KERO Bomang'ombe-HAI: Viwanda Katikati ya Makazi, Nani Anahusika Kutoa Vibali?

KERO Bomang'ombe-HAI: Viwanda Katikati ya Makazi, Nani Anahusika Kutoa Vibali?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mji mdogo wa Bomang'ombe, uliopo Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, umekuwa ukikua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo, ukuaji huu umeletwa na changamoto kubwa ya uanzishwaji wa viwanda vidogo katikati ya makazi ya watu, jambo linaloathiri utulivu na maisha ya wananchi.

Kumekuwa na ukiukwaji wa sheria za Mipango Mji katika mji mdogo wa Bomang'ombe . Viwanda vidogo kama vya kufyatua tofali na kuchana mbao vimekuwa vikianzishwa katikati ya makazi, maeneo ambayo yamepimwa kwa ajili ya makazi ya watu tu .

Hali hii imesababisha:
  • Kelele za mashine zinazosumbua wakazi
  • Uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya makazi
  • Hatari za kiafya kwa wakazi wanaoishi karibu na viwanda hivyo
  • Kupoteza uhalisia wa mipango miji
Kinachotia wasiwasi ni kwamba, wakati watendaji wa mji wako bize kusimamisha ujenzi wa nyumba zinazojengwa bila vibali kwa kuandika "STOP-KIBALI CHA UJENZI", wanaacha viwanda vidogo viwepo kwenye maeneo ya makazi.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mazingira wakishirikiana na ofisi ya ujenzi wamekuwa wakitoa vibali vya ujenzi wa viwanda hivyo bila kuzingatia sheria za mipango miji.
  1. Je, mji mdogo wa Bomang'ombe hauna eneo rasmi la kuanzisha viwanda?
    • Kama lipo, kwa nini viwanda vinaanzishwa katikati ya makazi ya watu?
    • Kama hakuna, kwa nini eneo lisitengwe ili mji upangike vizuri?
  2. Kwanini watendaji wanasimamisha ujenzi wa nyumba na sio viwanda vidogo ndani ya makazi ya watu?
Kuacha viwanda katikati ya makazi ya watu kunajenga chuki baina ya watu na serikali . Hali hii inaweza kusababisha:
  • Migogoro ya ardhi baada ya muda, hasa wakati wananchi watakapotaka kiwanda kiondolewa
  • Upotevu wa fedha za wawekezaji ambao wamepewa baraka za kuanzisha viwanda katika maeneo yasiyofaa
  • Kudhoofika kwa imani ya wananchi kwa serikali na watendaji wake
Ushauri:
  1. Serikali itenge eneo maalum la viwanda nje ya makazi ya watu
  2. Watumishi wahusika warudi kusoma sheria zinazoongoza uanzishwaji wa mji mdogo
  3. Viwanda vilivyopo katikati ya makazi vihamishwe hadi maeneo yaliyotengwa
  4. Ufuatiliaji wa karibu ufanyike kuhusu utoaji wa vibali vya ujenzi wa viwanda
Ni wakati sasa kwa viongozi wa mji mdogo wa Bomang'ombe na Halmashauri ya Hai kuchukua hatua madhubuti kuhusu suala hili.

Ustawi wa wananchi na mpangilio mzuri wa miji ni muhimu kuliko maslahi ya kikundi au ya muda mfupi.
 
Mkuu nafikiri hapa unazungumzia kiwanda cha mbao cha seko karibu na idara ya ardhi pale, au kiwanda cha maziwa karibu na mahakamani au kile kiwanda cha mawe karibu na mahakama

Me huko ndo kwetu,
 
Mkuu nafikiri hapa unazungumzia kiwanda cha mbao cha seko karibu na idara ya ardhi pale, au kiwanda cha maziwa karibu na mahakamani au kile kiwanda cha mawe karibu na mahakama

Me huko ndo kwetu,
hivyo ni baadhi tu, vingine viko katikat ya makazi ya watu.
 
Back
Top Bottom