Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi yazionya Hospitali Binafsi kutokupokea Wagonjwa Wa dharura na Kuwa Discharge Wagonjwa mahtuti

Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi yazionya Hospitali Binafsi kutokupokea Wagonjwa Wa dharura na Kuwa Discharge Wagonjwa mahtuti

Serikali ya ccm siku zote inatumia nguvu, sasa watasemaje mbele ya walala hoi(Siye). Wamezoea kutuambia mama anaupiga mwingi, sasa kwenye hili Serikali haitaki mjadala wanataka kutumia nguvu na blackmail. Serikali inatoa vibali na usajili wa hospitali binafsi zote nchini, hiyo ndiyo karata yake. Utasikia hospitali isiyotaka kupokea wagonjwa wa NHIF tutaifungia kutoa huduma, hawana jingine.

Jamani tuwe fair na biashara za wenzetu, kama serikali inaona hicho kitita ni kizuri na kinafaa, iboreshe Hospitali za serikali na wagonjwa wote waende huko, wakiwemo Rais, makamu,mawaziri wakuu, mawaziri, wabunge, yani wote bila kujali hadhi ya mpata huduma nasi wananchi wote twende huko hospitali za serikali.

Hospitali binafsi hawapati subsides kwenye vitendanishi, wala dawa. Hawanunui MSD. Huduma zao ziko ghali zaidi kwasababu ya gharama za vitendea kazi, na gharama za utoaji huduma pia. Hivyo NHIF iwalipe kulingana na huduma zao, siyo kuwalinganisha na hospitali za serikali.

Naungana nao kwamba waachwe wajitafutie wateja wa cash kama hawa wa bima hii ya NHIF hawalipi kulingana na huduma inayotolewa. Wanapotua huduma, wanapeleka bill kwa NHIF, hawa NHIF wanaanza longolongo kwenye malipo, utasikia tunahakiki, mara hatuwezi kulipa hii ni kubwa sana, kwanini ulifanya hiki na sio kile, sasa huo usumbufu wa malipo halafu unakuja baada ya huduma kuwa imeshatolewa, kama huko private ni gharama sana basi wenye bima za NHIF waende huko huko serikalini basi.

Kwanini kulazimishana?
Msajili hawezi kuzifungia hospitali kwa kugoma kuhudumia wagonjwa wa bima ya NHIF. Hapo zaidi zaidi NHIF ataanza ku terminate mikataba yake na hospitali za private, kisheria yuko sahihi kufanya hivyo. Long run naona wakija kuzifanyia changes hizo bei za kitita kipya na wakiongeza masharti magumu kwa watoa huduma ambao watataka kuomba upya mikataba ya NHIF. Watu wa policy huwa wanacheza tu na akili zenu.
 
Kwa hiyo outcomes mnazotaka ni zile za kuwapendelea nyie wahudumu WA afya Tu.
Sio kuwapendelea unajua walikuwa wanalipwa kiasi gani kipindi hicho MD alikuwa analipwa 600k

Bora baada ya mgomo Kikwete aliboresha Kufikia mpaka MD kulipwa 1.4Milion..

So kulingana na kazi wanazofanya Yes wanastahili na bado hicho ni kiasi kidogo sana..
 
Private hospitals ni wezi wanawaibia serikali na wateja kwasababu taarifa nyingi wanazojaza ni za uongo na kwasababu watanzania wengi hawana shule wao wanakubali kila kitu .
 
Ni aibu kuona magonjwa yamekuwa mtaji mbele ya baadhi ya binadamu!
Kwani kunashida gani hii fedha ikazunguka humo humo serikalini kwa kuanzisha vituo vya kutoa huduma hadimu kila wilaya!!? Maana ni upuuzi dawa ya 30 kwa kidonge unauziwa kwa 5000! Kuna maamuzi engine hayahitaji PHD au masters kuyatekeleza ni uamuzi tu na utendaji! Wapeni jeshi kitengo cha matibabu waje na plan kama huko bingeni hamuwezi!
Taja mfano wa hiyo dawa ya sh. 30 bima ikalipa 5,000/=. Acha stori za vijiweni
 
Huko Umeenda mbali jiulize wale CO (Clinical officer) wa Hospitali za Rufaa za mkoa watafanyaje maana Kitita kimewatoa huko..
Ila Juzi wametoa Ajira wamewachagua kama 20 hivi
Hiki nacho ni kichekesho cha Karne. Inawezekanaje CO akaajiriwa RRH wakati ikama ya NHIF haitambui uwepo wake huko?!
Lengo lilikuwa nini?!
 
Nchi za dunia ya tatu, usicheze na aliyeshika mpini ukiwa umeshika makali utaumia tu.

Soon wataanza kulia.

Na hii haihusiani na nani yupo right, nani ypo wrong.

Ila namjua atakayelia ni nani mwisho wa hili game.
Atakayelia ni ambaye ameomba leseni ya biashara bila kujali wagonjwa watakaojifia bila hatia kwa kukosa huduma sababu ya ugomvi usiowahusu.
 
Udikteta haukuishia awamu ya 5

Hata hii awamu ya 6 ina udikteta pia
Tofauti ya udikteta wa awamu ya 5 na ya 6 ni yule anaeathirika na udikteta.

Awamu hii mnyonge ndio ananyooshwa na mfumo kisawasawa ila awamu iliopita wenye nazo ndio walikuwa wananyooshwa na mfumo ili kuleta fairness kwenye jamii.
 
Weka mfano wa wizi waliofanya mkuu..
Nipo tayari kupokea kuuona..
Kama hujui kitu Ni bora kunyamaza unawezaji

kumuibia mtu anayekupangia bei ya kuuza,
Ukitibu anakagua Kila kitu na unatibu kwa kujaza Online bidhaa hiyo muda huo huo unapotibu, Unapata namba ya kukubaliwa kumtibu mgonjwa kwao (Authorisation number)..
Ukiandila madai yeye mdo anakagua na anaamua akulipe kipi..

Unapataje ujasiri Wa kusema private wanaibia Bima..
Nafikiri mtu kaam hujui jinsi hivi vitu vinavyofanya kazi ni bora kuuliza kwanza
Chief

Naomba unielimishe juu ya hili, kwanini unapopata matibabu ile form haiandikwi gharama za matibabu, matokeo yake unasaini tu bila kujua gharama halisi
 
Mnajua lakini bei mnazotetea? Ukivunjika mkono kurekebisha (reduction) na POP kuweka kituo cha afya 3,000/= Kushona kidonda 3,000/= (Nyuzi nyenhine pekee zinazidi bei hii kwa pc 1 tu). Na malipo yake utasuburi miezi nenda rudi wasikulipe.

Usishabikie jambo kabla ya kuona upuuzi gani umetendeka na NHIF

dcaa88b3-9255-4bf5-83dc-cfde38993734.jpeg

IMG_4384.jpeg
 
Ummy is way more intelligent than you think. Hapo hakuna tatizo atapata labda kama useme situation ingekuwa kwamba Madaktari kupitia chama chao MAT, wameigomea NHIF na kitita chao kipya, ndo ingekuwa na shida ila hapo wala hamna mtu ataingilia. Zaidi zaidi anyanyue macho aziandae hospitali za serikali na shifting kubwa ya wagonjwa watakaorudi kwenye public centres kama Janabi alivyofanya Muhimbili since jana.
Sawa.
 
Chief

Naomba unielimishe juu ya hili, kwanini unapopata matibabu ile form haiandikwi gharama za matibabu, matokeo yake unasaini tu bila kujua gharama halisi
Kwa Hospitali Kubwa Ni vigumu kwa Daktari kufanya kazi ya kuandika gharama za matibabu..
Ila anapaswa kuandika matibabu aliokupatia..
Na unaruhusiwa kuhakika matibabu hayo..

Kazi ya kuandika gharama za Matibabu Ni kazi ya Medical Insurance officer..

Na chief nikutoe wasiwasi tu kuwa gharama za kila dawa NHIF ndo hutoa kitita kila miaka na wao ndo huamua dawa fulani iuzwe bei gani..

Huwezi kuandika Bei ya juu wala.ya Chini..

Hivi ni baadhi ya vitita vinavyomaliza muda wake 2016..
Screenshot_20240302_102101_Adobe Acrobat.jpg

Screenshot_20240302_102135_Adobe Acrobat.jpg
 
Hebu niambie mkuu ulikonunua Kidonge cha Carbamazepine kwa Tsh 30 na mimi nikanunue huko nikaweke kwenye pharmacy yangu niwe Tajiri mkubwa maana cabamazepine kwa bei ya Jumla tu Bei yake ni Tsh 140 mpaka 170 kwa kidonge..

Nachukia sana Uongo aisee..

Bima mwaka 2016..Ilikuwa Tsh 200
View attachment 2921855
BIMA 2024 Tsh 138 bei ambayo.huuzwa Kwa bei ya Dukani yaani bei ya Jumla
View attachment 2921857


Nielekeze Duka wanakouza Carbamazepine kwa kidonge Tsh 30 Mkuu niwe Tajiri..
Maana vidonge 10 hapo nachukua 300..
Na hata nikiuza bei ya Bima ya Tsh 138 sina hasara..

Na ulinunua Olanzapine Wapi kwa Tshs 300 kidonge????

Natamani kupajua Ili na mimi nitibu wagonjwa wangu wa Mental health kwa bwerere kabisa
Hospital ya mirembe huwa tunachukua kwa bei hiyo ,, huwa tunamuona dokta ,sindano ya modicate pamoja na hizo tembe za cabamazapine za mwezi mzima ,garama huwa haifiki elfu 18 pamoja na kumuona docta ,

Mimi sio mtaalamu wa mambo ya afya ila awal tulikuwa tunatumia garama zaidi ya 50,000 elfu kila mwezi ,ila sasa garama zimeshuku ,,
Naweza nikawa nimekosea bei exactly ya tembe ,,ila ukitaka ntakuwekea screenshot ya garama zote tulizotumia kuanzia kumuona docta ,sindano na dawa hizo za mwezi mzima haikufika 18,000
 
Kwa Hospitali Kubwa Ni vigumu kwa Daktari kufanya kazi ya kuandika gharama za matibabu..
Ila anapaswa kuandika matibabu aliokupatia..
Na unaruhusiwa kuhakika matibabu hayo..

Kazi ya kuandika gharama za Matibabu Ni kazi ya Medical Insurance officer..

Na chief nikutoe wasiwasi tu kuwa gharama za kila dawa NHIF ndo hutoa kitita kila miaka na wao ndo huamua dawa fulani iuzwe bei gani..

Huwezi kuandika Bei ya juu wala.ya Chini..

Hivi ni baadhi ya vitita vinavyomaliza muda wake 2016..
View attachment 2922024
View attachment 2922023
Shukrani chief nimeelewa
 
Hospital ya mirembe huwa tunachukua kwa bei hiyo ,, huwa tunamuona dokta ,sindano ya modicate pamoja na hizo tembe za cabamazapine za mwezi mzima ,garama huwa haifiki elfu 18 pamoja na kumuona docta ,

Mimi sio mtaalamu wa mambo ya afya ila awal tulikuwa tunatumia garama zaidi ya 50,000 elfu kila mwezi ,ila sasa garama zimeshuku ,,
Naweza nikawa nimekosea bei exactly ya tembe ,,ila ukitaka ntakuwekea screenshot ya garama zote tulizotumia kuanzia kumuona docta ,sindano na dawa hizo za mwezi mzima haikufika 18,000
Basi huenda kwa Mirembe kwa sababu ni Hospitali ya Taifa ya Mental Health huenda wanapokea Ruzuku ya Punguzo la Dawa..
ILa kwa sokoni haiko hivyo..

Tukumbuke Private haipati Ruzuku kutoka serkalini inajiendesha yenyewe
 
Back
Top Bottom