Boeing wamefeli tena. Safari ya siku 8 imekuwa ya miezi 8

Boeing wamefeli tena. Safari ya siku 8 imekuwa ya miezi 8

Wakihidhinishwa wanaweza, tatizo wahidhinishaji wenyewe nao wamefeli kuwarudisha astronauts wao 🤣

Kuidhinishwa siyo kuhidhinishwa. maana umeirudia mara mbili -wahidhinishaji (waidhinishaji). Ila sie tunaendelea kuwasoma
 
Mwenye wivu ni huyu aliyemnanga mwenzake asiwe kwenye space program
Yeye China space station yake amemleta nani pale? Naye tuseme ana wivu?

Mnachukulia space program kama sherehe za ngoma kwamba yeyote unamleta tu aje kulewa ulanzi. Mnaleta Uswahili kwenye mambo ya msingi😂
 
Unaringia kudock ilihali wenzako wana ISS ya kisasa utafikiri upo hotel Verde zanzibar
Ya kwao imeanza lini na ya Marekani & Russia imeanza lini?
Kuna gap ya miaka pale, si ajabu upcoming station ya Marekani itakuwa ya kisasa kuliko hii ya China. China kafundishwa na hao Wamarekani na Warusi, hata docking parameters kapewa, US & Russia almost wao ndio wameweka kila vipimo, standards, sheria, taratibu, wewe unakuja unalingia magodoro yaliyopo ndani eti ya Wachina ni ya kisasa.
 
Wakihidhinishwa wanaweza, tatizo wahidhinishaji wenyewe nao wamefeli kuwarudisha astronauts wao 🤣

"Wakihidhinishwa...."
Wachina hawahitajiki, mbona mna kisebengo na kujipendekeza kwa Marekani. Kila kitu mnafanya kumfurahisha ili muitwe. Hamuhitajiki, hamtoitwa.
 
Acha tuone T14 Armata anakwamba Marekani hawashindwi kuwarudisha hata kesho wakitaka ila wataachwa huko hadi Feb, 2025 kwa sababu za kiusalama
Space visits sio kama bodaboda yako ya Kichina unapiga kiki unaendesha.

Zina ratiba, na ratiba ya hivi karibuni ni ya SpaceX capsule kwenda uko. Ratiba ya kurudi ni ya Soyuz inayokuja na watatu, ratiba ya kuwarudisha hawa wawili ilikuwa ya hii Boeing na capsule ilirudi vizuri bila shida yoyote. Ingeweza kuwaleta vizuri tu ila hakuna uharaka.

Sasa wewe uko Majichumvi unalazimisha Marekani wafanye vitu kwa unavyotaka wewe, na hujui lolote kuhusu space.
 
"Wakihidhinishwa...."
Wachina hawahitajiki, mbona mna kisebengo na kujipendekeza kwa Marekani. Kila kitu mnafanya kumfurahisha ili muitwe. Hamuhitajiki, hamtoitwa.
Mchina hajawahi kujipendekeza kwa Mmarekani ndio maana ana version zake za kila tech.

Badala ya GPS ana BeiDou, badala ya google ana Baidu, badala ya google map ana Baidu Map,badala ya ISS ana TSS, badala ya Amazon ana Alibaba

Hiyo ni mifano michache tu
 
Ila wabongo bwana. Kwenye vita ya Russia na Nato huko Ukraine, wapo siti za mbele.

Kwenye Hamas vs Israel, wamo.

Kwenye kesi za afande, ni wao tuuuu.

Kwenye ngono, haachwi mtu

Huu muda watu wangekutumia kuwazia na kubishana kimaendeleo,taifa lingekuwa mbali
 
Ni habari yenye kuhuzunisha masaa kadhaa yaliyopita Boeing Starliner imeshindwa kuwarudisha duniani wanaanga wawili waliopelekwa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu, International Space Station (ISS)

Ikumbukwe kuwa wanaanga hawa Barry Wilmore (M) na Sunita Williams (F) walienda na Boeing Starliner June 6, 2024 na ilikuwa ni safari ya siku 8 tu.

Lakini mpaka kufikia sasa Boeing na NASA wameshindwa kuwarudisha kwa sababu ya hitilifu (technical issues) kwenye chombo hicho.

View attachment 3089234
Boeing Starliner Space Capsule jana imerudi duniani bila wanaanga iliowapeleka

Kwa sasa Boeing na NASA zinashirikiana na SpaceX ya Elon Musk kuona jinsi ya kuwanasua wanaanga hao wawili. Ambapo inasemekana huenda kufikia February 2025 wataweza kuwarudisha. Safari ya wiki moja yawa ya miezi 8.

Boeing imekuwa na technical issues kwenye ndege zake na sasa hata kwenye spacecraft.

Je, ifike wakati NASA na Boeing waombe kushirikiana na China kuwanasua wanaanga wao?
Hayakuhusu.

Jifunze kwanza kusuka ndondo za nchi 24 na kumwaga zege la barabara ili usimwite Mchina akujengee njia ya mwendo kasi.

Mwafrika, mvivu wa kujifanyia vitu wenyewe, tuna kamasi vichwani, tunaanza anzaje kukosoa ufundi wa BOEING ?
 
tatiba ya kuwarudisha hawa wawili ilikuwa ya hii Boeing na capsule ilirudi vizuri bila shida yoyote. Ingeweza kuwaleta vizuri tu ila hakuna uharaka.
Hakuna uharaka sio? Kwani lengo la safari yao ilikuwa wakae huko kwa muda gani? Lengo lilikuwa ni siku 8 tu utasemaje hawana uharaka
 
Hayakuhusu.

Jifunze kwanza kusuka ndondo za nchi 24 na kumwaga zege la barabara ili usimwite Mchina akujengee njia ya mwendo kasi.

Mwafrika, mvivu wa kujifanyia vitu wenyewe, tuna kamasi vichwani, tunaanza anzaje kukosoa ufundi wa BOEING ?
Pole lengo la uzi sio kuzungumzia Afrika
 
Ni suala la muda tu project iko tayari na mwanzo ni mzuri satellites zimeshatumwa soon Spacesail inakuja kumpa ushindani Starlink
As always China ni kama mbwa anayemfuata bwana wake lazima atanguliwe kila kitu na Marekani.

Kwenda kwenye mwezi Marekani kaenda 1969, China anaenda 2030s. Gap la miaka zaidi ya 60.

Kujenga space station US, Russia na washirika 1998. China 2021 hapo tofauti ya miaka 23.

Sasa na hapa unakuja na kauli za "soon". Soon nini bwana, China haina hiyo kitu usilete future tense.
 
Sasa China ajiunge kwenye ISS ya nini wakati wana ya kwao TSS

Picha ya juu mwonekano wa ndani wa Space station ya Mchina. Picha ya chini ya Marekani na washirika wake

Kuna moja hapo kama upo dampo la takataka
View attachment 3089818
We jamaa yani ya mmarekani uniita takataka hujui kila kitu happ sio screpa kila kitu kina kazi yake huo mdude ISS una kilo 450,0000
 
Mchina hajawahi kujipendekeza kwa Mmarekani ndio maana ana version zake za kila tech.

Badala ya GPS ana BeiDou, badala ya google ana Baidu, badala ya google map ana Baidu Map,badala ya ISS ana TSS, badala ya Amazon ana Alibaba

Hiyo ni mifano michache tu
Vyote hivi kavifanya baada ya Marekani kumtangulia, kaiga kwa Marekani.

Marekani yuko hatua mbele ya China. Alafu si ni wewe ulikuwa unalia unasema Marekani ilimnyima nafasi China kwenye space station? Mara tena unasema haijipendekezi.
 
As always China ni kama mbwa anayemfuata bwana wake lazima atanguliwe kila kitu na Marekani.

Kwenda kwenye mwezi Marekani kaenda 1969, China anaenda 2030s. Gap la miaka zaidi ya 60.

Kujenga space station US, Russia na washirika 1998. China 2021 hapo tofauti ya miaka 23.

Sasa na hapa unakuja na kauli za "soon". Soon nini bwana, China haina hiyo kitu usilete future tense.
Suala sio gap la miaka mingapi suala ni kuwa na technological independence kwenye tech ya kufanya jambo fulani

Mbona China imefika moon's far side ambako Mrusi na Mmarekani hawajawahi kufika
 
Hakuna uharaka sio? Kwani lengo la safari yao ilikuwa wakae huko kwa muda gani? Lengo lilikuwa ni siku 8 tu utasemaje hawana uharaka
Warusi waliopo sasa hivi wamekaa mwaka mzima, mbona husemi wana uharaka?

Warusi waliwahi kukaa zaidi ya mwaka ilikuwa 2023, hukuona uharaka?

Hawa Americans walienda kutest capsule mpya ya Boeing ili warudi nayo kutoa technical analysis. Hawajarudi nayo imekuja na autopilot, wao uharaka unauona wapi. NASA waseme hawana haraka, wewe na makoti yako vichochoroni udai wana haraka?

Bado unaendelea kujipa umuhimu bodi ya NASA.
 
Tunazungumzia Marekani na NASA jinsi wameshindwa kuwarudisha astronauts wao tuachane na habari za Warusi kwanza. Usijifiche kwenye kivuli cha Russia

Kama Marekani na Russia zimeshindwa basi kwa taarifa yako China haijawahi kushindwa kuwarudisha astronauts wao ndani ya ratiba

Kwa hiyo wote Marekani na Russia wana lesson kutoka China's space tech
 
Ni habari yenye kuhuzunisha masaa kadhaa yaliyopita Boeing Starliner imeshindwa kuwarudisha duniani wanaanga wawili waliopelekwa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu, International Space Station (ISS)

Ikumbukwe kuwa wanaanga hawa Barry Wilmore (M) na Sunita Williams (F) walienda na Boeing Starliner June 6, 2024 na ilikuwa ni safari ya siku 8 tu.

Lakini mpaka kufikia sasa Boeing na NASA wameshindwa kuwarudisha kwa sababu ya hitilifu (technical issues) kwenye chombo hicho.

View attachment 3089234
Boeing Starliner Space Capsule jana imerudi duniani bila wanaanga iliowapeleka

Kwa sasa Boeing na NASA zinashirikiana na SpaceX ya Elon Musk kuona jinsi ya kuwanasua wanaanga hao wawili. Ambapo inasemekana huenda kufikia February 2025 wataweza kuwarudisha. Safari ya wiki moja yawa ya miezi 8.

Boeing imekuwa na technical issues kwenye ndege zake na sasa hata kwenye spacecraft.

Mwaka 2011 Marekani iliizuia China isijiunge kwenye Kituo hicho cha Kimataifa cha Anga za Juu cha ISS na China ikaamua kuanzisha rasmi kituo chake cha anga za juu kinachoitwa Tiangong Space Station.

Kwa sasa kuna vituo viwili tu vya anga za juu cha Kimataifa na cha China.

View attachment 3089246
Wanaanga wa China wakifurahia kwenye Tiangong Space Station hawana wasiwasi wa kutorudi duniani

Je, ifike wakati NASA na Boeing waombe kushirikiana na China kuwanasua wanaanga wao?
Lengo la uzi lilikuwa ni hilo kwenye paragraph ya mwisho kabisa

Hongera sana China wameupiga mwingi sana kwa kweli
 
Back
Top Bottom