Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi yazionya Hospitali Binafsi kutokupokea Wagonjwa Wa dharura na Kuwa Discharge Wagonjwa mahtuti

Msajili hawezi kuzifungia hospitali kwa kugoma kuhudumia wagonjwa wa bima ya NHIF. Hapo zaidi zaidi NHIF ataanza ku terminate mikataba yake na hospitali za private, kisheria yuko sahihi kufanya hivyo. Long run naona wakija kuzifanyia changes hizo bei za kitita kipya na wakiongeza masharti magumu kwa watoa huduma ambao watataka kuomba upya mikataba ya NHIF. Watu wa policy huwa wanacheza tu na akili zenu.
 
Kwa hiyo outcomes mnazotaka ni zile za kuwapendelea nyie wahudumu WA afya Tu.
Sio kuwapendelea unajua walikuwa wanalipwa kiasi gani kipindi hicho MD alikuwa analipwa 600k

Bora baada ya mgomo Kikwete aliboresha Kufikia mpaka MD kulipwa 1.4Milion..

So kulingana na kazi wanazofanya Yes wanastahili na bado hicho ni kiasi kidogo sana..
 
Private hospitals ni wezi wanawaibia serikali na wateja kwasababu taarifa nyingi wanazojaza ni za uongo na kwasababu watanzania wengi hawana shule wao wanakubali kila kitu .
 
Taja mfano wa hiyo dawa ya sh. 30 bima ikalipa 5,000/=. Acha stori za vijiweni
 
Huko Umeenda mbali jiulize wale CO (Clinical officer) wa Hospitali za Rufaa za mkoa watafanyaje maana Kitita kimewatoa huko..
Ila Juzi wametoa Ajira wamewachagua kama 20 hivi
Hiki nacho ni kichekesho cha Karne. Inawezekanaje CO akaajiriwa RRH wakati ikama ya NHIF haitambui uwepo wake huko?!
Lengo lilikuwa nini?!
 
Nchi za dunia ya tatu, usicheze na aliyeshika mpini ukiwa umeshika makali utaumia tu.

Soon wataanza kulia.

Na hii haihusiani na nani yupo right, nani ypo wrong.

Ila namjua atakayelia ni nani mwisho wa hili game.
Atakayelia ni ambaye ameomba leseni ya biashara bila kujali wagonjwa watakaojifia bila hatia kwa kukosa huduma sababu ya ugomvi usiowahusu.
 
Udikteta haukuishia awamu ya 5

Hata hii awamu ya 6 ina udikteta pia
Tofauti ya udikteta wa awamu ya 5 na ya 6 ni yule anaeathirika na udikteta.

Awamu hii mnyonge ndio ananyooshwa na mfumo kisawasawa ila awamu iliopita wenye nazo ndio walikuwa wananyooshwa na mfumo ili kuleta fairness kwenye jamii.
 
Chief

Naomba unielimishe juu ya hili, kwanini unapopata matibabu ile form haiandikwi gharama za matibabu, matokeo yake unasaini tu bila kujua gharama halisi
 
Mnajua lakini bei mnazotetea? Ukivunjika mkono kurekebisha (reduction) na POP kuweka kituo cha afya 3,000/= Kushona kidonda 3,000/= (Nyuzi nyenhine pekee zinazidi bei hii kwa pc 1 tu). Na malipo yake utasuburi miezi nenda rudi wasikulipe.

Usishabikie jambo kabla ya kuona upuuzi gani umetendeka na NHIF


 
Sawa.
 
Chief

Naomba unielimishe juu ya hili, kwanini unapopata matibabu ile form haiandikwi gharama za matibabu, matokeo yake unasaini tu bila kujua gharama halisi
Kwa Hospitali Kubwa Ni vigumu kwa Daktari kufanya kazi ya kuandika gharama za matibabu..
Ila anapaswa kuandika matibabu aliokupatia..
Na unaruhusiwa kuhakika matibabu hayo..

Kazi ya kuandika gharama za Matibabu Ni kazi ya Medical Insurance officer..

Na chief nikutoe wasiwasi tu kuwa gharama za kila dawa NHIF ndo hutoa kitita kila miaka na wao ndo huamua dawa fulani iuzwe bei gani..

Huwezi kuandika Bei ya juu wala.ya Chini..

Hivi ni baadhi ya vitita vinavyomaliza muda wake 2016..

 
Hospital ya mirembe huwa tunachukua kwa bei hiyo ,, huwa tunamuona dokta ,sindano ya modicate pamoja na hizo tembe za cabamazapine za mwezi mzima ,garama huwa haifiki elfu 18 pamoja na kumuona docta ,

Mimi sio mtaalamu wa mambo ya afya ila awal tulikuwa tunatumia garama zaidi ya 50,000 elfu kila mwezi ,ila sasa garama zimeshuku ,,
Naweza nikawa nimekosea bei exactly ya tembe ,,ila ukitaka ntakuwekea screenshot ya garama zote tulizotumia kuanzia kumuona docta ,sindano na dawa hizo za mwezi mzima haikufika 18,000
 
Shukrani chief nimeelewa
 
Basi huenda kwa Mirembe kwa sababu ni Hospitali ya Taifa ya Mental Health huenda wanapokea Ruzuku ya Punguzo la Dawa..
ILa kwa sokoni haiko hivyo..

Tukumbuke Private haipati Ruzuku kutoka serkalini inajiendesha yenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…