Boeing wamefeli tena. Safari ya siku 8 imekuwa ya miezi 8

Boeing wamefeli tena. Safari ya siku 8 imekuwa ya miezi 8

Basi nawe ungana kwenye swali la mwenzio. Ni capsule ipi ya China ita-dock pale ISS?

Au mnahisi space capsule ni kama lori la matofali la Kichina, leo unaamua utumie Howo kesho utumie FAW.
Ndio maana Mchina akaanzisha space station yake kuwapa jibu Marekani walidhani Mchina hataweza

Capsule ileile anayotumia kwenye TSS, Shenzhou
 
Satellite kutuma na internet kuanza ni vitu viwili tofauti. Kwa nilivyosikia nilijua wataanza mwakani internet, unless uniambie wameishaanza mkuu. Ujue nawafuatilia sana Wachina hasa CCTV
Kama satellite zimekuwa successfully delivered into orbit kinachofuata hapo ni ultra-reliable satellite broadband internet services
 
Ndio maana Mchina akaanzisha space station yake kuwapa jibu Marekani walidhani Mchina hataweza
Conclusion: Hakuna zaidi ya Mmarekani atakayeweza watoa wale stranded astronauts.
Nilitaka mjue hilo muache kujipa umuhimu, mnatisha watu humu mara Marekani aombe msaada Urusi mara China.

Alafu ISS haikuwa inamhitaji Mchina, hakukuwa na haja aingie project ishafika mbali. Mmarekani na Mrusi wanatosha na soon wanaachana. Ayo mambo ya wivu unasema wewe.
 
Conclusion: Hakuna zaidi ya Mmarekani atakayeweza watoa wale stranded astronauts.
Mchina anaweza kama anaweza kuwapeleka na kuwarudisha astronauts wake wa TSS atashindwaje wa ISS
 
Alafu ISS haikuwa inamhitaji Mchina, hakukuwa na haja aingie project ishafika mbali. Mmarekani na Mrusi wanatosha na soon wanaachana. Ayo mambo ya wivu unasema wewe.
Hiyo haikuwa sababu ya Marekani kumzuia Mchina fanya utafiti kidogo acha kudanganya watu humu
 
Kama satellite zimekuwa successfully delivered them into orbit kinachofuata hapo ni ultra-reliable satellite broadband internet services
Mpaka zitumwe satellites nyingi. Ndio maana hao Wachina wako hujaona wanauza internet service, kwa lugha nyepesi ni kwamba hakuna space internet ya Kichina hadi sasa. Na itaanzia kwao kwanza kabla kwenda kwingine
 
Ni suala la muda tu project iko tayari na mwanzo ni mzuri satellites zimeshatumwa soon Spacesail inakuja kumpa ushindani Starlink
 
Kwa kutumia space capsule ipi Mchina ataweza?

Yaani unaambiwa BMW X6 imekufa injini, unasema tutaweka ya Toyota Harrier Hybrid kisa nalo ni gari linatembea?
Shenzhou space capsule
 
Shenzhou space capsule
China hawana kibali cha kutua ISS, Urusi na Marekani hawajawahi wakagua wakawahidhinisha. Ingawa technically China iliwakopi Warusi docking system yao ambayo walishirikiana na Marekani kuitengeneza. Process za kuwaruhusu ni ndefu kama ambavyo iliwachukua muda SpaceX kuruhusiwa.

Mpaka huo muda wanakuja kuruhusiwa tiyari SpaceX imeishawarudisha astronauts.
 
China hawana kibali cha kutua ISS, Urusi na Marekani hawajawahi wakagua wakawahidhinisha.
Wakihidhinishwa wanaweza, tatizo wahidhinishaji wenyewe nao wamefeli kuwarudisha astronauts wao 🤣

Sasa kama wamenasa watawezaje kurudi February mwakani wangali hai 🙄
 
Process za kuwaruhusu ni ndefu kama ambavyo iliwachukua muda SpaceX kuruhusiwa.
Sasa China ajiunge kwenye ISS ya nini wakati wana ya kwao TSS

Picha ya juu mwonekano wa ndani wa Space station ya Mchina. Picha ya chini ya Marekani na washirika wake

Kuna moja hapo kama upo dampo la takataka
20240908_005004.jpg
 
Marekani ni watu makini kwenye safety ya watu wake. Ndio maana OSHA ndio wao waliianzisha na ilikuwa chini ya mamlaka yao ya ajira, kabla hawajaifundisha na kuisambaza duniani. Vitu vingi sana unavyotumia kwenye usalama ni vya Wamarekani.

Huwezi walinganisha Wamarekani na Wachina ambao waliwahi kuuana mamilioni kwa mamilioni kila baada ya miaka kadhaa. Mara ya mwisho hapo Mao Zedong alisababisha njaa kuanzia 1959, njaa kubwa zaidi ya mwisho kutokea duniani wakafa Wachina zaidi ya milioni 30 kwa sera mbovu za kiongozi wao.

Kwanza kwa taarifa yenu Boeing Starliner imetua duniani salama kabisa kwa autopilot, na haikuwa na tatizo lolote hivyo hata wangekuja nayo hawa astronauts wawili isingekuwa shida. Boeing walihakikisha iko sawa, NASA hawakubisha ila walitaka kuwa na uhakika kabisa. Wamefanya hivi tabia za Kimarekani kuzingatia usalama.

Wachina waombwe msaada kwa lipi? Tueleze ni capsule gani ya Kichina inaweza dock pale ISS.
Unaringia kudock ilihali wenzako wana ISS ya kisasa utafikiri upo hotel Verde zanzibar
 
Conclusion: Hakuna zaidi ya Mmarekani atakayeweza watoa wale stranded astronauts.
Nilitaka mjue hilo muache kujipa umuhimu, mnatisha watu humu mara Marekani aombe msaada Urusi mara China.

Alafu ISS haikuwa inamhitaji Mchina, hakukuwa na haja aingie project ishafika mbali. Mmarekani na Mrusi wanatosha na soon wanaachana. Ayo mambo ya wivu unasema wewe.
Mwenye wivu ni huyu aliyemnanga mwenzake asiwe kwenye space program
 
Back
Top Bottom