Boeing wamefeli tena. Safari ya siku 8 imekuwa ya miezi 8

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
Ni habari yenye kuhuzunisha masaa kadhaa yaliyopita Boeing Starliner imeshindwa kuwarudisha duniani wanaanga wawili waliopelekwa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu, International Space Station (ISS)

Ikumbukwe kuwa wanaanga hawa Barry Wilmore (M) na Sunita Williams (F) walienda na Boeing Starliner June 6, 2024 na ilikuwa ni safari ya siku 8 tu.

Lakini mpaka kufikia sasa Boeing na NASA wameshindwa kuwarudisha kwa sababu ya hitilifu (technical issues) kwenye chombo hicho.



Boeing Starliner Space Capsule jana imerudi duniani bila wanaanga iliowapeleka

Kwa sasa Boeing na NASA zinashirikiana na SpaceX ya Elon Musk kuona jinsi ya kuwanasua wanaanga hao wawili. Ambapo inasemekana huenda kufikia February 2025 wataweza kuwarudisha. Safari ya wiki moja yawa ya miezi 8.

Boeing imekuwa na technical issues kwenye ndege zake na sasa hata kwenye spacecraft.

Mwaka 2011 Marekani iliizuia China isijiunge kwenye Kituo hicho cha Kimataifa cha Anga za Juu cha ISS na China ikaamua kuanzisha rasmi kituo chake cha anga za juu kinachoitwa Tiangong Space Station.

Kwa sasa kuna vituo viwili tu vya anga za juu cha Kimataifa na cha China.


Your browser is not able to display this video.

Wanaanga wa China wakifurahia kwenye Tiangong Space Station hawana wasiwasi wa kutorudi duniani

Je, ifike wakati NASA na Boeing waombe kushirikiana na China kuwanasua wanaanga wao?
 
Yani hii safari imekuwa ni shida, kwanza waliporuka ilibidi wakae kwenye orbit kuliko ilivyotegemewa kwa sababu thrusters 4 kati ya 12 ziliacha kufanya kazi. Sema space x itawarudisha na chombo kinarejea alone nadhani week ijayo. boeing naona kwa sasa inafail kila kona na sababu kubwa ni kwamba eti top management ilibadilishwa kutoka kuwa engineers ikawa watu wa biashara wanaoangalia zaidi faidi kuliko ubora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…