Kinachoniogopesha zaidi ni hii kampeni yake ya industrialization, Kenya inategemea sana soko la EA katika kuuza bidhaa zake, hasa Tanzania na Uganda, kama Tanzania ikiwa na viwanda vyake, ni wazi Kenya itapoteza competitive edge ya viwanda, hasa ukizingatia kwamba production costs Tanzania zipo chini ukilinganisha na Kenya.
Jambo la pili ni jinsi Tanzania inavyozika kabisa utalii wa Kenya, kufufuka kwa ATCL, ujenzi wa biggest airport in EA, na kukataa kufungua Bologojo border point kati ya Serengeti na Masai mara, ni sawa na death sentence kwa utalii wa Kenya, hasa ukizingatia hali ya usalama wa Kenya.
Mwisho kabisa ni hii train ya umeme tunayojenga toka Dar hadi Kigali na Bujumbura, wafanya biashara wote toka Eastern DRC, Uganda na Rwanda wanaukujA Nairobi kununua bidhaa, itakuwa ni rahisi sana kwao kutumia passenger trains kuja Dar kununua mizigo na kurudi kw haraka, kuliko kutumia barabara au ndege ambazo ni ghali na sio reliable sana, Nairobi itakaukiwa sana na biashara.