Marekani ni watu makini kwenye safety ya watu wake. Ndio maana OSHA ndio wao waliianzisha na ilikuwa chini ya mamlaka yao ya ajira, kabla hawajaifundisha na kuisambaza duniani. Vitu vingi sana unavyotumia kwenye usalama ni vya Wamarekani.
Huwezi walinganisha Wamarekani na Wachina ambao waliwahi kuuana mamilioni kwa mamilioni kila baada ya miaka kadhaa. Mara ya mwisho hapo Mao Zedong alisababisha njaa kuanzia 1959, njaa kubwa zaidi ya mwisho kutokea duniani wakafa Wachina zaidi ya milioni 30 kwa sera mbovu za kiongozi wao.
Kwanza kwa taarifa yenu Boeing Starliner imetua duniani salama kabisa kwa autopilot, na haikuwa na tatizo lolote hivyo hata wangekuja nayo hawa astronauts wawili isingekuwa shida. Boeing walihakikisha iko sawa, NASA hawakubisha ila walitaka kuwa na uhakika kabisa. Wamefanya hivi tabia za Kimarekani kuzingatia usalama.
Wachina waombwe msaada kwa lipi? Tueleze ni capsule gani ya Kichina inaweza dock pale ISS.