kuchungulia akaona kuna miguu tupu bila minofu na kidali ambayo ilishateketea.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote
 
Hivi polisi wana hiyo mamlaka?
Hivi utaratibu wa desposal ukoje? Najua inge teketezwa kwenye insenerator. Na sio kwa makaratasi.
incenerator hazipo kila mahali, kwa utaratibu polisi kazi yao Ni kusimamia tu Ila uteketezaji unafanywa na hao wahusika wenyewe waliokamata nyama.
 
Kwanini hawakwenda na wale wafanyabiashara wa nyama kushuhudia? hii issue imewakalia vibaya sana, shuhuda mmoja alisema aliwaona askari wakigawana nyama kituoni, na kwa njaa ya askari wetu kubambikia watu kesi mpaka wapewe chochote nakubaliana na shuhuda.
pia hakuna sheria au taratibu inayosema lazima mfanyabiashara awepo wakat wa uchomaji
 
Huyu jamaa wa bodi ya Nyuma hafai anataka kufanganya Kama sisi Ni watoto. Uchome ng'ombe mzima na karatasi. Aache ujinga. Hii mbuzi ipingwe chini irudi kijiweni nkutafuta maisha.
 
Back
Top Bottom